Ijumaa, 10 Januari 2020

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AWAPONGEZA UVCCM KWA KUENDELEA KUYAENZI MAPINDUZI YA ZANZIBAR KWA VITENDO

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AWAPONGEZA UVCCM KWA KUENDELEA KUYAENZI MAPINDUZI YA ZANZIBAR KWA VITENDO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika kilele Cha Matembezi ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ameipongeza UVCCM kwa Kuendelea kuwa Na Umoja na Mshikamano katika Shughuli mbalimbali za kukijenga Chama na Serikali.

Akizungumza katika Mkutano huo Mhe,Samia Suluhu amempongeza Mwenyekiti wa Umoja Wa Vijana Wa CCM Ndugu Kheri James na wasaidizi wake wote kwa namna Umoja huo ulivyo yaendesha matembezi hayo kwa kutoa michango ya nguvu kazi Katika maeneo mbalimbali ya kujenga Chama na Serikali kwa kujenga madarasa na Ofisi za Chama Cha Mapinduzi katika maeneo ambayo matembezi hayo yalikuwa yanapita.

Aidha, Katika Mkutano huo Mama Samia Suluhu amesema  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepiga hatua kubwa katika sekta mbalimbali  kutokana na misingi bora iliyowekwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar na Muasisi wa Mapinduzi Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,.

Mhe, Samia ameyasema hayo katika kilele cha kufunga matembezi ya Miaka 56 ya Maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar , ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yatakayo Tarehe 12 Januari 2020.

Amesema juhudi zilizochukuliwa na Muasisi huyo, zimeweka misingi bora ya upatikanaji wa masuala mbalimbali mfano katika Elimu nchini na kubainisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa elimu bure kwa wananchi wake pamoja na kuimarisha sekta hiyo kwa kuweka miundombinu bora ikiwemo kujenga Skuli za kisasa Zanzibar.

Ameongeza kuwa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Dk. Ali Mohammed Shein inajitahidi kuhakikisha watoto wote nchini wanapata elimu bora na katika mazingira bora kuanzia ngazi ya Maandalizi, Msingi na Sekondari ikiwa ni msingi wa kuendeleza malengo ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya kufuta ujinga kwa kuwapatia wananchi wake elimu bora.

Katika hatua nyengine, Mhe. Samia amewataka vijana nchini kutokubali kutumiwa  na watu wachache  wanaobeza Mapinduzi matukufu ya Zanzibar pamoja na juhudi hizo za Serikali badala yake waongeze bidii katika kusoma kwa manufaa yao na Taifa kwa jumla.

#Zanzibar
#Miaka56YaMapinduzi
#TogetherTunaweza
#MatembeziYaVijanaWaCCM

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni