#BARIADI :- DC BARIADI AMTEMBELEA MWANAFUNZILAMECK LUGEDENGA ALIEPATA A MASOMO YAKE YOT E TISA
Festo Kiswaga- DC Bariadi,Leo nimemtembelea kijana yohana lameck lugedenga aliyefaulu mtihani wa kidato cha nne kwa kupata A masomo yote tisa, kutoka shule ya igaganulwa kata ya dutwa wilaya ya Bariadi, mkoa wa Simiyu, . Hapa ndio nyumbani kwao. Baba yake mzazi kijana huyo alimtelekeza akiwa darasa la tano. Inasemekana alitokomea kusikojulikana kutokana na hali ngumu ya maisha lakini zaidi kukimbia majukumu ya kulisha familia yake. Hapa Chini ni nyumbani kwa mama yake Masalu Lulyalya . Picha ya Kwanza ni mimi na kijana huyu mwenye akili sana maana hata mtihani wa form two alipata A nane na B moja. Picha ya pili ni mimi na mama yake mzazi. Na picha ya tatu ni mimi, mama yake pamoja na bibi yake Mbuke Limbu. Niliposikia historia ya familia hii initia hamasa sana na kumshukuru sana Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli kwa kuleta elimu bure maana taarifa ni kwamba kijana huyu hata uniform za shule kwa miaka yote alikuwa ananunuliwa na walimu wake kwa vile alijulikana kwa kuwa na akili nyingi sana. Je isingekuwa elimu bure ingekuwaje kwa watoto Hawa kutoka familia masikini . AHSANTE DR JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI kwa maono ya hali ya juu kwa waTanzania wako Hawa. Yohana amexlelewa na mama yake pekee.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni