Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia kijana mmoja jina Alfred Kamugisha ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Kishaanda, Kata Kibale wilayani Kyerwa kwa tuhuma za mauaji ya Afisa wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kufanya vitendo vya ujangili.
Alfred anatuhumiwa kumuua Matondo Masunga Januari 6 mwaka huu kwa kumchoma na mkuki wenye sumu wakati akifanya shughuli za ujangili katika Hifadhi ya Rumanyika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni