KOMBORA LA MTAMBO WA DR. BASHIRU ALLY KAKULWA Katibu mkuu CCM Taifa leo wilayani Tanga limesambaratisha ngome ya CUF wilayani Tanga baada ya Waheshimiwa Madiwani 8 kujisalimisha mikononi mwa kamanda wa vita Mhe. Katibu Mkuu Dr. Bashiru.
*Madiwani hao ni* :-
1.Mhe. Mswahili Njama ( Chongoliani)
2.Mhe. Said Alei (Masiwani)
3.Habibu Mpa ( Ngamiani kati)
4.Mhe.Nassoro Salim (Tongoni)
5.Mhe.Akida Akida ( Ngamiani kaskazini)
6.Mhe.Mwanasha Abdallah ( Viti maalum)
7. Mhe. Thurekha Mahadh (Viti maalum)
8. Mhe. Haniu Ally ( NAIBU MEYA JIJI LA TANGA - Tangasisi).
*VIONGOZI* *WENGINE* :
9.Mhe. Mambea Pashua (Mwenyekiti wa CUF wilaya na mkoa wa Tanga)
10. Mhe.Hidaya Ahamed (Kampeni meneja CUF).
Mhe. Bashiru amewambia wanaccm kuwa amefunga mitambo mikali Wilayani Tanga, kiasi kwamba imelazimika kuwa na VITUO VIWILI VYA KUPOZESHEA MITAMBO HIYO. Kituo kimoja kimesetiwa Pangani na kingine hapa Tanga. Kwa hiyo ushindi wa jimbo la Tanga ni lazima katika jambo hili CCM haina utani.
Awali Mhe. Bashiru Ally jana aliongea na kupata chakula cha pamoja na wazee nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa, na leo alitembelea ofisi ya CCM wilaya , Mabalozi kata ya Majengo na kuzindua mpango wa vitambulisho kwa mabalozi wote wilayani. Na akatoa vitambulisho.
Aidha katika uwanja wa mkwakwani alisikiliza wimbo maalum wa KIKUNDI CHA SANAA CCM ikiwa ni agizo lake na kukabidhiwa CD kama zawadi toka IDARA YA SIASA NA UENEZI wilaya ya Tanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni