Alhamisi, 16 Januari 2020

MBUNGE WA ROMBO MR SELASINI AJIUZULU NAFASI YA MNADHIMU WA UPINZANI BUNGENI: Sasa msiseme ni njama za CCM.....

MBUNGE WA ROMBO MR SELASINI AJIUZULU NAFASI YA MNADHIMU WA UPINZANI BUNGENI:

Sasa msiseme ni njama za CCM.....

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesikitishwa na uamuzi wa Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini wa kujiuzulu nafasi ya Mnadhimu wa Upinzani Bungeni na kusema wazi sababu alizotoa hazina mashiko.

Mbowe ameshangazwa na taarifa ya Selasini kwamba hakuwahi kupewa Barua ya Uteuzi. Ameuliza, kama hakupewa barua ya uteuzi imekuwaje aandike barua ya kujiuzulu?.

Mbowe amesema, Selasini amekuwa Mnadhimu kwa miaka miwili, anaheshimiwa na Wabunge wote wa Upinzani huku akipewa ushirikiano wote na Ofisi ya Bunge, amekuwa akihudhuria Vikao vyote vya Kamati za Uongozi na kulipwa posho.

Kiongozi huyo Mkuu wa Upinzani Nchini ameonyesha wazi kutofurahishwa na uamuzi huo wa Mbunge Selasini na kusema labda kama ana mambo yake ya Siri ndiyo maana ameamua kufanya hivyo.

Mnasemaje wadau?😋😋🇹🇿

KOMBORA LA MTAMBO WA DR. BASHIRU ALLY KAKULWA Katibu mkuu CCM Taifa leo wilayani Tanga limesambaratisha ngome ya CUF wilayani Tanga baada ya Waheshimiwa Madiwani 8 kujisalimisha mikononi mwa kamanda wa vita Mhe. Katibu Mkuu Dr. Bashiru. *Madiwani hao ni* :-

KOMBORA LA MTAMBO WA DR. BASHIRU ALLY KAKULWA Katibu mkuu CCM Taifa leo wilayani Tanga limesambaratisha ngome ya CUF wilayani Tanga baada ya Waheshimiwa Madiwani 8 kujisalimisha mikononi mwa kamanda wa vita Mhe. Katibu Mkuu Dr. Bashiru.
*Madiwani hao ni* :-
1.Mhe. Mswahili Njama ( Chongoliani)
2.Mhe. Said Alei (Masiwani)
3.Habibu Mpa ( Ngamiani kati)
4.Mhe.Nassoro Salim (Tongoni)
5.Mhe.Akida Akida ( Ngamiani  kaskazini)
6.Mhe.Mwanasha Abdallah ( Viti maalum)
7. Mhe. Thurekha Mahadh (Viti maalum)
8. Mhe. Haniu Ally ( NAIBU MEYA JIJI LA TANGA - Tangasisi).

*VIONGOZI* *WENGINE* :
9.Mhe. Mambea Pashua (Mwenyekiti wa CUF wilaya na mkoa wa Tanga)
10. Mhe.Hidaya Ahamed (Kampeni meneja CUF).

Mhe. Bashiru amewambia wanaccm kuwa amefunga mitambo mikali Wilayani Tanga, kiasi kwamba imelazimika kuwa na VITUO VIWILI VYA KUPOZESHEA MITAMBO HIYO.  Kituo kimoja kimesetiwa Pangani na kingine hapa Tanga. Kwa hiyo ushindi wa jimbo la Tanga ni lazima katika jambo hili CCM haina utani.
Awali Mhe. Bashiru Ally jana  aliongea na kupata chakula cha pamoja na wazee nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa, na leo alitembelea ofisi ya CCM  wilaya ,  Mabalozi kata ya Majengo na kuzindua mpango wa vitambulisho kwa mabalozi wote wilayani. Na akatoa vitambulisho.
Aidha  katika uwanja wa mkwakwani alisikiliza wimbo maalum wa KIKUNDI CHA SANAA CCM ikiwa ni agizo lake na kukabidhiwa CD kama zawadi toka IDARA YA SIASA NA UENEZI wilaya ya Tanga.

Jumapili, 12 Januari 2020

#BARIADI :- DC BARIADI AMTEMBELEA MWANAFUNZILAMECK LUGEDENGA ALIEPATA A MASOMO YAKE YOT E TISA

#BARIADI :- DC BARIADI AMTEMBELEA MWANAFUNZILAMECK  LUGEDENGA ALIEPATA A MASOMO YAKE YOT E TISA

Festo Kiswaga- DC Bariadi,Leo nimemtembelea  kijana yohana lameck lugedenga aliyefaulu mtihani wa kidato  cha nne kwa kupata  A masomo yote tisa, kutoka  shule ya igaganulwa  kata ya dutwa wilaya ya Bariadi, mkoa wa Simiyu,  . Hapa ndio nyumbani kwao. Baba yake mzazi kijana huyo alimtelekeza  akiwa darasa la tano. Inasemekana alitokomea kusikojulikana kutokana na hali ngumu ya maisha lakini zaidi kukimbia majukumu ya kulisha familia yake. Hapa Chini ni nyumbani kwa mama yake Masalu  Lulyalya . Picha ya Kwanza ni mimi na kijana huyu mwenye akili sana maana hata mtihani wa form two  alipata A nane na B moja. Picha ya pili ni mimi na mama yake mzazi. Na picha ya tatu ni mimi, mama  yake pamoja na bibi yake Mbuke Limbu. Niliposikia historia ya familia hii initia hamasa sana na kumshukuru sana Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli kwa kuleta elimu bure maana taarifa ni kwamba kijana huyu hata uniform za shule kwa miaka yote alikuwa ananunuliwa na walimu wake kwa vile alijulikana kwa kuwa na akili nyingi sana. Je isingekuwa elimu bure ingekuwaje kwa watoto Hawa kutoka familia masikini . AHSANTE DR JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI kwa maono  ya hali ya juu kwa waTanzania wako Hawa. Yohana amexlelewa na mama yake pekee.

Ijumaa, 10 Januari 2020

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AWAPONGEZA UVCCM KWA KUENDELEA KUYAENZI MAPINDUZI YA ZANZIBAR KWA VITENDO

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AWAPONGEZA UVCCM KWA KUENDELEA KUYAENZI MAPINDUZI YA ZANZIBAR KWA VITENDO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika kilele Cha Matembezi ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ameipongeza UVCCM kwa Kuendelea kuwa Na Umoja na Mshikamano katika Shughuli mbalimbali za kukijenga Chama na Serikali.

Akizungumza katika Mkutano huo Mhe,Samia Suluhu amempongeza Mwenyekiti wa Umoja Wa Vijana Wa CCM Ndugu Kheri James na wasaidizi wake wote kwa namna Umoja huo ulivyo yaendesha matembezi hayo kwa kutoa michango ya nguvu kazi Katika maeneo mbalimbali ya kujenga Chama na Serikali kwa kujenga madarasa na Ofisi za Chama Cha Mapinduzi katika maeneo ambayo matembezi hayo yalikuwa yanapita.

Aidha, Katika Mkutano huo Mama Samia Suluhu amesema  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepiga hatua kubwa katika sekta mbalimbali  kutokana na misingi bora iliyowekwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar na Muasisi wa Mapinduzi Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,.

Mhe, Samia ameyasema hayo katika kilele cha kufunga matembezi ya Miaka 56 ya Maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar , ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yatakayo Tarehe 12 Januari 2020.

Amesema juhudi zilizochukuliwa na Muasisi huyo, zimeweka misingi bora ya upatikanaji wa masuala mbalimbali mfano katika Elimu nchini na kubainisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa elimu bure kwa wananchi wake pamoja na kuimarisha sekta hiyo kwa kuweka miundombinu bora ikiwemo kujenga Skuli za kisasa Zanzibar.

Ameongeza kuwa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Dk. Ali Mohammed Shein inajitahidi kuhakikisha watoto wote nchini wanapata elimu bora na katika mazingira bora kuanzia ngazi ya Maandalizi, Msingi na Sekondari ikiwa ni msingi wa kuendeleza malengo ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya kufuta ujinga kwa kuwapatia wananchi wake elimu bora.

Katika hatua nyengine, Mhe. Samia amewataka vijana nchini kutokubali kutumiwa  na watu wachache  wanaobeza Mapinduzi matukufu ya Zanzibar pamoja na juhudi hizo za Serikali badala yake waongeze bidii katika kusoma kwa manufaa yao na Taifa kwa jumla.

#Zanzibar
#Miaka56YaMapinduzi
#TogetherTunaweza
#MatembeziYaVijanaWaCCM

ALIYESHIKA NAMBA 1 KITAIFA KIDATO CHA NNE, HAJAWAHI KUONGOZA DARASANI.

ALIYESHIKA NAMBA 1 KITAIFA KIDATO CHA NNE, HAJAWAHI KUONGOZA DARASANI.

Mwanafunzi Tanzania One, matokeo ya kidato cha Nne yaliyotangazwa siku ya jana, Joan Ritte kutoka shule ya Sekondari St. Francis Girls, amesema hakuwahi kushika namba moja kwenye mitihani ya kawaida ya darasani. .
.
"Ilikuwa ni Mungu nimelelewa katika shule ambayo ina maadili ya Kikristo, walitulea kidini zaidi kutujenga kiimani kwamba tunaweza katika yeye atutiaye nguvu, sikutarajia kama nitashika namba moja ilikuwa 'surprise' kwa sababu hata REKODI yangu nikiwa shule sikuwahi kushika namba moja, na kuwapita wale waliokuwa juu yangu, nataka kuwa Civil Engineer"

Ndani ya mji wa Tunduma.

8~1~2020.
Ndani ya mji wa Tunduma.
Ktk kanisa la Mch mwakabenga lililo kata ya MAKAMBINI tulikutana viongozi wa chama cha Mapinduzi (ccm) wilaya ya Momba Pamoja na wenyeviti wa mitaa yote 71, watumishi mbali mbali wa serikali wakiongozwa wakiongozwa na Mhe mkuu wa wilaya Ndg. Jumaa Said Irando ikiwa ni utaratibu wa kawaida wa chama na serikali yake kukutana.

Pia chama cha Mapinduzi (w) Momba Tunamshukuru Baba Mch mwakabenga kwa hutubayake nzuri na ametufundisha kuto hofu ktk kufanya kazi za kuwatumikia wananchi akisema viongozi wote wametoka kwa Mungu, na Mungu ametupa upanga hivyo tutumie upanga huo kukata waovu, wavizu, wachongamishi, wasio itambua serikali tukate tuu! Nandio kazi ya upanga, ispokua upanga usiwaguse watu wema. WARUMI 13 (1-5).

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia kijana mmoja

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia kijana mmoja jina Alfred Kamugisha ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Kishaanda, Kata Kibale wilayani Kyerwa kwa tuhuma za mauaji ya Afisa wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kufanya vitendo vya ujangili.

Alfred anatuhumiwa kumuua Matondo Masunga Januari 6 mwaka huu kwa kumchoma na mkuki wenye sumu wakati akifanya shughuli za ujangili katika Hifadhi ya Rumanyika.

MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA WA CCM TAIFA NDUGU KHERI JEMES AKIZUNGUMZA NA WAAANDISHI WA HABARI AKITOA TAMKO LA KUELEKEA KILELE CHA MATEMBEZI YA MIAKA 56 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YALIYOJUMUISHA ZAIDI YA VIJANA 500 KUTOKA MIKOA YOTE YA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR.

MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA WA CCM TAIFA  NDUGU  KHERI JEMES AKIZUNGUMZA NA WAAANDISHI WA HABARI AKITOA TAMKO LA KUELEKEA KILELE CHA  MATEMBEZI  YA MIAKA 56 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YALIYOJUMUISHA ZAIDI YA VIJANA 500 KUTOKA MIKOA YOTE  YA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR. 

katika kikao hicho amewasihi vijana kuendelea kunga mkono kwa nguvu zote kwani mapinduzi hayo yamesaidia kuwakomboa wanyonge na kuwaomba vijana hao kuachana na maneno ya kejeli yanayotolewa na wasiotakia mema nchi yetu .

Pia Katika kikao hicho aliwaasa vijana kuendele a kuyaenzi  mapinduzi matukufu  kwani yalikuwa na malengo  makuu matatu   ambayo ni  kuenzi historia ya mapinduzi, utatashi wa kujiongoza wenyewe, kuwa na  kihakikisha rasili mali zilizokuwepo Zanzibar zinabaki kuwa ni rasili mali za wazanzibari wenyewe.

pia ameendelea kusema kwamba kwa kuyaenzi mapinduzi  umoja wa vijana hautakubali wala kuwafumbia macho wale ambao wanayabeza mapinduzi  hayo kwa faida zao na atahakikisha watambambana nao kwa namna yoyote ile kwani mapinduzi hayo yana faida kwa wananchi na yamesaidia katika kukuza miradi mbali mbali ya kimaendeleo.

#Viva vijana viva
#MAPINDUZI_DAIMA

Jumatano, 8 Januari 2020

WATAFITI MKO WAPI?

WATAFITI MKO WAPI? Ni muda muafaka kujitokeza ili muweze kuyawekea kumbukizi maajabu yake. Zifuatilieni nyayo zake kila akanyagapo ili muweze kugundua;
1. Uwezo wake
2. Miongozo yake
3. Kanuni zake
4. Ujasiri wake,
Pengine mtaweza kugundua maono yake kwa Nchi hii na kama yakifuatwa siku moja na kuendelezwa, naamini tutakuwa na maisha ya Paradiso angali tu DUNIANI.
Ni wachache sana wa aina yake katika historia mwenye uwezo wa juu " HYPERSONIC" aliyethubutu kufanikisha NDOTO KUWA KWELI.
Tusisubiri Wazungu kuyagundua haya. Tujivunie kuwa wa kwanza kuyagundua na kuyaandikia kupitia TAFITI.
KONGOLE MAGU

e Magufuli katekekeza wajibu au laahasha 😆😆😁 acha tuone

Je Magufuli  katekekeza wajibu au laahasha 😆😆😁 acha tuone

👇👇👇

-Tunataka Rais ambaye hataangalia sura (mnyika ) 2012 akiwa Morogoro 

-Tunataka Rais mkali asiye cheka Cheka namtu (Msigwa)  akiwa mbeya

-Tunataka Rais asiye safiri safiri kwenda nchi za nje akitumia Kodi za wtz (MBOWE)  akiwa kanda ya ziwa  2013

-Tunataka rais ambaye atakwa anausanya kodi za wtz na kuzitumia vizuri (Mbowe)  akiwa Tandahimba  2014

-Nchi hii unahitaji rais 👉 dicteta👈 na si vinginevyo (Lissu) akiwa Dar ES salaam😳

-Tunataka  rais ambaye atairudisha Nidhamu Serikalini (LEMA)  akiwa mbeya 2010

-Nchi hii inataka Rais atakaye inyoosha na wafunga Maafisadi (Heche)

-Tunataka Rais atakaye zilinda maliasili zetu (Msigwa)  akiwa bungeni 2013

-Nyalandu ni fisadi akiwa ccm (Nassary) akiwa bungeni 2012 tumefuna dume alipo Hamia cdm 2017 😎😆

-Nawashangaa wanaochoma moto vibaka na kumuacha fisadi lowasa akikamua mitaani Lowasa akiwa ccm (Mbowe)  2010 lowasa ni nabii(Mbowe) lowasa alipohamia cdm  2015  😊

-CCM wamempatia fisadi Lowasa FOMU ya kugombea urais ni hatare (Lissu)  Lowasa akiwa ccm Freb, 2015 Lowasa ni rais wa mioyo ya watu (Lissu)  baada ya lowasa kuhamia cdm 😳😆

-Nina ushahidi wa kutosha wa kuhusiana na wizi na ufisadi wa LOWASA (MNYIKA)  lowasa akiwa ccm Mwanaume aliye na ushahidi wa kutosha kuhusu ufisadi mnaomchafua mh. LOWASA  ampeleke mahakamani (MNYIKA)  baada ya LOWASA kuhamia cdm  😁😀

-Ni heshima kwa Mungu kumzomea na kumtukana mtu kama LOWASA kuwa ni fisadi  (LEMA)  LOWASA akiwa ccm
👉 sasa tuna tutaing'oa ccm madarakani wamekula nchi hii Sana wtz twende na mh Lowasa (LEMA)  baada ya lowasa kuhamia cdm 😂😋

-Anae muunga mkono fisadi lowasa akapimwe akili haraka (Msigwa)  March 2015 lowasa akiwa ccm
👉wtz tufike  wakati tukatae unyenyasaji huu wa ccm kula na kuzigawa kodi zetu ccm siyo watu kabisa mpe mh.  LOWASA  Kura ayabadilishe maisha ya wtz (Msigwa) baada ya LOWASA kuhamia CDM 😳😋

Nawauliza wananchi wa Tanzania kwa kauli hizo hapo juu za vigeugeu ukiwa na akili  timamu  Kabisa na ubongo uliyojaa jaakabisa unaweza kupugia chadema kura ya kuliongoza Taifa la Tanzania....

Kumbukumbu

👇

-Kiongozi wa  mwenye maarifa ya kuliongoza TAIFA hili atatoka ccm Baba wa TAIFA JK Nyerere 👏👏👏

-msije kuwapa warafi nchi baba wa TAIFA JK Nyerere  👏👏👏

Hivi maneno hayo wanayakumbuka naomba m-share yawafikie ili waone wtz siyo wajinga wanawachora tu 😀😁😁😁