Ijumaa, 1 Juni 2018

MAKOSA KATIKA MALEZI

Makosa 12 yafanywayo ktk malezi ya watoto ktk enzi tuliyonayo:    

1. Kutokuwa na ratiba maalum ya kula na kulala watoto.  Itatusaidia kujua tabia zao kwa kiasi fulani                   
2. Kutokupenda kuwatumikisha watoto hata kwa kazi ndogo ndogo wanazoziweza kama kufyeka majani majumbani mwetu.  

3. Kuwachia huru kutazama vyombo hatari vya mawasiliano kama simu na video bila usimamizi wa mzazi.                      

4. Kutofuatilia watoto mienendo yao ktk matembezi na maongezi na marafiki zao.           

5. Kutokupenda kula pamoja  wazazi na watoto. Wakiume kula na baba na wakike kula na mama. Mara nyingi baba huzungumza na watoto kwa muda mrefu baada ya kula.                       

6. Kutokuwa na tabia ya kufanya vikao vya kifamilia . Tuko mbele ktk kuandaa vikao vya kisiasi au kijamii kuliko vya ndani mwetu.         

7. Kutokuwazoesha watoto kushiriki shughuli impatishayo mzazi kipato. Mfano kama unauza dagaa kwanini mwanao asianue dagaa mbugani.                 

8. Wazazi kutokuwa pamoja watoto ktk  matembezi yao ya kawaida.             

9. Mzazi wa kike kumpinga au kutetea mtoto mbele ya mtoto pindi mzazi wa kiume anapomuonya/kumfokea mtoto ktk kumfundisha adabu.                    

10. Mzazi kutii masharti/matakwa ya mtoto kila anapotakiwa mtoto kufanya jambo.
                    
11. Mzazi kumwachia majukumu ya malezi wasaidizi wa nyumbani na wao kubaki na jukumu la kuwanunuĺia mahitaji yao tu yaani msaidizi ajenge akili ya mtoto mzazi ajenge mwilï. 

12. Wazazi kutoyapa umuhimu masomo ya dini kwa watoto.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni