Alhamisi, 7 Juni 2018

*HIZI NDIZO SABABU ZINAZOSABABISHA ULIPIE UMEME KWA GHARAMA KUBWA*.

*HIZI NDIZO SABABU ZINAZOSABABISHA ULIPIE UMEME KWA GHARAMA KUBWA*.

Unaweza kushangaa kuona *wengine wakinunua Umeme wa 9,150 Wanapata Unit 75 wewe ukinunua Umeme wa 10,000 unapata Unit 28.1*

Iko hivi, Watumiaji wadogo wa Umeme ambao kwa mwezi *Matumizi yao hayazidi Unit 75 Wapo Tarrif D1(4)* Na wanauziwa Unit moja kwa Sh.122,

Wakati watumiaji walio wengi wako Tarrif T1 hawa Unit moja wanauziwa Sh.kati ya sh.356.45 tu.

*Maana yake mtumiaji aliyeko Tarrif D1(4) Ananunua Unit 41 Kwa sh 5,000*
*Wakati walioko Tarrif T1 Wananunua Unit 14 kwa sh.5000*

NAWEZAJE KUWA MIONGONI MWA WATUMIAJI WADOGO WA UMEME YAANI (TARIFF D1)?

Kama ni nyumba ya kupanga na mko wengi ni ngumu kidogo. Kwanza unatakiwa Kupunguza Matumizi Ya Umeme Yasiyo ya Lazima
Pili nunua Vifaa vyenye Wats ndogo vitu kama taa, Tv, Friji, Pasi n.k

Tuchukulie mfano wa Taa zenye Wats 40 nje zikiwa nne na za Wats 18 kwa ndani zikawa Taa 8 nyumba yako nzima itakua na jumla ya Taa 12 Ambazo zitakua na Jumla ya Wats 304
Lakini ukinunua Taa zenye Wats ndogo *(*Energy Saver*) Japo bei yake iko juu kidogo ukilinganisha na Taa zenye Watts kubwa. Kwa mfano huu huu ukanunua Taa zenye Watts 5 kila moja za nje Nne na taa 8 za ndani zenye Wats 3 kila moja
Jumla ya taa 12 zitakua na Jumla ya Wats 44 tu.

Maana yake utakuwa umepunguza jumla ya Wats 250 upande wa Taa tu lakini idadi ya Taa imeendelea kuwa ni ile ile. Mtu mwenye taa moja ya Wats 40 akiwasha nawew ukawa taa zote 12 Matumizi yenu yatakua hayana tofauti kubwa
Mwisho kabisa, *matumizi yako ya Umeme yakiwa chini ya Unit 75 kwa miezi mitatu mpaka Sita Mfululizo*  unatakiwa kwenda TANESCO  Ofisi uliyo Karibu nayo kuomba kubadilishiwa Kutoka Tarrif 1 kwenda Tarrif 4.

*NB*: Hata baada ya kurudishwa Tarrif 4, Siku ukitumia zaidi ya Unit 75 kwa mwezi utarudishwa Tariff 1. Baadhi wanapopata fedha nyingi na hawana uhakika wa kuzipata tena kwa kipindi kirefu, huamua kununua umeme mwingi ili asihangaike kwa muda mrefu. Hilo ni kosa na mara Tanesco wanapoona "manunuzi"  yako ya Umeme ni makubwa wanakuhamishia kwenye Tariff kubwa bila kukupa taarifa. Hivyo, usifanye matumizi holela. ELIMU HII NI KWA HISANI YA SINGIDA REGIONAL CONSUMERS COMMITTEE (Singida RCC) - Kamati ya Watumiaji huduma za Nishati na Maji mkoa wa Singida.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni