*MBUNIFU WA JINA TANZANIA NA MATUMIZI YA JINA LETU LA MUUNGANO.*
Miezi mitatu baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana lilitangazwa shindano la kubuni jina litakalowakilisha hadhi na kuwepo kwa Muungano wa nchi mbili ,mshindi aliahidiwa zawadi ya shilingi 200 na Medali.
Kamati ndogo ya baraza la mawaziri iliteuliwa kupokea na kuchambua majina yaliyopendekezwa 1,534 na kuwasilisha machache ( idadi haifahamiki) kwenye baraza la mawaziri kwa uamuzi wa mwisho.
Inasemekana kuwa majina yalipokelewa kutoka ndani na nje ya nchi ,Zikiwemo Urusi, Uingereza Sweden ,Uchina ,Ufaransa , Poland ,italia, na Australia .katika mkutano na waandishi wa habari ,ikulu oktoba 29, 1964, Rais Nyerere alitangaza kwamba baraza la Mawaziri " limechagua jina Tanzania " kuwakilisha jamhuri ya Muungano, lakini hakutaja jina la mshindi..
Nyerere aliwafundisha pia namna ya kulitamka jina jipya kwamba ni " Tan- Zan- ia" sio " Tanzania" kama tunavyoita sasa,kati ya majina manne yaliyochuana mwisho na " Tan-Zan-ia" ni pamoja na " Tanzan" " Tangibar" na Zantan. Ifahamike wazi kuwa jina hili Tan-zan-ia .
Na mbali na kuzua mgongano na jina la Muungano (United Republic of Tanganyika and Zanzibar) kwa mujibu wa mkataba wa sheria ya Muungano lilikusudia kuwakilisha " Muungano na mambo ya Muungano ,lakini halikufuta muundo wa Muungano uliokusudiwa wala kufuta Serikali za Tanganyika na Zanzibar na mamlaka zake.
Mpaka miaka ya hivi karibuni mbunifu wa jina Tanzania wengi tunamfahamu, kwa leo ngoja tumuelezee kidogo kwa undani zaidi ,ili tupate kumuelewa zaidi na kuifahamu kumbukizi yake kwa ufasaha.
Aliitwa Mohamed Iqbal Dar ,ni kijana wa Marehemu Dkt Tufail Ahmed Dar ,mwenye asili ya kihindi ,alizaliwa Agosti 8 ,1944 mkoani Tanga, Baba yake alifahamika kama Dr. Dar. Alikuwa ni daktari kwenye mashamba ya mkonge ,Tanga .
Mwaka 1963 Mohamed Iqbal Dar ,alijiunga na shule ya Sekondari ya H.H. Aga khan mkoani Morogoro na mwaka 1964 alijiunga na Shule ya Sekondari ya Mzumbe Akiwa darasa moja na Mh. Shamim Khan.
Siku moja wakati yupo maktaba ya shule ya Mzumbe anasoma gazeti la "Tanganyika Standard " ( sasa Daily News) akiwa na miaka 18 alikutana na tangazo lililohitaji kubuni jina litakalounganisha majina ya Tanganyika na Zanzibar ili kuwakilisha Taifa moj.
Dakika tano baadaye ,akawa kashaandika jina lake mezani, anasema alichukua kipande cha karatasi akaandika Bismillah Raahman Rahim hii ni kutokana na imani yake ya dini.
Baada ya hapo akaandika jina la Tanganyika kisha akaandika jina Zanzibar halafu akaandika jina lake la Iqbal halafu akaandika jina la jumuiya yake la Ahmadiyya, washiriki kwenye shindano hilo walikuwa wapo 16.
Akachukua neno 'TAN' toka Tanganyika na 'ZAN' toka Zanzibar ,na kupata neno ' TANZAN' akaona halijakamilika vizuri, akachukua herufi ya kwanza ya jina lake ambayo ni 'I' katika jina lake la Iqbal kisha Akachukua herufi ya kwanza ya jina la dini yake ' AHMADIYYA , akaandika jina la Awali la ' TANZAN akaunga na herufi hizo na likawa ' Tanzania' akaona ni jina kamili tena zuri.
Kabla ya kulipeleka kunakohusika Serikalini alifanya utafiti kidogo na kugundua kwamba nchi nyingi za Afrika majina yake yanaishia na ' IA' kwa mfano Ethiop 'IA' ,Zamb 'IA' ,Tunis 'IA' ,Somal 'IA' ,Gamb 'IA' ,Namib 'IA' ,Liber 'IA' ,Mauritan ' IA' nk. Baada ya utafiti huo akapendekeza na kuamua kwamba jina la 'TANZANIA ' ndilo litumike kuwakilisha nchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar ,kwa maana majina manne ambayo ni Tanganyika, Zanzibar, Iqbal na Ahmadiyya.
Iqbal alipoliandika jana la Tanzania na kujiridhisha kuwa jina hilo linafaa alilituma kwenye kamati ya kuratibu shindano ,baada ya muda mrefu kupita Baba yake Dkt Dar. Alipokea barua nzito kutoka iliyokuwa Wizara ya Habari na utalii ilisomeka kama ifuatavyo; "
"Utakumbuka kuwa miezi michache iliyopita ulituandikia kutupa ushauri kuhusu jina jipya la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar......... Ili iitwe Tanzania,
Nafurahi kukutaarifu kuwa mshirikiane zawadi ya sh 200 iliyoahidiwa na leo nakuletea cheki ya sh 12/50 ikiwa ni hisa yako katika zile sh 200/=
Nashukuru sana kwa jitihada ya kufikiria jina la jamhuri yetu "
Barua ikasainiwa na Idrisa Abdul Wakili, Waziri wa Habari na Utalii kipindi hicho ,wakati ule alijitokeza mtu mmoja aliyeitwa Yusufal Pir Mohamed aliyedai naye alishinda ,hata hivyo, alikosa sifa baada ya kushindwa kutoa barua ya uthibitisho na kupongezwa kama alivyoandikiwa Iqbal na Serikali.
Iqbal ni mhandisi wa masuala ya Redio kazi anayoifanya huko Uingereza ,nyumba yake anayoishi huko Uingereza ameipa jina la Dar es salaam ikiwakilisha ubini wake, pamoja na jiji la Dar es salaam kuonyesha uzalendo wake.
Iqbal hakuwa maarufu na kufahamika toka miaka hiyo kwasababu alikuwa bado mwanafunzi wa miaka 19 alipoondoka na kwenda kuishi Uingereza eneo la Birmingham b35 6ps UK. Dar es salaam House,18 Turnhouse Roads, Mwaka 1964.
Muda ulisonga na baada ya miaka mingi kupita, jina lake halikutajwa wala kusikika kwenye rekodi yoyote ya historia za Tanzania, hakuna hata mmoja aliyemfahamu ,ilidhaniwa kuwa ni Mwl Nyerere ndiye aliyebuni jina la Tanzania ,lakini Iqbal akaandika barua Siku moja ili apate kutambuliwa Kwamba ndiye aliyebuni jina la Tanzania .
Akamwandikia Rais Ali Hassan Mwinyi na kipindi cha Rais Benjamin Mkapa lakini hakupata majibu yoyote, mwaka 2003 akaja nchini Tanzania lakini.
Hakupata kibali cha kuonana na Rais, akaamua kufanya mkutano na waandishi wa habari akiwa mkononi na vyeti na medali ,lakini pia alikumbana na maswali makali na kupata majibu hasi toka kwenye vyombo vya habari kuhusu madai yake hayo ,kuna wakati walimweleza inawezekana hata jina lake la Dar kalitoa kwenye jina la Dar es salaam.
Hadi Gazeti la serikali, Daily News, lilimkatalia madai yake ,akahuzunika ,baada ya kutopata mapokezi mazuri nyumbani kwake kama alivyotegemea.
Siku moja aliitwa na ndugu zake kutoka Uingereza na kumpa habari kwamba Rais Jakaya Kikwete pamoja na wabunge baada ya kwa uangalifu kupitia madai yake wanatarajia kumtangaza kama mtu aliyebuni jina la Tanzania, alilia sana kwa furaha , akaalikwa na serikali ili kuja kupongezwa ,lakini kutokana na Afya yake kuwa sio nzuri hakuweza kusafiri kuja Tanzania .
Mohamed Iqbal Dar akawaomba ndugu zake wampelekee salamu za ukunjufu kwa watanzania wote toka kwenye sakafu ya moyo wake na asante kwa serikali ya Tanzania kwa juhudi zao kufanya haki ya kumtambua yeye.
Watu wengi wanaamini kwa makosa kwamba Tanganyika na Zanzibar zilipoungana April 26 ,1964 ziliunda Muungano wa nchi inayoitwa Tanzania, ukweli ni kwamba tangu kuungana kwa nchi hizi mbili hadi miezi sita baadae hapakuwa na Muungano wala nchi iliyoitwa Tanzania na Muungano huo uliendelea vizuri.
Ndio kusema kwamba Muungano wa nchi hizi mbili haukuzaa Tanzania, wala Tanzania sio Muungano wa nchi hizi mbili.
Muungano uliofikiwa na kutiwa sahihi na waasisi wake ,Baba wa taifa Mwalimu Nyerere wa Tanganyika na Abeid Amani Karume wa Zanzibar hapo 1964, na kuridhiwa na mabingwa wa nchi hizi mbili kama mkataba wa kimataifa April 25, 1964.
Na kuwa sheria ( No. 22 ya 1964) kabla ya kutangazwa hapo April 26, 1964 unajulikana kama " Muungano wa Tanganyika na Zanzibar " hapajawa na Muungano mwingine zaidi ya huo na kwa jina tofauti na hilo.
Kufikia hapo wengi wanaweza kujiuliza kama hapajawa na Muungano mwingine basi jina hili " Muungano wa Tanzania " linatoka wapi? Marekebisho gani yalitokea hadi kufikia " Tanzania " badala ya " Tanganyika na Zanzibar"?.
Jina la Muungano huu limetajwa kwenye sheria ya Muungano kuwa ni " Muungano wa jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar " (URTZ) kuanzia Siku ya Muungano na baada ya hapo" ( sheria ya Muungano - kifungu cha 4)
Wakati nchi hizi mbili zikiungana hapakuwa na katiba iliyoandaliwa kusimamia muungano .kwa hiyo ilikubaliwa kuwa katika kipindi cha mpito
wakati muungano huo ukiandaliwa ,katiba ya jamhuri ya Tanganyika itumike pia kama katiba ya muungano kwa kufanyiwa marekebiaho kuingiza.
Yale mambo 11 yaliyopitishwa kushughulikiwa na serikali ya muungano na kuwepo kwa serikali ya Zanzibar ( sheria ya Muungano kifungu cha 5) ikumbukwe kuwa Zanzibar haikuwa na katiba yake wakati huo, hadi mwaka 1984, lakini ilikuwa na sheria zake zitokanazo na matamko ya Rais( decree).
Kwa kutambua serikali za Tanganyika na Zanzibar hazikufa baada ya Muungano, ikawekwa wazi sheria za Tanganyika na Zanzibar zitaendelea kutumika katika nchi hizo( kifungu cha 8 cha sheria ya Muungano na ibara ya 5 ya mkataba wa Muungano) bila kuingiliana na serikali ya Muungano.
Machi 24, 1964 bunge lilipitisha sheria namba 18 ya 1965 kuongeza muda wa kuitisha bunge la katiba hadi hapo itakapoonekana vyema kufanya hivyo.
Ili kuokoa MUUNGANO usiendelee kuchangia katiba na Serikali ya Tanganyika, julai 10, 1965 ,Bunge lilipitisha katiba ya muda ( sheria no.43 ya 1965) ya Tanzania iliyotambua kuwa " Tanzania ni jamhuri ya Muungano " ( ibara ya 1) inayoundwa na Tanganyika na Zanzibar ( ibara ya 2) na kwamba kutakuwa na chama kimoja cha siasa Tanzania ( ibara ya 3) lakini hapo TANU na ASP vitakapoungana ,chama cha siasa kwa Tanganyika kitakuwa "the Tanganyika African national union na kwa Zanzibar kitakuwa " Afro - Shirazi Party "
Hapo ndipo jina la Tanzania lilipoanza kuonekana kwenye katiba ya Muungano, na kuleta mgongano kati ya lile jina asilia la Muungano huo linalotambulika katika mkataba wa Muungano, na katika sheria ya Muungano ya mwaka 1964.mpaka sasa mkataba wa Muungano na sheria ya Muungano zinasomeka kama zilivyopitishwa mwaka 1964.
Pichani chini ni Iqbal akiwa na cheti chake cha ushindi wa ubunifu wa jina Tanzania, na medali yake alivyokabidhiwa na Serikali ya Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni