Jumanne, 14 Mei 2019

MAMA VANESAA SEHEMU YA 9

MAMA VANESAA

        SEHEMU YA 9

         WHATSAPP 0655585220

             ZANZIBAR

“Hapana mimi sitolala hapa nitaenda kulala kwa rafiki yangu, hicho nimekuchukulia wewe ili ukapumzike kama muda utakuwa umeenda sana. Sasa hivi tayari ni saa kumi na mbili sasa huoni kuwa utachelewa.

“Ni kweli lakini umewezaje kulipia chumba cha ghali hili hali huna kazi maisha yako yao hatariini huna pesa?”

Lilikuwa swali kumbwa ambalo hakulitarajia. Hapo alikosa jibu akanyamaza kimya huku simu yake ikiita na kuangalia alikuwa ni Kimaro akipiga. Alishindwa kuipokea na badala yake alitoa funguo na kumkabidhi mama Vanesa.

“Huko mikono salama nenda chumba namba tano badili nguo then urudi tupange mikakati na muda ukiruhusu basi utarudi”. Lucas safari hii alionekana kubadilika kidogo. Mama Vanesa hakutaka kupingana naye alijinyanyua hapo na kuanza kuelekea huko alipoelekezwa. Hapakuwa mbali sana hivyo alipiga hatua zake za madaha na kumuacha Lucas akimsindikiza kwa macho. Mmacho ya Lucas yaliendelea kukiri kuwa mwanamke huyo ni miongoni mwa wanawake wazuri na warembo huku duniani. Baada ya mama Vanesa kuondoka ilikuwa ni nafasi nzuri kwake kunynyua simu yake na kumpigia Kimaro. Kimaro alimweleza kuwa yupo eneo hilo na yupo na kimwana ..

“Upon a Julieth?Lucas aliuliza kwa kuhamaki.

“ Aaaaaah kwani umeambiwa kimwana ni Julieth tu.”

“Sijamaanisha hivyo ila ukimleta huyo atatuona sisi wote ni Malaya tu na imani yake juu yako itapungua.Lucasa alijaribu kueleza wasiwasi wake.

“ Ebu wacha maneno mengi nishafika hapa naingia umekaa kwa wapi?.

“Huku karibu na ziwa kabisa”

“Sawa dakika sufuri”.

Baaada ya nusu dakikaa Kimaro aliingia eneo hilo huku akiongozana na msichana mwingine ambaye yeye alimwita kimwana. Alikuwa ni mwanamke mrembo kwa maana nachelea kusema ni mzuri sana. Maana uzuri ni tofauti na urembo. Uzuri ni kitu ulichozaliwa nacho ni kutokana na uuumbaji wa Mungu. Urembo ni jinsi ulivyojitengneza kuanzia mwonekano, mavazi na mapozi. Alikuwa ni mwanamke mrembo na alivutia machoni pa Lucas.
“Yani huyu kwa kubadili wanawake kama nguo.. Sasa amempata wapi na huyu?” Lucas aliwaza mara baada ya kuwaona wakiingia kupitia boti ambalo lilikuwa linawavusha watu kutoka nchi kavu na kuwapeleka kwenye kisiwa hicho. Kilikuwa ni kisiwa ambacho hakikuwa mbali sana na nchi kavu na hakikuwa kikumbwa zaidi kilikuwa na hote hiyo na sehemu zilizojengwa kwa ajili ya utalii.. Aliwapungia mkono na wao walimwona. Hao kwa mwendo wa madaha kama mtu na mpenzi wake walijisogeza eneo hilo. Walifika na kuvuta viti kukaa. Walikuwa wenye furaha na waliochangamka sana. Kwa kuwa viti vilikuwa ni vichacahe n kilea alichokuwa amekalia mama Vanesa kilishatumika ilimlazimu kumwita muhudu ili awasikilize wageni na aongeze kiti kimoja.

Muhudumu aliwasikiliza na kwenda kuchukua vinywaji. Mara Mama Vanesa naye alikuwa akija kutoka kwenye hotel. Alichukua muda mrefu lakini haikuwa tatizo kwa Lucas maana anajua kabisa wasichana linapokuja swala la kubadili nguo lazima waanze kujiremba upya. Ni kweli maana mama Vanesa alikuwa amebadilika kabisa na kuzidi kuonekana kuwa alikuwa ni msichana mdogo. Alivaa kimini kilichofanya kuacha mapaja yake nje. Alionekana ni binti mdogo pengine waweza kusema ni msichana amabye hajaolewa. Lucas hakujua kwa nini amevaa hivyo lakini huenda labda aliamua kujiachia mara baada ya kuhisi kuwa watakuwa wawili tu. Hakujua kama kuna wageni wanaweza kuja. Hata hivyo hakuonesha kushtushwa sana alivuta kiti na kukaa. Kimaro aliyatumbua macho na hakuamini kama huyo ndo mke wa boss ambaye alikuwa akizungumziwa..

“Habari zenu” Mama Vanessa alitoa salamu ya jumla.

“Nzuri” Kimaro na kimwana aliyekuja naye walijibu kwa pamoja.Kimya kikatawala kidogo kabla ya Lucas kuvunja ukimya.

“Mama Vanessa huyu anaitwa Kimaro ni rafiki wangu wa kufa na kuzikana. Mr Kimaro huyu ndio mama Vanessa mwanamke aliyeamua kuniokota mara baada ya Mishel kunitupa.

“Nashukuru sana bwana Lucas nashukuru pia kumfahamu mama Vannesa..Kimaro aliongea huku akimpa mkono mama Vanessa. Alifanya utani wake kidogo kwa kuubinya mkono kwa nguvu jambo lilofanya mama Vanesa ahisi maumivu.

“Aiseee kweli unastahili hili kuitwa mrembo mikono laini kama maini” Kimaro aliongea huku akionesha kushangaa.

Wote kwa pamoja walicheka na kufanya kuchangamka. Muhudumu alikuja tena na kumleta kinywaji mama Vanesa. Safari hii alibadilisha na kuanza kunywa wine. Stori mbili tatu za kuchekesha ziliendelea na kufanya muda kuzidi kuyoyoma. Kimaro alitumia muda huo vizuri kuwafurahisha na kuwachekesha kwa sababu moja ya vitu alivyojaliwa ni kuwafurahisha watu na kuwafanya wamsikilize kwa muda mrefu.
Wakati stori zikiendelea mama Vanessa yeye alikuwa ulimwengu mwingine kabisa. Alikuwa akiwaza ni jinsi gani atarudi Musoma hili hali muda ulikuwa umeenda sana. Aliendelea kunywa kinywaji huku akili yake ikifanya kazi ya ziada juu ya uwongo gani afanye ili mme wake amuelewe. Yaani mama Vanesa alikuwa ni mwanamke wa ajabu sana huku duniani kwa sababu ingawa mme wake alikuwa akimtenda vibaya kila mara lakini hakuwahi kuwa mkaidi. Siku zote amekuwa mtiifu na amekuwa akijishusha. Haya yote aliyafanya kwa sababu alitokea kwenye familia masikini. Alijifanya kipofu kwa kwa mabaya yote ambayo alikuwa akitendewa na mumewe. Lakini alikuwa na lake moyoni kwa kuwa muda huo yeye kujifanya boya ulikuwa umekwisha. Tayari alikuwa ameshachuma mali za kutosha. Alishajenga kwao na alishakuwa na nyumba mjini. Mumewe alimwamini sana na hakujua kuwa ipo siku atabadilika.

“Mbona mama Vanesa anaonekana kama mwenye mawazo?”Kimaro aliuliza mara baada ya kuona huyo ametulia tu.

“Hamna mimi sina mawazo yoyote tupo pamoja” Mama Vanesa alisema huku akitaka kusema kuwa anataka kuondoka. Ila aliamua kujiuliza maswali na kujijibu mwenyewe.Sasa nitaondokaje na kilichokileta huku sijakipata. Hata hatujaweka mikakati ya kumkomesha baba Vanesa. Ilibidi amuandikie sms Lucas kumueleza nia yake ya kutaka kuondoka. Lucas na yeye alimuuliza swali lile kuwa sasa ataondokaje wakati bado hatujapanga mikakati. “Mimi naona utafute njia ulale kwa sababu tayari chumba kipo.Lucas alishauri na wakati huo huo Lucas pia alianza kuchati ana Kimaro kumwambia kuwa mama Vanesa anataka kuondoka. Kimaro akasisitiza kuwa hilo haiwezi kutokea kama yeye yupo.

“Inaoenkana watu mmekaa kiunyonge nyonge sasa napendekeza tuhame kwa muda kuna mahali nasikia kuna nyama choma twendeni tukale.” Kimaro aliongea huku akiinuka na kumpa mkono msichana aliyekuja naye kisha kuanza kupiga hatua na kuondoka. Lucas alitamani kucheka lakini alijikausha na yeye akafanya kumpa mkono Mama Vanesaa.

“Leo upo na vijana wenzako huna haja ya kuwa na wasiwasi. Sahau hata mawazo ya kuumizwa kimapenzi na baba Vanessa..

“Ni sawa lakini nitamwambia nipo wapi au nimelala wapi.

“Kwanini yeye anavyoondokaga na kulala nje ya ndoa huwa anakwambai ukweli kuwa amekwenda kukusaliti?

“Hapana”

“Sasa na wewe tafuta uwongo mtakatifu”
Ilibidi na wao waanze kupiga hatua na kuondoka eneo hilo. Walivuka tena na boti na kutoka nchi kavu. Lucas alikuwa ameenda na gari hivyo waliingia kwenye gari. Mama Vanesa licha ya kuwa alikuwa amechoshwa na tabia za mumewe lakni pia mumewe alikuwa hana uwezo wa kumrizisha kitandani. Huo ulikuwa ni ukweli ambao haupingiki kuwa mume wake hakuwahi kurizisha hasa siku hizi za karibuni ingawa kipindi kile wameanza uhusiano wao alikuwa akifurahia. Alichokifanya mama Vanesa ni kuzima simu na alimtumia sms mume wake kuwa simu yake inazima chaji. Hakumwambia kuwa hatorudi nyumbani wala nini. Waliondoka na kuenda hiyo sehemu ambayo Kimaro alisema. Mama Vanesaa aliamua kuamishia mawazo yake kwenye kujipa raha usiku huo. Mpaka muda huo alikuwa hajaelewa kama Lucas anampango wa kulala naye au ndo kama vile aivyomwambia. Na kama atalala mwenyewe basi kuna umuhimu gani wa kufanya hivyo.

Waliingia sehemu ambayo palikuwa pamechangamka sana. Ilikuwa ni sehemu ambayo ilionekana ni ya gharama maana muziki laini ulikuwa ukiimbwa live. Ingawa nyimbo zilizokuwa zikiimbiwa zilikuwa ni nyimbo za zamani lakini ziliwavutia. Haraka haraka waliagiza na kuendelea kunywa huku wakisubri nyama choma. Hapo hapakuwa ana longolongo ya kusubiri muda mrefu. Nyama zilikuja na wakaendelea kula.Wakaendelea kula na kunywa.Wote walizidi kuchangamka na wakajikuta wanatamani kucheza musiki. Lucas na Kimaro wakawa tayari wamepanga mambo hayo. Akaanza Kimaro kuamka na kumchukua huyo mwanamke aliyekuwa naye na kuanza kucheza naye. Lucas na yeye akajifanya kuwa uzalendo umemshindwa.Alimnyanya mama Vanessa na kuanza kucheza naye musiki.

Walianza kucheza huku Kimaro alikuwa akirekodi lile tukio na kuchukua picha. Lengo ilikuwa ni kulipiza kisasi kwa kumrusha roho boss. Lucas alijifanya amelewa maana alikuwa akicheza na mama Vanesa kama mtu na mpenzi wake.Burudani iliendelea mpaka mida ya usiku. Kwa kuwa Kimaro siku hiyo hakutaka kukaa sana waliamua kuondoka . Waliingia kwenye gari na kitu cha kwanza walichofanya ni kuwapeleka Lucas na Mama Vanesaa kwenye ile hotel ambayo walikuwa wao mwanzo. Tayari kamera ziliwekwa kwa ajili ya kuwarekodi. Kamera ziliwekwa kisiri mradi tu kupata picha za matukio ambayo kama boss wake akiziona basi lazima atakufa kwa presha. Lucas safari hii alibadilika alikuwa tofauti kabisa na mwanzo hakuwa mtu wa kujadiliana zaidi aliongoza mpaka pale kwenye chumba walichokodi. Vitu vya mama Vanesa vilikuwa humo na hivyo kwake yeye ilikuwa ni faida lazima mwanamke huyo angeingia humo.

Waliingia wote na Lucas alifunga mlango kisha akajitupa kitandani. Alijifanya kuwa alikuwa akisikia vibaya na pombe zilikuwa zimemzidi hivyo alihitaji kupumzika. Mama Vanesa alisimama kama mlingoti kisha akatupa swali la kizushi.

“Kwa hiyo Lucas unataka kulala na mke wa boss wako chumba kimoja”

ITAENDELEA………………………………

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni