Jumanne, 14 Mei 2019

MAMA VANESSA SEHEMU YA 7

MAMA VANESSA

          SEHEMU YA 7

             WHATSAPP 0655585220

                 ZANZIBAR

Kwa kuwa ndani kulikuwa na joto alirudi zake nje na kuendelea kutafakari mustakabali wa maisha yake. Roho iliendelea kupwitapwita kwa kuuma na kutamani kama angekuwa na nguvu ya kupambana na huyo boss. Pamoja kuwa wana pesa sitokubali kwa njia yoyote ile nifukuzwe kazi. “Afanye yote lakini sitokubali kwa maana kama anatembea na mke wangu na mimi nitatembea na mke wake. Sio mke wake tu hata mtoto wake. Nipo tayari hata kufa lakini sio kudhalilishwa kwa kiasi hiki kikumbwa. Mke anauma sana na sijui kwa nini nimeweza kuvumilia kwa kipindi chote hicho. Nitaenda hata kwa mganga kumloga. Maisha ndo haya haya kwa kweli sipo tayari kwa namna yoyote ile kudhalilika kisa madaraka au pesa.” Lucas aliyawaza hayo kisha akakunja uso wake kwa nguvu. Alikunja pia ngumi yake kwa nguvu akaizungusha kwenye uso na kuing’ata.
Usiku uliendelea kuwa mgumu sana kwa bwana Lucas Manyama. Kwa sasa alikuwa akisubiri kwa hamu kumbwa hiyo kamati ya nidhamau na maadili ya kazini kwao. Maisha yaliendelea huku akimwomba mwenye nyumba amvumilie kwa mwezi huo kwani mambo hayakai sawa kwa upande wake. Mwenye nyumba alimweleza bayana kuwa hatoweza kumvumilia zaidi ya mwezi hivyo kama hawezi kulipa kodi basi atafute kitu kingine cha kufanya. Zilikuwa ni kauli za kuumiza lakini alijikaza kama mwanamume na kuamini hizo ni changamoo za maisha na huwa zinakuja kwa nayakati na kuondoka na pengine kusaulika. Siku zilizidi kuyoyoma na hatimaye siku ya kusikiliza shitaka lake ilifika akaitwa. Alifika na kusikilizwa na inaonekana boss alijipanga sana maana utetezi wake haukufua dafu mbele ya kamati hiyo. Maamuzi yakatoka kuwa ataendelea kusimamishwa kazi mpaka hapo atakapo lipa deni la million 5 ambalo yeye amesababishia kampuni hiyo. Alitamani kutoa ya moyoni mwake kuwa boss alikuwa na uhusiano na mfanyakazi mpya ambaye na yeye alianza kuwa uhusiano naye lakini roho moja ilimwambia inampasa kukaa kimya maana anaweza kuharibu kabisa.
Lucas alijijengea katika maisha kuwa kamwe hasifanye maamuzi akiwa na hasira au akiwa hana mtu wa kumsapoti. Alitamani sana kuelezaa kamati hiyo ya maadili ya mabaya yote ambayo amefanyiwa na boss. Alitamani kuwaambia kuwa mfanyakazi mpya aliyekuja ndio chanzo cha ugomvi. Alitamani kueleza kuwa boss amemwaribia maisha kwa kumchukua boss wake. Hasira zilimpanda sana na bila kutarajia aliamua kuondoka hili hali kikao kilikuwa bado kinaendelea.
“Ndugu zangu kwa sasa nina hasira sana ambazo zimechanganyika na uchungu wa kile ambacho kilikuwa kikitokea.. Nina mengi sana ya kuwaeleza kwa kuwa mmeshindwa kunisikiliza naomba nitawakilisha ushahidi wangu wa picha na vitu vingine kuonesha ni jinsi gani nimeonewa sana na nimedhulumiwa haki zangu za msingi. Nimekuwa nikipitia kwenye kipidi kigumu sana na naamini kama kamati ya ndani ya maadili ikishindwa kunitetea basi nitaenda idara ya kazi” Lucas aliyasema hayo kisha akapiga ngumi kweye meza na kuanza kuondoka zake. Hakika alionesha kufadhaishwa sana na kilichojadiliwa hapo na kumfanya aonekane ana mengi sana moyoni lakini hana imani na sehemu hiyo. Alishindwa kuyawasilisha kwa kukosa imani na kamati ya maadili. Kamati ambayo ilikuwa imetengenezwa na boss kamati ambayo ipo radhi kupindisha ukweli kamati ambayo ipo tayari kwa gharama yoyote kulinda maslai ya kampuni.
Lucas Manyama aliondoka na kurudi nyumbani. Alikuwa ni mtu mwenye hasira sana na alichokifanya ni kununua pombe kali na kunywa. Alikunywa viroba japo huwa hapendi kabisa kunywa. Aliingia ndani na kulala. Alifanikiwa kupata usingizi akalala na alikuja kushtushwa na njaa ambayo ilikuwa ikimkabili. Alijinynyua na kwenda kutafauta kitu cha kula. Alikula na baaada ya hapo alaipata fusa ya kutafakari yote yaliyotokea kwenye kamati ya maadili. Limshukuru Mungu hakuweza kutoa ya moyoni maana anageweza kuchafua hali ya hewa na kufanya hata watu wapigane.Aliwaaambia yaliyojiri na wengi walimshauri kuwa awe mvumilivu kwa kipindi hiki na pia awaambie hiyo kamati yao impe kwa maandishi kila walichokijadili na maamuzi yake ili wasije mgeuka kipindi atakapoeenda idara ya kazi. Alikubali kufuata ushauri huo na akaseam kesho ataenda kazini. Baada ya kuongea na washauri wake kuna namba ngeni iliyokuwa ikimpigia , aliamua kuipokea.
“Helow mpenzi nimekumiss sana na siamini kama kweli umefika Musoma na hujataka kunitafuta.” Lucas alitega sikio kwa umakini sana na kufanikiwa kugundua kuwa alikuwa ni Juliana.
“Samahani sana mwenzio sipo sawa kwa kweli yaani maisha yananichanganya. Sio mimi ni maisha tu ndo yamenifikisha hapa.” Lucas aliongea kwa sauti ya upole.

“Usijali mpenzi najua unaweza kuchanganyikiwa kwa majanga yaliyokukuta mke anauma sana na pengine kuliko kitu kingine chochote. Cha msingi kwa sasa usipende kukaa mwenyewe kuwa na marafiki watakusaidia sana”

“Asante sana Juliana kwa kuendelea kuwa karibu nami.Naamini pia katika ushauri wako, Wewe ni mwanamke mwenye akili ubarikiwe kwa ukarimu na ushauri.

“Mungu yu mwema naomba niwe karibu yako nahitaji kukupa faraja kwa muda wowote. Naamini kuwa naiweza hiyo kazi naomba nikupe faraja kwa kiwango cha kukufanya usahau shida kwa muda.

“Nashukuru sana Juliana kazi hiyo nimeshakupa na endelea kuifanya kwa umakini zaidi.”
Waliongea mengi na Lucas alimwaidi mrembo huyo kuwa wikiendi Mungu ikijalia ataenda tena Mwanza ili waweze kuwa pamoja. Jambo ambalo Lucas hakulijua ni kwamba Juliana alikuwa amepewa kazi hiyo ya kumpa faraja akishirikiana na Julieth kwa shinikizo la mpenzi wake Kimaro. Kulikuwa na ukaribu mkumbwa uliofanywa ili angalau Lucas hasione kuwa dunia ilikuwa imemtenga. Lucas akashindwa kuelewa kwa nini kipindi hicho wanawake walikuwa wakiwa karibu yake sana. Aliona kama ni bahati na anaweza hata kufanya maamuzi magumu ya kuwa na wasichana wengine wengi maradi kupunguza machungu ya kupokonywa mke wake. Pamoja kuwa alikuwa akitaka kufuata taratibu za sheria za kazi bado alikuwa akiamini na akatamani kuivuruga familia ya boss wake. Alianza kuifuatilia familia hiyo kuwa na habari za ukaribu. Kwanza aliambiwa boss huyo alikuwa na mtoto wa kike ambaye alikuwa mkumbwa na alikuwa akisoma chuo kikuu cha Dar es salaam.

ITAENDELEA………………………………….

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni