Alhamisi, 14 Juni 2018

WORLD CUP FIXTURE

For all football ⚽ lovers

*FIFA WORLD CUP 2018(RUSSIA) FIXTURES WITH INDIAN TIMING. There will be 64 matches in TOTAL*

*Group A:-* Russia, Saudi Arabia, Egypt, Uruguay 
*Group B:-* Portugal, Spain, Morocco, Iran 
*Group C:-* France, Australia, Peru, Denmark 
*Group D:-* Argentina, Iceland, Croatia, Nigeria 
*Group E:-* Brazil, Switzerland, Costa Rica, Serbia 
*Group F:-* Germany, Mexico, Sweden, South Korea 
*Group G:-* Belgium, Panama, Tunisia, England 
*Group H:-* Poland, Senegal, Colombia, Japan

*THURSDAY, June 14/6/2018*
1.RUSSIA vs SAUDI ARABIA  (8:30pm)

*FRIDAY, June 15/6/2018*
2.EGYPT vs URUGUAY (5:30pm)
3.Morocco vs Iran (8:30pm)
4.Portugal vs Spain (11:30pm)

*SATURDAY, June 16/6/2018*
5.FRANCE vs AUSTRALIA (3:30pm)
6.ARGENTINA vs ICELAND  (6:30pm)
7.PERU vs DENMARK (9:30pm)
8.CROATIA vs NIGERIA (5:30pm)

*SUNDAY, June 17/6/2018*
9.COSTA RICA vs SERBIA (12:30am)
10.GERMANY vs MEXICO (8:30pm)
11.BRAZIL vs SWITZERLAND (11:30pm)

*MONDAY, June 18/6/2018*
12.SWEDEN vs SOUTH KOREA (5:30pm
13.BELGIUM vs PANAMA 8:30pm
14.TUNISIA vs ENGLAND 11:30pm

*TUESDAY, June 19/6/2018*
15.POLAND vs SENEGAL (5:30pm)
16.COLOMBIA vs JAPAN (8:30pm)
17.RUSSIA vs EGYPT (11:30pm)

*WEDNESDAY, June 20/6/2018*
18.PORTUGAL vs MOROCCO (5:30pm)
19.URUGUAY vs SAUDI ARABIA (8:30pm)
20.IRAN vs SPAIN (11:30pm)

*THURSDAY, June 21/6/2018*
21.FRANCE vs PERU (5:30pm)
22.DENMARK vs AUSTRALIA (4:30pm)
23.ARGENTINA vs CROATIA (11:30pm)

*FRIDAY, June 22/6/2018*
24.BRAZIL vs COSTA RICA (5:30pm)
25.NIGERIA vs ICELAND (8:30pm)
26.SERBIA vs SWITZERLAND (4:30pm)

*SATURDAY, June 23/62018*
27.BELGIUM vs TUNISIA (5:30pm)
28.GERMANY vs SWEDEN (8:30pm)
29.SOUTH KOREA vs MEXICO (11:30pm)

*SUNDAY, June 24/6/2018*
30.ENGLAND vs PANAMA (5:30pm)
31.JAPAN vs SENEGAL (8:30pm)
32.POLAND vs COLOMBIA (11:30pm)

*MONDAY, June 25/6/2017*
33.SAUDI ARABIA vs EGYPT (7:30pm)
34.URUGUAY vs RUSSIA (8:30pm)
35.IRAN vs PORTUGAL (11:30pm)
36.SPAIN vs MOROCCO (10:30pm)

*TUESDAY, June 26/6/2018*
37.AUSTRALIA vs PERU (7:30pm)
38.DENMARK vs FRANCE (7:30pm)
39.NIGERIA vs ARGENTINA (11:30pm)
40.ICELAND vs CROATIA (11:30pm)

*WEDNESDAY, June 27/6/2018*
41.S. KOREA vs GERMANY (7:30pm)
42.MEXICO vs SWEDEN (7:30pm)
43.SERBIA vs BRAZIL (11:30pm)
44.SWITZERLAND vs COSTA RICA (11:30pm)

*THURSDAY, June 28/6/2018*
45.JAPAN vs POLAND (7:30pm)
46.SENEGAL vs COLOMBIA (7:30pm)
47.PANAMA vs TUNISIA (11:30pm)
48.ENGLAND vs BELGIUM (10:30pm)

*LAST -16:-*
*SATURDAY, June 30/6/2018*
49.Group C-1st vs D-2nd (7:30pm)
50.Group A-1st vs B-2nd (11:30pm)

*SUNDAY, July 1/7/2018*
51.Group B-1st vs A-2nd (7:30pm)
52.Group D-1st vs Group C-2nd (11:30pm)

*Monday, July 2/7/2018*
53.Group E-1st vs F-2nd (12:30am)
54.Group G-1st vs Group H-2nd (11:30pm)
55.Group F-1st vs E-2nd (7:30pm)
56.Group H-1st vs G-2nd (11:30pm)

*QUARTER-FINALS:-*
*Friday, July 6/7/2018*
57.Winner 49 vs winner 50 (7:30pm)
58.Winner 53 vs winner 54 (11:30pm)

*SATURDAY, July 7/7/2018*
59.Winner 55 vs winner 56 (11:30pm)
60.Winner 51 vs winner 52 (12:00am)

*SEMI-FINALS:-*
*TUESDAY, July 10/7/2018*
61.Winner 57 vs winner 58 (11:30pm)

*WEDNESDAY, July 11/7/2018*
62.Winner 59 vs winner 60 (11:30pm)

*THIRD-PLACE PLAY-OFF:-*
Saturday, July 14/7/2018
63.Loser 60 vs Loser 62

*FINAL:-*
Sunday, July 15/7/2018
64. Winner 61 vs winner 62 (8:30pm)

MANCHESTER UNITED 2018/2019

MECHI ZA UFUNGUZI ENGLAND

Jumatano, 13 Juni 2018

SOMO LINAENDELEA

DALILI KUU 6 ZINAZOONYESHA MTU AMBAYE ATACHELEWA SANA KUFANIKIWA.

1)Siku zote ana pesa za kununua vocha na kuweka vifurushi,ana pesa za kununua nguo  lakini hana pesa za kununua kitabu kitakachomuongezea maarifa.

2)Siku Zote ana muda wa kuchart watsapp, kuangalia Movie,kusoma magazeti na Kupiga stori za mpira ama za wasanii lakini hana muda wa Kusoma kuhusu taaluma yake ama mambo ya kumpongeza ujuzi.

3)Siku zote akiona waliofanikiwa anawatuhumu aidha wameiba, ni freemason ama wana bahati katika maisha.Huwachukia na hataki kujifunza Kwao.

4)Siku zote hupenda kuhalalisha kufeli kwake kwa kujitetea,kulaumu uchumi,wazazi,serikali au amerogwa.

5)Siku Zote Hujiona anajua Kuliko Mtu Yeyote Yule na hapendi Kujifunza kwa wengine. Huongea sana Kuliko Kusikiliza.

6)Kila anachoingiza anatumia,ukimwambia kusave ama kuwekeza anasema ngoja nipate cha ziada nitaanza kesho.

Je Unayo dalili mojawapo kati ya hizo?

SWALI LA MTOTO

“Baba kwani mtu akifa anaweza kumnunulia mtu zawadi?” Lilikua ni swali kutoka kwa mwanangu wa miaka 5, nilistuka kidogo kwani alikua anazungumzia mambo ya kufa. Ndiyo kwanza tulikua tumetoka kuzunguka Mlimani City kwaajili ya kuwanunulia wanangu watatu zawadi na tulikaa kidogo ili kunywa Juice kabla ya kurejea nyumbani. Nilimuuliza kwanini anasema hivyo lakini hakua tayari kunijibu, aliniambie nimjibu tu na kumuambia “Hapana, mtu akishakufa hawezi kufanya kitu chochote.”
Nilimuona alivyonyong’onyea na kila nilivyojaribu kumchangamsha hakuchangamka tena. Nilirudi nyumbani na kuanza kugombana na mke wangu nikimuambia ni kwanini wanangu wanazungumzia habari za kufa kipindi kile. Alisema hajui chochote lakini nilijua tu ni yeye tu kawajaza ujinga wanangu, nilikasirika sana na kila wakati niliwaambia wanangu wasiwaze chochote kwani Baba yao nipo na siendi popote.
Siku zilienda na sikukuu ilikua inakaribia, wanangu wote walikua na furaha kasoro Anna peke yake, yule ambaye aliniuliza kuhusu kufa, kila wakati nilipojaribu kumpa vizawadi na kumfurahisha alikua akiishia kulia tu. Sikujua anausmbuliwa na nini lakini nilihisi kuna kitu, mpaka wakati mwingine niliogopa na kudhani kua labda kwakua ni mtoto kuna kitu kaoteshwa na maisha yangu yapo hatarini lakini niliziondoa hizo fikra.
Usiku mmoja nikiwa nimetulia chumbani Anna alikuja chumbani, mkononi alikua amebeba begi lake la shule, alikuja na kukaa kitandani, alikua analia, niliacha kusoma Kitabu na kumkumbatia nikimuuliza tatizo ni nini, hakusema chochote zaidi ya kufungua Begi lake. Alitoa fungu la hela elfu mojamoja na miatano tano zilikua nyingi kidogo, bila kuzihesabu zilikua zinafika kama elfu hamsini hivi. Alinikabidhi zile hela, nilimuuliza kazipata wapi na kwanini ananipa ndipo akanijibu.
“Nizakwangu Baba, nimekua nikikusanya Poket Money unayonipa na zawadi ili nikupe ukamnunulie Dada Jane nguo mpya, yeye Baba yake amefariki hawezi kumnunulia zawadi kama unavyotununulia sisi hivyo anakua anavaa nguo mbaya kila sikukuu. Nataka umnunulie ili uwe kama Baba yake, mimi siwezi kumnunulia kwani mimi si mwanaume siwezi kuwa Baba yake, yeye hana Baba”
Nilikuta machoazi yanaanza kunidondoka kama mtoto mdogo. “Nimefanya nini?” Niliwaza. Jane ni mtoto wa kwanza wa mke wangu, alizaa na mwanaume mwingine kabla sijakutana naye na yule mwanaume kumtelekeza hivyo mke wangu alikua anamlea yeye mwenyewe. Ingawa hakumuambia hivyo lakini ni kama kila mtu alijua kuwa Baba yake Jane kafariki ndiyo maana alikua haji kumtembelea.
Baada ya kumuoa nilianza kuishi naye, ingawa mwanzo niliona itakua kawaida na nilikua nikimpenda Jane lakini baada ya mimi kupata watoto wangu niliwapenda zaidi, nilimtenga na kusema kweli sikumchukulia kama mwanangu, sikujua kama wanangu wanajua kwani muda wote nilikua nawapa kila kitu nawanunulia zawadi huku Jane nikimtenga. Mpaka pale Anna aliponipa ile hela ndiyo nilijua kua inawaumiza wanangu namna ninavyomtenga Jane.
Machozi yalinidondoka uchungu nilioupata ulinifanya nijione kama mnyama. “Hivi napata faida gani kumtenga mtoto wa watu asiye na hatia, huyu si Dada wa wanangu? Kwani ni shilingi ngapi kumpenda huyu Binti…” Niliwaza mambo mengi bila majibu, nilikua katika lindi la mawazo mpaka Anna aliponistua “Baba utamnunulia nguo Dada Jane?” Nilimuambia ndiyo na kumuambia abaki na zile pesa nitamnunulia na pesa zangu.
Siku iliyofuata niliwachukua wanangu wote na mke wangu na ilikua ni siku ya kumnunulia mke wangu pamoja na Jane zawadi. Mke wangu alishangaa upendo niliomuonyesha Jane siku ile, Jane mwenyewe lishangaa kwani nilikua mtu mpya sana, alikua na furaha mpaka machozi, kila wakati alikua na wasiwasi, hata kuchagua nguo aligopa aloposikia bei yake, hakujua nini kimetoke lakini nilimuaomba msamaha mke wangu na kumuambia Jane sasa nitakua Baba yake, sasa najiona mtu mwenye furaha zaidi.
%%%MWISHO

KAZI KWENU WABABA WENYE KUWATENGA WATOTO WA KAMBO NA KUWAJARI WAKWENU SIKUKUU HIYO
MUNGU AWAFANYIE WEPESI

mwalimubahati

Jumanne, 12 Juni 2018

UNGEFANYA NINI HAPA?

NAWATAKIA MJADALA MWEMA:
Mkeo Anarudi Nyumbani kavimba vibaya usoni! Unamuuliza anakujibu kuwa kakutana na vibaka wamemvamia na kumpiga, lakini ukimcheki kwa makini unakuta kila kitu chake amerudi nacho na kiko salama. Unaanza kupeleleza, unagundua kapigwa na “Mchepuko” wake. Unaoneshwa mchepuko huo, nawe unakwenda moja kwa moja (straight) kwa huyo jamaa, unapomuuliza anakujibu kama ifuatavyo:
".....Bro mimi yule ni Mpnz wangu wa muda mrefu hata kabla hujamuoa, tuna miaka mingi ni wapnz wa siku nyingi sana. Mimi nakujua wewe kuwa huyo ni mkeo, ulimuoa wakati mimi sina uwezo kifedha, lakini hatukuwahi kugombana, tumeendelea na mapnz Muda mrefu, na hata watoto unaodhani ni wako, Mimi mwenyewe tulipanga majira, sasa yawezekana nami yupo wangu, kwani huwa natoa matumizi ya mtoto mmoja yule Jenerose. So kuwa na amani, nakufahamu vema.
"....Lakini kilichoniuma sana mimi ni kwamba huyu Mwanamke mshnz, nimegundua ananichet mimi, anatembea na njemba fulani, so iliniuma sana, nilitamani sana ufahamu hili, lakini ningeanzaje kukwambia wakati wewe hujui kama mimi mkeo ni mpnz wangu. Mimi sina tatizo na wewe, na hata akiniambia jana mmefanya sijali, lakini kwanini atembee na mwanmum mwingine tofauti na sisi (wewe na mimi). Kwahiyo kweli nimemfumua hayo makonde, tena kajikanda hapa.
"....Amebadilika sana huyu mwanamke, amekuwa na tabia chafu sana siku hizi, haiwezekani nichangie na mwanamme mwingine kwa mtu ninayempenda. Wee mwenyewe hujui tu ninavyoumia………”
Swali
Kama ndo wewe, utafanyaje, utaanza na huyo jamaa au utarudi mdogo mdogo kwa mkeo? Je utamfanya nini Mkeo?

WAMEKUTANA WAKUBWA, WATOTO ENDELEENI KUWASEMA

Jumatatu, 11 Juni 2018

VIJANA SOMA HAPA

INew York iko masaa 3 mbele ya Calfornia...lakini hii haimaanishi Calfornia inaenda taratibu au labda New York iko mbio sana..Zote ziko sawa isipokuwa kila moja ina TIME ZONE yake

Kuna mtu yuko single sasa hivi. Kuna mtu ameolewa na kusubiri miaka 10 kabla ya kupata mtoto..wakati kuna mtu amepata mtoto ndani ya mwaka wa kwanza wa ndoa

Au, kuna mtu amemaliza degree akiwa na miaka 22, lakini akasubiri miaka 5 kabla ya kupata kazi, wakati kuna mwingine amemaliza degree akiwa na miaka 27  na akapata kazi mwaka huo huo

Kuna mtu kawa mkurugenzi akiwa na miaka 25 na kufariki akiwa na umri wa miaka 50 , wakati mwingine amepata ukurugenzi akiwa na miaka 50 na kuishi mpaka miaka 90

Kila mmoja anaishi kulinga na TIME ZONE yake

RAFIKI ZAKO, NDUGU ZAKO AU WADOGO ZAKO WANAWEZA KUONEKANA MBELE YAKO , AU WENGINE NYUMA YAKO
KILA MMOJA HAPA DUNIANI ANATEMBEA/KUISHI KWENYE BARABARA YAKE PEKE YAKE YA MUDA..MUNGU ANA MPANGO TOFAUTI KWA KILA BINADAMU..TOFAUTI NI MUDA TU..
Tazama , Obama anastaafu akiwa na miaka 55, Trump anaanza akiwa na 70.

USIMWONEE WIVU ,WALA KUMLAUMU MTU, KILA MMOJA NA TIMEZONE YAKE

ENDELEA  KUJIAMINI, KILA KITU KITAKUWA SAWA.

HAUJAWAHI WALA HAUJACHELEWA..ISSUE NI TIME ZONE YAKO TU

USIUMIZWE SANA KICHWA KWAMBA ..MBONA MWENZANGU KAJENGA MIMI BADO, ANA GARI MIMI SINA, KAOLEWA MIMI BADO..KAOA MIMI BADO....N.K

CHAPA KAZI KWA BIDII,HUKU UKISUBIRIA MUDA WAKO..MCHE MUNGU UMTEGEMEE...KILA UFANYALO FANYA KWA IMANI.
bahati

Jumapili, 10 Juni 2018

ELIMU

*_ZINGATIA_*

*_MWANAUME USIMWACHIE MKEO HELA CHUMBANI,_*

*_MWACHIE MBELE YA WATOTO  NA UMWAMBIE NA MATUMIZI YAKE, NA WATOTO WASIKIE USIJE KUISHI MAISHA YA UPWEKE UZEENI_*

👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽

*MWANAUME*
Unamwachia mkeo hela ya Chakula Chumbani, Mke Anatoka na Kapu anaenda kununua Chakula, Anapika, Anawaambia watoto, Njooni Wanangu Mle Nimewapikia Chakula Kitamu, Watoto wakishakula Wanasema Asante Mama.

*MWANAUME*
Unamwachia Mkeo hela ya Nguo za Sikukuu Chumbani,
Kesho Yake mkeo Anatoka kwenda Kununua Nguo, Akirudi Anawaambia Wanangu Nimewanunulia Nguo za Sikukuu Njooni Mjipimie, Watoto Wakishajipima, Anawaambia Wanangu  Mmependeza Eeee, Simnaona  Ninavyowapenda
Watoto wanafurahi na Kusema Asante Mama,

*MWANAUME*
Kila Aina ya Pesa ya Matumizi Unamwachia Mkeo Hela Chumbani,

*MWANANUME*
Ukifika muda wa kutoa Ada Unamkabidhi Mkeo Hela Chumbani,
Kesho yake Mkeo Anawaambia Watoto kuwa Anaenda kuwalipia Ada ya Shule, Akirudi Anawaambia Wananhu nimeshawalipia Ada, Na gari za Shule Zitakua Zinawapitia, Nataka Msome Wanangu ili Baadae Mje Mnitunze, Watoto Wanasema Asante Mama.

*KIBAYA ZAIDI*
Ukifika muda wa kutoa  Adhabu, Mkeo  yeye hatoi Adhabu, Anawaambia Watoto, Ngoja Babayenu Arudi, Nawewe Ukirudi Unaelezwa na Mkeo matatizo ya Wanao, Unachukua Bakora Unawaadhibu Watoto, Bila kujua kuwa Unazidi Kujenga Uhusiano M'BAYA na Wanao.

*NGUMU KUMEZA*
Ukifika Uzeeni, Watoto wako Hawana  *KUMBUKUMBU* Yoyote Ya Mema Uliyowafanyia.

*NA*
*UKUMBUKE KUWA-->>*
*MTOTO ANAANZA KULISHWA SUMU YA MANENO KUTOKA KWA MAMAYAKE KUANZIA UMRI WA MIAKA 9 --- 15*

*MWANAUME KUWA MAKINI SANA*

          *_ZINGATIA HAYO KWA MAISHA YA UZEENI_*

source mwalimubahati

Jumamosi, 9 Juni 2018

CHEKA

Wewe na demu wako mnaenda kwa rafik ako wewe..Ambae pia anafuga mbwa, mnapofika mbwa anakubwekea wewe anamuacha demu wako, hapa tumia busara, narudia tena tumia busara.

Wa kunielewa wanielewe.

KOBOKO

#FAHAMU:Huyu ndio nyoka mwenyekasi zaidi na mwenye sumu kali zaidi duniani,Nyoka huyu ujulikana kama KOBOKO au Black Mamba.
hupatikana katika sehemu za Mashariki na Kusini mwa Afrika huishi katika Makazi yoyote ambayo hutoa joto na unyevunyevu.
Nyoka huyu akitaka kufanya shambulio hutanua kinywa chake na shingo yake na hutoa sauti kama ile ya tairi likiwa linatoa upepo.
Black mamba ana aina mbili ya sumu zinazozalishwa katika mwili wake moja ni huitwa (Neuro)  hii huathiri mfumo wa neva na nyingine ni (Cardio-toxin) hii huathiri mfumo wa moyo na sumu hizi zinaweza kuua binadamu chini ya dakika 20.
Pia imethibitika kuwa matone mawili ya sumu yake yanaweza kuua lakini mbali na kiasi kikubwa cha sumu kali sana aliyonayo, Koboko hana ujanja mbele ya Nguchiro,Mbweha, na Nyegere.

Ijumaa, 8 Juni 2018

PUNYETO

.Je hili unalifaham?🤔🤔🤔🤔😳😳😳 soma hapa uelewe zaidi👇👇

JINSI PUNYETO (MASTURBATION) INAVYOATHIRI SUALA LA NGUVU ZA KIUME.

Kama wewe upo kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii utakuwa umeshaona jinsi magroup ya mambo ya picha za uchi na video za ngono yalivyo mengi kuanzia instagram facebook na WhatsApp. Washiriki wengi ni wanaume hasa vijana, na tafiti mbali mbali zinaonyesha kuwa wanaathiriwa sana na picha hizo na kuchochewa kujichua (kupiga punyeto) ili kumaliza hamu zinazoamshwa na hisia kali za ngono baada ya kutazama picha hizo na vidoe hizo.

Wengi wao hawafahamu namna gani suala hilo (masturbation) linavyoweza kuathiri afyaya uzazi hasa nguvu za kiume.

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Of course ipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume. 

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi ya kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafirisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja na  upigaji punyeto kwa  muda  mrefu.

Na leo nataka tuangalie  namna suala la upigaji punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  mfumo wa nguvu za kiume.

SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME IKOJE?

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa suala la nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (spinal  chord)

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huua  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i. Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii. Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana.

Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  mtoto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i. Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii. Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.        Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.       Uume kurudi  ndani
iii.      Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

Ndo unakuja kuoa binti wa watu baada ya muda mfupi tu anashangaa tendo la ndoa huwezi anahisi una michepuko au humpendi tena migogoro inaanza... kumbe kuna jambo lilishaharibika na hukuwahi kujua nini ufanye ili kurejesha hali imara na murua.

MSAADA WA UHAKIKA UPO.

Hata hivyo inawezekana kabisa kuondoa ATHARI hizo zinazosababishwa na kujichua kwa muda mrefu. Ingawaje ni lazima kuongea na mhusika na kujua amefanya hivyo kwa muda gani na mara ngapi kwa wiki nk kwa miaka mingapi, na kufahamu mazingira aliyopo na mambo yaliyofanya akaanza kujichua. Yoye haya tunasema ni case to case basis. Ila kuna njia za kukusaidia kurejesha nguvu zako za kiume na kuimarisha tena misuli ya uume na kuufanya usiwe unarudi ndani kama wa mtoto pamoja na kukusaidia kabisa kuacha kujichua.

Kama unataka kujifunza zaidi na kusaidiwa kuondokana na athari hizo karibu tuzungumze

Alhamisi, 7 Juni 2018

*HIZI NDIZO SABABU ZINAZOSABABISHA ULIPIE UMEME KWA GHARAMA KUBWA*.

*HIZI NDIZO SABABU ZINAZOSABABISHA ULIPIE UMEME KWA GHARAMA KUBWA*.

Unaweza kushangaa kuona *wengine wakinunua Umeme wa 9,150 Wanapata Unit 75 wewe ukinunua Umeme wa 10,000 unapata Unit 28.1*

Iko hivi, Watumiaji wadogo wa Umeme ambao kwa mwezi *Matumizi yao hayazidi Unit 75 Wapo Tarrif D1(4)* Na wanauziwa Unit moja kwa Sh.122,

Wakati watumiaji walio wengi wako Tarrif T1 hawa Unit moja wanauziwa Sh.kati ya sh.356.45 tu.

*Maana yake mtumiaji aliyeko Tarrif D1(4) Ananunua Unit 41 Kwa sh 5,000*
*Wakati walioko Tarrif T1 Wananunua Unit 14 kwa sh.5000*

NAWEZAJE KUWA MIONGONI MWA WATUMIAJI WADOGO WA UMEME YAANI (TARIFF D1)?

Kama ni nyumba ya kupanga na mko wengi ni ngumu kidogo. Kwanza unatakiwa Kupunguza Matumizi Ya Umeme Yasiyo ya Lazima
Pili nunua Vifaa vyenye Wats ndogo vitu kama taa, Tv, Friji, Pasi n.k

Tuchukulie mfano wa Taa zenye Wats 40 nje zikiwa nne na za Wats 18 kwa ndani zikawa Taa 8 nyumba yako nzima itakua na jumla ya Taa 12 Ambazo zitakua na Jumla ya Wats 304
Lakini ukinunua Taa zenye Wats ndogo *(*Energy Saver*) Japo bei yake iko juu kidogo ukilinganisha na Taa zenye Watts kubwa. Kwa mfano huu huu ukanunua Taa zenye Watts 5 kila moja za nje Nne na taa 8 za ndani zenye Wats 3 kila moja
Jumla ya taa 12 zitakua na Jumla ya Wats 44 tu.

Maana yake utakuwa umepunguza jumla ya Wats 250 upande wa Taa tu lakini idadi ya Taa imeendelea kuwa ni ile ile. Mtu mwenye taa moja ya Wats 40 akiwasha nawew ukawa taa zote 12 Matumizi yenu yatakua hayana tofauti kubwa
Mwisho kabisa, *matumizi yako ya Umeme yakiwa chini ya Unit 75 kwa miezi mitatu mpaka Sita Mfululizo*  unatakiwa kwenda TANESCO  Ofisi uliyo Karibu nayo kuomba kubadilishiwa Kutoka Tarrif 1 kwenda Tarrif 4.

*NB*: Hata baada ya kurudishwa Tarrif 4, Siku ukitumia zaidi ya Unit 75 kwa mwezi utarudishwa Tariff 1. Baadhi wanapopata fedha nyingi na hawana uhakika wa kuzipata tena kwa kipindi kirefu, huamua kununua umeme mwingi ili asihangaike kwa muda mrefu. Hilo ni kosa na mara Tanesco wanapoona "manunuzi"  yako ya Umeme ni makubwa wanakuhamishia kwenye Tariff kubwa bila kukupa taarifa. Hivyo, usifanye matumizi holela. ELIMU HII NI KWA HISANI YA SINGIDA REGIONAL CONSUMERS COMMITTEE (Singida RCC) - Kamati ya Watumiaji huduma za Nishati na Maji mkoa wa Singida.

Jumatano, 6 Juni 2018

UJUMBE MZURI

Inaumiza na kufunza.
Nmekopy kwenye group moja la WhatsApp
“Baba Karanga za Diamond! Baba nataka Karanga za Diamond!” Huu ni ule wakati ambao unasimama kwenye foleni na unatamani hata kuwasha gari na kusukuma magari yaliyo mbele yako. Ilikua ni jioni nimetoka kuwachukua wanangu shule na mtoto wangu mdogo wa mwisho alianza kupika kelele za kutaka karanga. Pembeni yangu kulikua na kijana, au niseme mtoto kashikilia Karanga za Diamond kazizungusha shingoni anauza.
Alikua akipita kila gari kuuza, kwa kawaida sipendi kushusha vioo kwenye gari lakini kutokana na kelele nilijua na ile foleni angeanza kulia, nilimdekeza sana hivyo sikutaka alie kwa kitu cha Shilingi elfu moja. Nilishusha Kioo cha gari na kumuita yule kijana. “Karanga bei gani?” Nilimuuliza, “Moja mia tatu, tatu buku, aliongea huku akinionyeshe kama anataka nikate. “Naomba za elfu tatu.” Niliongea huku nikimkabidhi noti ya Shilingi elfu kumi.
“Shikamoo Baba Mdogo…” Ilikua ni salamu yake wakati anaipokea ile pesa, nilistuka kidogo na kunyanyua uso wangu kumuangalia. Sikua namfahamu hivyo nilidhani ni salamu tu za vijana kwakua nilinunua Karanga nyingi. “Umenisahau? Mimi Peter, Peter Jackson…” Sasa aliongea akionyesha kuwa ananifahamu kabisa, alitaja jina la Marehemu Kaka yangu. nilijikuta nakodoa macho kumuangalia vizuri.
Nilistuka kwani mbele yangu ni kama alikua amesimama Jackson, sura yake kipindi tunaenda kuteka maji kule Kijijini Iringa ilinijia. Hapo ndipo nilikumbuka, yule alikua ni mtoto wa Marahemu Kaka yangu, ndiyo najua mnashangaa, mimi niko kwenye Gari nauziwa Karanga na mtoto wa Marehemu Kaka yangu, mnadhani labda ni Kaka wa jirani. Hapana, ni Kaka yangu, tena si tumbo moja tu, hapana yeye ndiyo aliniachia ziwa.
Najua mnashangaa mnajiuliza labda alitutenga tangu zamani. Hapana yeye ndiyo alinisomesha mpaka kumaliza chuo kikuu. Wakati huo yeye akifanya kazi nzuri tu kama Mkatoika kampuni moja, baada ya kuishi maisha ya shida kipindi cha utotoni na yeye kusoma kwa bidii na kufanikiwa kutoka kimaisha hakutusahau ndugu zake. Mpaka anafariki miaka mitatu iliyopita alihakikisha kuwa wote tunasoma na sikusoma tu bali alitutaftia kazi nzuri.
“Wewe unafanya nini huko Barabarani wewe si ulikua shule?” Niliuliza kwa aibu, nilitaka kumfokea lakini nilikumbuka tangu mazishi ya Kaka yangu na kugaiwa kwa mirathi sikugeuka nyuma. Sio mimi tu hata ndugu zangu wengine, kila mmoja alikua na familia yake hivyo kila mtu alikua bize na maisha yake. Baada ya wazazi wetu wote kufariki Kaka yetu yule ndiyo alikua akituunganisha hivyo yeye alipotangulia kila mmoja lishika hamsini zake.
“Niliacha Baba, sasa hivi niko nafanya biashara…” Aliongea kwa uchangamfu kabisa. Nakumbuka wakati Baba yake akifariki alikua akisoma kidato cha kwanza Nairobi na moja ya sehemu za Mirathi ilikua ni kwaajili ya kutunza watoto ikiwa ni pamoja na kuwasomesha. “Nishikie nikuombee chenji hapo kwa menzangu…” Aliongea huku akimuita kijana mwingine aliyekua pembeni yake na kumuomba chenji, mimi bado nilikua nimeduwaa.
Bado nilikua nawaza ni nini kilikua kimetokea mimi niko kwenye gari nina maisha mazuri wakati mtoto wa Kaka yangu anauza karanga, mchafu mchafu kachakaa na anaonekana kuchoka. Lakini hakua na makuu, wala hakutaka kuniomba chochote, alinipa chenchi yangu. “Msalimie Mama mdogo Baba, sisi ni wazima… Mama anakusalimia…”
Aliongea na kuondoka, huwezi amini nilimuangalia mpaka anapotelea bila kuweza kunyanyua mdomo kumuita. Machozi yalikua yananitoka bila kujua. “Nimefanya nini?” Nilijiuliza bila majibu. Nilikuja kustuliwa na honi za magari mengine wakiniambia kuwa niondoke kwani nawachelewesha. “Baba unaumwa? Mbona unalia?” Mwanangu mkubwa aliniuliza lakini sikua na jibu.
Nilifika nyumbani na kumuuliza mke wangu kama anawasiliana na mke mwenzake, mke wa marehemu kaka yangu. Hakua akiwasiliana naye, alikua hata hajui anaishi wapi? Nilishindwa kukaa ndani, niliamua kwenda kumtafuta, nilifika kwenye nyumba yao, kufika ndipo nilikumbuka kuwa ile nyumba ilikua ni ya shirika ambayo Kaka yangu alipewa hivyo baada ya kufariki waliondolewa na alikua anaishi mtu mwingine.
Nikakumbuka kuna sehemu Kaka alikua anajenga, nilienda nyumba ilikua haijakamilika, alikua anajenga nyumba kubwa ya ghorofa. Nilifika na kukutana na watoto wengine wa Kaka, walikua wakicheza nnje ya lile ghorofa kubwa ambalo lilikua kama Gofu. Wao walikua wadogo hata hawakunitambua, lakini mimi niliwakumbuka. Walinisalimia niliwaulizia Mama yao wakaniambia ametoka, sikua na haraka nilitaka kumsubiri kwani hata hakua na namba za simu.
Nilikaa pale mpaka kwenye saa moja hivi za usiku. Peter ndiyo alikuja na kuniona, alishangaa kuniona pale na kunisalimia, alinikaribisha ndani. Alionekana kuchoka sana lakini alijitahidi kutabasamu, alishakua kijana anaelewa. Nilimuulizia alipo Mama yake na kama atachelewa. “Nyie si mngempeleka kumuona Mama! Mnamchelewesha Baba mdogo au hamjui ana kazi zake huko za kufanya!” Aliwafokea kidogo, nilimuambia haina shida ndipo akaniambia alipo Mama yake.
Hakukua mbali sana, tuliingia kwenye Gari na kuanza safari, ndani alinichangamkia, aliniulizia kuhusu wanangu, kuhusu Shangazi zake, kuhusu Baba zake wadogo wengine na watu wengi wa familia. Alikua akimjua kila mtu lakini kwa bahati mbaya sisi ni kama tulikua tumewasahau. Mimi na ndugu zangu tulikua tukikutana mara kwa mara lakini hata mara moja tulikua hatujawahi kuwazungumzia lakini yeye ambaye hata alikua hatujui vizuri anaulizia tunaendeleaje.
Nilifika alipokua shemeji yangu, nilimuona kakaa Barabarani, karai la ndizi na kibatari kiko mbele yake. “Mama kuna mgeni wako…” Alimuita Mama yake ambaye alishtuka kuniona. Nilimuona yule shemeji yetu ambaye alikua anatupikia mara kwa mara tukienda kumsalimia. Aalikua kachoka, kakonda imebaki sura tu, alijitahidi kutasabasamu, alichangamka, alijitahidi kuonyesha kama hana shida yoyote lakini shida zilijionyesha.
Tulisalimiana, aliona aibu hata kunishika mkono akihisi atanichafua. Nilimuomba turudi nyumbani naye hakubisha, nilifika mpaka kwake ndipo nikagundua kuwa walikua wakiishi katika gofu, hata milango lilikua halina zaidi ya shuka lililotundikwa kama mlango. Kweli niliumia, aliniletea kiti nikakaa, kila nikifumbua macho nilimuona Marehemu Kaka yangu kasimama ananisuta.
Nilihisi kama ananiambia “Kweli nyie ndiyo wa kuwafanyia hivi wanangu, nyie niliowaamini nikawasomesha! Hivi kweli mke wangu ambaye nilimkataza kufanya kazi awe Mama wa nyumbani nyie nikawatafutia kazi ndiyo analea wanangu nyie na kazi nzuri hata kuwasomesha hamuwezi?” Nilishindwa kuvumilia nilimuuliza shemeji yangu nini kimetokea akaniambia, maisha.
Baada ya kupata mirathi alitegemea kuendelea kuwasomesha watoto, alitumia tumia akijua ni pesa nyingi lakini matumizi yalikua makubwa, anashtuka zishakatika nusu hapo ndipo akaamua afungue biashara, kwakua hakua na uzoefu alitapeliwa mara mbili na kupoteza kila kitu. Nilisikitika na kumuambia kwanini hakuja kuomba msaada alinikumbusha alishanipigia simu mara ziadi ya kumi zote namuambia nitamtafuta nitamtafuta.
Nilikumbuka mara ya mwisho alikuja ofisini kuniambia kuhusu ada ya watoto nikampa elfu kumi. Sikua na chakuongea zaidi nilijua sisi ndiyo tumemuangusha, Kaka yangu hakumuandaa kubeba majukumu kama yale. Alimfanya Mama wa nyumbani, alimkataza hata kutoka ndani, kila kitu alikua ananunuliwa, Kaka alikua na wivu na mara nyingi akitoka alikua anapigwa na kweli tulikua tunamuona Kaka yuko sawa na shemeji anakosea.
Hata katika mali hakua akimshirikisha zaidi ya sisi ndugu zake, hata ndugu wa shemeji alikua hawasaidii na kila mara alisema hana pesa. Niliona aibu kuendelea kuuliza, nilimuambia anyanyuke tunaondoka pale na kuanzia siku ile nitamsaidia kulea familia kwani ni jukumu letu wale ni wenetu. Sikutaka waendelee kulala pale niliwachukua na kuondoka nao. Sasa hivi watoto wamerudi shule na shemeji nimemfungulia biashara.
Nyumba nimepata watu wa kuimalizia wanataka kufungua ofisi hivyo naamini mpaka mwezi wa nane mwaka huu wataanza kuchukua kodi kidogo kidogo. Nimeandika kisa changu ili kumuomba msamaha Kaka yangu kwa kushindwa kulea familia yake na kuwaambia wanaume wenzangu kuwa hata kama una mali kiasi gani hakikisha unamuandaa mkeo kuhudumia wanao kwani ndugu wana familia zao na ukiondoka watakusahau, nawaambia kwasababu sisi tulisahau pamoja na kusaidiwa sana.
Najua watu wengi hatuwazi kuhusu kifo lakini kipo. Je, mwanaume umemuandaa mke wako kubeba majukumu ya kuhudumia wanao au unategemea ndugu na wewe mwanamke Je, umejiandaa kubeba majukumu au unasubiri yakufike kwanza

TAHADHARI

TAHADHALI TOKA UMOJA WA MATAIFA "Imetafsiriwa"

Biashara ya viungo vya binadamu imeshamiri au inaongezeka sana Mashariki ya kati.

Viungo kama: Figo inauzwa takribani dola $262,000; sawa na shilingi milioni 940 za kitanzania.
Moyo unauzwa dola za Kimarekani $ 119,000; sawa na shilingi za Kitanzania milioni 430. Na Ini linauzwa dola za Kimarekani dola $157,000; sawa na Shilingi za Kitanzania shilingi milioni 562.

Kwa hiyo basi, muwe makini na makampuni au mawakala wanaojifanya, kuwatafutia kazi nje ya nchi au nafasi ya masomo(scholarship) ambapo mwisho wa siku, ukifika huko nje, unauawa, kisha kutolewa viungo vyako muhimu  ambavyo vimetajwa hapo juu na kuuzwa.

Hivyo basi, ni vizuri watoto wetu na wajukuu zetu wajulishwe hali hii, ili  wasiangamie kwa tamaa ya kutaka kupata kazi nje ya Nchi.

Tuma ujumbe huu, ili kuweka wazi uovu huu ambao shetani kwa kushirikiana na mawakala wake wanafanya ili kuangamiza maisha ya watu.

Ili kuokoa maisha ya watu(wahanga) tuma  kwa mwingine pia ujumbe huu. Ubarikiwe!!

UGONJWA WA Alzheimer

*KWA VIJANA WA ZAMANI*

Baada ya kufikisha umri wa miaka 50, mtu anaweza kupata aina nyingi za magonjwa. Lakini ugonjwa mmoja ambao nina na wasiwasi nao zaidi ni _Alzheimer's_. Sio tu kuwa sitaweza kujihudumia, lakini unaweza kusababisha usumbufu mwingi kwa wanafamilia.

Siku moja, mwanangu alirudi nyumbani akaniambia kuwa daktari rafiki alikuwa amemfundisha zoezi linaloutumia ulimi. Zoezi la ulimi linafaa sana katika kupunguza na kutokewa na _Alzheimer’s_ na pia hufaa kupunguza / kuboresha yafuatayo:
1. Uzito wa mwili
2. Shinikizo la damu
3. Kuganda kwa Damu katika Ubongo
4. Pumu
5. Kutoona mbali
6. Sikio linalovuma
7. Maambukizi ya Koo
8. Maambukizi ya bega / shingo
9. Kutopata usingizi

Hatua husika ni rahisi sana na nyepesi kujifunza. Kila asubuhi, unapoosha uso wako, mbele ya kioo, fanya zoezi kama ilivyoelezwa hapo chini:

*Utoe ulimi wako na kunyoosha - upeleke kulia kisha kushoto mara 10*

Tangu nilipoanza kuufanyia mazoezi ulimi wangu kila siku, kulikuwa na uboreshaji katika kumbukumbu yangu ya Ubongo.

Akili yangu ilitulia na safi na pia kulikuwa na maboresho mengine.
1. Kuona mbali kuliimarika
2. Kupotea kizunguzungu
3. Kuboreka afya
4. Usagaji bora wa chakula
5. Kupungua mafua ya mara kwa mara
Nina nguvu na najihisi mwepesi zaidi.

Zoezi la ulimi husaidia kudhibiti na kuuzuia ugonjwa wa _Alzheimer's_. Utafiti wa kiganga umegundua kuwa ulimi una uhusiano na ubongo MKUBWA. Wakati mwili wetu unapozeeka na kuwa dhaifu, dalili ya kwanza kuonekana ni kwamba ulimi wetu unakuwa mgumu na mara nyingi unatamani kujitafuna wenyewe.
Kuuzoeza ulimi wako mara kwa mara kutausaidia ubongo, kutasaidia kupunguza fikra zetu kushuka na hivyo kuwa na mwili wenye afya.

_*"Madaktari wanahimiza kila mtu akipokea ujumbe huu aupeleke kwa watu wengine kumi, na kwa hakika angalau maisha ya mtu mmoja yataokolewa ...”*_

WADADA, MABINTI NA MAMA WA MAREHEMU

ANGALIZO KWA MABINTI, USIPUUZE..!!

Mimi sikukatazi kutumia mwili wako kama kitega uchumi.

Sikukatazi kulala na wanaume kwaajili ya pesa,mavazi,vipodoxi na hata magari

Lala na kila mwanaume unayemwona mbele yako.

Endelea tu  kubadili wanaume kama hereni leo unavaa nyekundu kesho pinki.

Endelea kuweka rekodi ya kulala kwenye mahotel mengi na wanaume tofauti tofauti.....Aqwiline hotel, sheraton hotel n.k

Endelea kuwapanga tu mpaka idadi ya wanaume uliolala nao iwe kubwa kuliko hata umri wako mfano una miaka 25 na umeshalala na wanaume 30 tofauti tofauti.
.
.
Endelea tu kuwa mama huruma mtaani na kuwachuna wanaume kwasababu tu unataka kwenda na wakati:
Unataka kutumia simu ya kisasa:
Unataka kuseti nywele za bei kubwa.
Unataka kuvaa nguo za bei ghali, na Kutembelea magari.
we wachune tu.

Na zile kauri zako za dharau pia usiziache "Its
none of ur business"
Ni kweli hainihusu na wala sina mpango na hayo unayofanya.
.
.
Ila utakapoanza kuona inanihusu ni pale utakapoanza kufungua mdomo wako na kusema unatamani mwanaume wa kukuoao akupende hivo hivo ulivyo
Hususani pale utakapokuwa umri wako umeenda na umeshapoteza kila kitu hujabakiwa na chochote cha kusema utaringia

Hapa ndo utaanza kutamani mwanaume yeyote akutongoze uende ukakatalie geto ili tu upate kuolewa.

Pamoja na yote kuolewa ndo utaolewa ila Mungu lazima atakupa mwanaume wa kuendana na ww mwanaume ambaye nae atakuwa alishafanya matukio ya ajabu na yasiyo simulika siku zake za nyuma
Na huyo ndo atakuwa mume wako.
.
.
Baada ya miaka miwili tu ya ndoa yako utakuwa unaanza sasa kujipashapasha kwa kwenda makanisani maana yawezekana ulishapoteza kizazi chako katika harakati za kutoa mimba mfululizo ili tu kuendelea kuufaidi ujana.

Wakati huu ndo utakapoanza kuwatafuta wachungaji na kuhamahama makanisa leo kwa mchungaji huyu kesho kwa yule mara leo kanisa hili kesho lile
Lengo tu kuutafuta muujiza uweze kupata mtoto.
Unasahau kuwa ulishatoa mimba nyingi na ulishatupa watoto kibao.

Utalia sana na kutamani nikuonee huruma
Lakini mm nasema kama ni kulia we lia tu hata machozi ya damu.

Mm ninaowaonea huruma na kuwasikitikia ni wale ambao hawajapata watoto kwa mpango wa mungu na sio wanaojitakia kama ww Ebooo

Nategemea hapa wakunichukia watakuwepo maana ukweli unauma.

Nimeeleweka?

Jumanne, 5 Juni 2018

SOMO LINAENDELEA HAPA

Mwanamke kutwa unalalamika wanaume waongo kwenye mapenzi wakikutumia tu wanasepa, huna hata akili ya kufikilia kwann kwako wagonge wasepe hawaingii ndani? Na daily unahudhuria harusi za wasichana wenzio wakiolewa?  Au wao wanaolewa namajini eti? 😂😂😂 hii dhana kujiona watoto wa mjini, wanawake wa kisasa sijui, basi ndo mnakuwa kama makuku ya kisasa kweli hamfai kwa kufugwa shida tupu!! Maana makuku ya kisasa ukitaka kuyafuga basi ujipange kweli kweli kuanzia mtaji wa kipesa hadi muda wa kuyahudumia!! Ndo nyie sasa, yaani kiukweli wanawake wa sikuhizi hata radha mmeisha kabisa 😂 We unataka mwanaume akuoe wakati hujawahi kujiongeza hata kusema umfulie, kazi kumsifia kapendeza hujui hata anafuliwa na nani?  Hujawahi hata kumpikia kazi kumsifia ananenepa hujui hata anakula wapi, halafu unataka ndoa?   kila siku ukienda gheto kwake we kazi kuulizia series za kikorea kama kaleta mpya, huulizi hata Leo unanunua mboga gani nije kukupikia, mwanamke mzima bila haya unaenda kwa bwana wako unafika unalia njaa halafu unamuagiza kabisa akakununulie chips kuku! Halafu unataka atoe posa kwenu??  Kazi mnayoijua ni kuomba omba hela tu utazani watoza ushuru wa manispaa? Mkifulia Ndo mnajifanya kusema "Bby nimekumiss nataka nije leo" pumbavu kumbe pesa Ndo inayokupeleka, mkishafumuliwa fasta mnaomba nauli na hela ya kula hata kukumbuka kutoa shuka utandike nyingine huna mda huo, tunawajua Sana ila tunawatazama tu mnajiona wajaanja kumbe mnajishusha wenyewe,  haya mambo mnayaona ya kipuuzi lakini ndo uchawi kwa mwanaume ajue thamani yako, asifikirie kukupoteza hata siku moja, sasa nyie endeleeni tu kufuata hela, mnaenda kwa wanaume mmejikoki sadolin za rangi mdomoni, machoni mpaka mtu anashindwa kukukiss! Umefuga makucha utazani visu vya kukeketea?? 😀😀 sijui hata mnasafishaje maumbile yenu, unakuta unang'aa usoni utazani duka la wahindi lakini ndani unatoa uvundo 😂😂😂 aisee mtalalamika Sana nawaambia, wanaume Ndo sisi mnaotuletea nyodo Ndo tunapaswa kuwaoa, tutawanyoosha mpaka mjute kuzaliwa! Pendeni hela tuwazeeshe!! NIMEITOA MAHALI HII NIKAONA TUIONE WOTE

Jumapili, 3 Juni 2018

MTOTO AMEOKOTWA ANAITWA MAGRETH ANASEMA KWAO TABATA.KAMA KUNA ANAEMFAHAMU AU WAZAZI WAKE WAPIGE SIMÙ NO 0784226375,0718642322 NAOMBA TUSAIDIANE KUTUMA KWENYE MAGROUP MENGINE WAPENDWA.

mbwa gani ni tofauti na wengine?

UJUMBE KUTOKA CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA MAFUNZO YA HOSPITALI CHA LAGOS (LUTH)


Tafadhali mjulishe mkeo kuhusiana na hili, , Hii ni tahdhari muhimu kutoka wataalamu wa afya [ LUTH ]  kwa  wanawake  wote  wawe  watoto  wachanga,  wasichana,  mabinti,  wanawake, akina mama; saratani ya kizazi imeenea tafadhali epuka kuosha sehemu zako za siri kwa kutumia sabuni, osha kwa kutumia maji tu, kuna kemikali mbali mbali kwenye sabuni ambazo kiujumla wake ni hatari sana naupo uwezekano zinasababisha saratani ya kizazi, kesi za saratani ya kizazi zimatapakaa katika hospitali nyingi kubwa kwa hiyo tahadhari na ujumbe huu muhimu.
Kama unawaonea huruma wafikishie ujumbe huu ambao pia ni muhimu kwako.
⭕  Wasichana 56 wamefariki kwa kutumia (Pedi) Whisper, Stayfree nk.

⭕ Usitumie pedi moja kwa kutwa nzima kwa sababu kemikali zilizotumika (kuitengenezea) inabadilisha maji maji na kuwa rojo rojo ambayo inasababisha saratani katika kibofu cha mkojo na kwenye fuko la uzazi. Kwa hiyo tafadhali jaribu kutumia pedi zilizotengenezwa kwa kutumia pamba, au kam unatumia aina nyengine ya pedi tafadhali angalau badilisha kila baada ya masaa matano kwa siku. Unapopitiliza muda damu (iliyopo kwenye pedi) hugeuka rangi na kuwa ya kijani na kuotesha ukungu (fungus) unaoingia ndani ya fuko la uzazi na kwenye mwili.

⭕ Tafadhali usione aibu kuusambaza ujumbe huu kwa wasichana na hata kwa wavulana watakao usambaza pia kwa marafiki zao na wake zao wanaowajali.

⭕ DHAMIRIA

Kutokomeza saratani ya matiti "Breast Cancer".

🔺 Mtunze mtoto wako (Kumuweka nadhifu).

🔺Fua sidiria yako kila siku.

🔺Epuka kuvaa sidiria nyeusi wakati wa kiangazi (Summer).

🔺Usivae sidiria wakati wa kulala.

🔺Usivae sidiria zenye chuma kwa muda mrefu.

🔺Unapokuwa juani ziba kifua chako chote kwa mtandio au kitambaa (Scarf).

🔺Tumia deodorant na usitumie Anti Perspirant.

Kwa faida yako. "Deodorant ni manukato yanayotumika kupaka chini ya kwapa kwa kuleta harufu nzuri na wakati huo huo sehemu ile ya mwili iliyopaka deodorant mwili kufanya kazi kama kawaida kwa kuruhusu vipenyo kupitisha jasho. Wakati Anti Perspirant huwa haifanyi hivyo, kazi yake ni kuzui jasho lisitoke na kuifanya sehemu hiyo ya mwili kuwa kavu jambo ambalo ni hatari kiafya na linaweza kusababisha saratani".

🔺Ujumbe huu umetolewa na Hospitali ya Saratani ya Tata " Tata Cancer Hospitali" ipo India.

⭕ Ufikishe ujumbe huu kwa wanawake wote unaowajali bila kusita.

⭕ Kupeana mwamko ni muhimu.

⭕ Nakujali.

⭕ Tafdhali usisite kuwajulisha wanawake wengine na usambaze ujumbe huu kwa kila mwanamke aliemo kwenye orodha yako.

⭕ Nitaanza na wewe.

❣ ❣ ❣ Tuma ujumbe huu angalau kwa group japo moja. By DOCTAR mwaka

Jumamosi, 2 Juni 2018

ACHA  NIKUAMBIE KITU!!

*Ukimhukumu samaki kwa kushindwa kupanda mti utakua umekosea, wewe mtupie kwenye maji uone atakavyo kata mawimbi. Kuna mahali ukiwekwa utafanya vitu vya ajabu mpaka Dunia itashangaa.*

*Usimpotezee mtu anayejitahidi kukujali. Siku akiondoka ndio utagundua ulikua bize unaokota mawe badala ya dhahabu.*

*Kwa nini unahangaika na kuumia unaposemwa vibaya na watu wasio kufahamu kiundani? Inamaana hujui kuwa mbwa hum'bwekea mtu asiyemfahamu.*

*Unapopaka make-up ili upendeze, jitahidi pia kuupendezesha moyo wako kwa kufanya matendo mema maana haina maana kupendeza usoni wakati moyoni ni pachafu.*

*Usikimbilie kuolewa au kuoa mtu tajiri, olewa au oa mtu mwema maana hakuna tajiri atakayeweza kuununua moyo mwema na moyo mwema ni chanzo cha amani na amani ikiwepo ndo kufurahia maisha sasa.*

*Hii na wewe chukua na weka akilini kabisa, ukitaka kupunguza matatizo katika maisha yako jitahidi uwe unafuata utaratibu.*

*Nakwambia ukweli na wewe ndio unamjua, watsap anauwezo wa kuku-block, instagram anauwezo wa kuku-block na facebook anaweza kuku-block lakini kamwe hawezi kuzi-block baraka zako kutoka kwa Mungu zitokako katika Mbingu yake tukufu.*

*Hivi unawezaje kuuza ng'ombe wako eti tu kwa vile umepata oda ya ngozi. Ukiona mtu anachezea utu wako kaa nae mbali maana watu wengine ni kweli kama mkaa, asipokuunguza basi atakuchafua.*

*Hivi, ulishawahi kuona mti uko bize unasumbuka na majani yaliyoanguka? Mti hua bize kutengeneza majani mapya, nawewe kuwa bize kutengeneza na kukaribisha vitu vipya na sio vilivyopita.*

*Swali lenye majibu ya maisha yako yote, Je hicho unachokifanya ndicho Mungu alichokuleta Duniani ukifanye? Kama jibu lako ni hapana, basi unahaki kuendelea ku-struggle bila faida (Sorry, ukweli unauma)*

*Bonus*

*Ukiona moyo wako unagoma katika jambo flani, acha, Mungu anakuepusha na balaa  maana moyo una macho ya kuona mpaka mwisho sema hua tunapuuzia tu.....*

*Learn about yourself better

Ijumaa, 1 Juni 2018

MAKOSA KATIKA MALEZI

Makosa 12 yafanywayo ktk malezi ya watoto ktk enzi tuliyonayo:    

1. Kutokuwa na ratiba maalum ya kula na kulala watoto.  Itatusaidia kujua tabia zao kwa kiasi fulani                   
2. Kutokupenda kuwatumikisha watoto hata kwa kazi ndogo ndogo wanazoziweza kama kufyeka majani majumbani mwetu.  

3. Kuwachia huru kutazama vyombo hatari vya mawasiliano kama simu na video bila usimamizi wa mzazi.                      

4. Kutofuatilia watoto mienendo yao ktk matembezi na maongezi na marafiki zao.           

5. Kutokupenda kula pamoja  wazazi na watoto. Wakiume kula na baba na wakike kula na mama. Mara nyingi baba huzungumza na watoto kwa muda mrefu baada ya kula.                       

6. Kutokuwa na tabia ya kufanya vikao vya kifamilia . Tuko mbele ktk kuandaa vikao vya kisiasi au kijamii kuliko vya ndani mwetu.         

7. Kutokuwazoesha watoto kushiriki shughuli impatishayo mzazi kipato. Mfano kama unauza dagaa kwanini mwanao asianue dagaa mbugani.                 

8. Wazazi kutokuwa pamoja watoto ktk  matembezi yao ya kawaida.             

9. Mzazi wa kike kumpinga au kutetea mtoto mbele ya mtoto pindi mzazi wa kiume anapomuonya/kumfokea mtoto ktk kumfundisha adabu.                    

10. Mzazi kutii masharti/matakwa ya mtoto kila anapotakiwa mtoto kufanya jambo.
                    
11. Mzazi kumwachia majukumu ya malezi wasaidizi wa nyumbani na wao kubaki na jukumu la kuwanunuĺia mahitaji yao tu yaani msaidizi ajenge akili ya mtoto mzazi ajenge mwilï. 

12. Wazazi kutoyapa umuhimu masomo ya dini kwa watoto.