Jumapili, 29 Desemba 2019

MFAHAMU MWANAUME SHUJAA WA SINGIDA ALIYETUMIA MVUA KUPAMBANA NA WAJERUMANI

MFAHAMU  MWANAUME SHUJAA WA SINGIDA ALIYETUMIA MVUA KUPAMBANA NA WAJERUMANI

-Ni KITENTEMI wa Isanzu- Mkalama
-Aliweza kutengeneza mvua wakati wowote  na kuituma kwa Maadui zake wajerumani na kuielekeza anavyotaka .

KITENTEMI mwanaume shujaa wa Singida aliyepambana vita kali na wajerumani walipojaribu kukanyaga ardhi ya Mkalama ambapo mtaalumu huyu wa Mvua aliamrisha mvua kunyesha na kuilekeza kwa majeshi ya wajerumani huku wapiganaji wake wakishambulia kwa mikuki na mishale ya uchungu, Ilikuwa ni vita ngumu iliyowashangaza wajerumani na kuita Miujiza ya kiafrika .

Mnamo mwaka 1901 Wajerumani walianza kuingia Turuland , Iramba na Isanzu wakitokea boma la Kilimatinde - Manyoni walikoweka kambi ya kimkakati .

Mwaka 1902 Jeshi la wajerumani wakitumia farasi , Huko Iambi  lilivamiwa na wapiganaji wa kienyeji na kupewa kichapo kikali sana baada ya KITENTEMI kuituma mvua iliyowavuruga wajerumani na kuona Giza tupu hivyo kupewa kipigo cha uhakika na kukimbia eneo la Pambano kwa amri ya Sajenti Zahn . Maafisa wawili wa jeshi la kijerumani waliuawa na wapiganaji wa kinyiramba na wanyisanzu .

Inaelezwa wajerumani walikimbia kama watoto pamoja na bunduki zao kutoka Iambi na kurudi Mkalama ambapo Sajenti Zahn ilibidi aombe msaada kutoka ngome yao kubwa ya Mpwapwa na kikosi kilitumwa haraka kuja eneo la vita , awamu hii wajerumani walipata ahueni baada ya kufanikiwa kumsaka na kumkamata KITENTEMI mtaalamu wa mvua na akachukuliwa toka Mkalama kupelekwa Kilimatinde-Manyoni  na kunyongwa . kifo cha KITENTEMI ilikuwa ni pigo kwa wapiganaji wenyeji ambapo Pambano la pili waliweza kuuawa wengi sana na kushindwa na wajerumani wakapata nguvu ya kuweka kambi Mkalama na kujenga boma lao lililoanza kujengwa 1902 na kukamilika 1910 .

Kabla ya vita na wajerumani KITENTEMI anatajwa pia kushiriki vita kati ya Wanyisanzu na wamasai waliovamia Mkalama kwa ajili ya kuiba na kupora ng'ombe ambapo alituma mvua ya mawe umbali wa  mita 500 na kuwasambaratisha wamasai .

Inaelezwa mtoto wa Dada yake KITENTEMI aliyeitwa KALI na mdogo wake wa kike aliyeitwa NYAMATALU  alimaarufu ANYAMPANDA walirithi Sayansi ya kutengeneza mvua ila haikuwa na nguvu na baadaye walihama kutoka Mkalama na kuhamia eneo la WAHADZABE upande wa kaskazini mwa Mkalama na hali ya amani ilitulia na vita viliisha .

Baadae KALI na NYAMATALU walirudi Mkalama ambapo KALI alitawazwa na wajerumani kuwa Chief au MTEMI KALI wa Mkalama na NYAMATALU alipewa kazi kwenye ofisi za wakoloni .

Chief KALI alifariki mwaka 1927 akiwa Mzee sana na nafasi hiyo kuchukuliwa na Mtemi  SAGILU (Sakilu) au ASUMANI mpaka alipofariki mwaka 1939 na kumwachia Mtemi Gunda .

Mwandishi wa makala hii ni ndugu ALFRED RINGI ni mwanahistoria aliyemua kufuatilia na kuwaibua mashujaa wetu waliosahaulika ili waweze kutambuliwa na kuwa sehemu ya Historia ya nchi yetu . Taarifa nyingi zilizofichwa zipo kwenye makumbusho ya Wakoloni wetu huko Ujerumani  .habari ni kwa msaada wa Maandiko na Simulizi za Wazee .( Oral and Written sources )

Ijumaa, 6 Desemba 2019

MKAPA ALIKUWA KIJANA WA NYERERE

MKAPA ALIKUWA KIJANA WA NYERERE

Nimemaliza kusoma kitabu cha mzee Mkapa na nilichojifunza ni kuwa Mkapa alitengenezwa na Mwalimu Nyerere.

Mkapa alianza kufundishwa na Nyerere St. Francis College Pugu katika mwaka wa mwisho wa Mwalimu kuwa pale ni wakati Mkapa alikuwa amejiunga hapo mwaka 1955 alimfundisha Kiingereza kwa muda mfupi kabla ya kujuliuzulu mwezi Machi 1955.

Baada ya kumaliza Makerere Mkapa alitaka kujiunga na wizara ya mambo ya nje lakini kwa kuwa hakuwa na uzoefu ilibidi aingie kwanza Serikalini na alipelekwa kuwa District  Officer Cadet  Dodoma Aprili 1962.

Agosti 1962 alikwenda Columbia University ili kusoma kozi ya Foreign Relations. Kozi ambayo ilimfanya kufanya kazi Wizara ya Mambo ya nje na Mwaka 1963 Alianza kazi Mambo ya nje wakati huo waziri akiwa Oscar Kambona akiwa kama Foreign Services Officer grade 3. Na hapo ndipo alipoanza kufanya kazi kwa karibu na Mwalimu kazi yake hasa ikiwa ni kuandika notes wakati Mwalimu au Kambona alipotembelewa na wageni kutoka nje. Pia alifanya kazi ya kusoma habari Radio Tanzania kutokana na umahiri wake wa kujua vizuri Kiingereza.

Anasema Jioni mmoja baada ya kusoma habari aliambiwa kuwa alikuwa akiitwa na Mwalimu Msasani na alipofika Mwalimu alimwambia kuwa alitaka awe Mhariri wa gazeti la chama The Nationalist. Baada ya Mkapa kusema kuwa hakuna tabu isipokuwa hakuwa na uzoefu na magazeti Mwalimu alimwambia kuwa atamfanyia mpango wa kwenda UK kujifunza.

Baada ya kutoka UK aliajiriwa kama Mhariri wa The Nationalist na Mwalimu mwenyewe akiwa Mhariri Mkuu ( Editor in chief). Kupitia gazeti hilo Mwalimu akisaidiana  na Mkapa waliweza kueneza Siasaa na Propaganda za chama cha TANU. Pia Nationalist na The Standard yaliunganishwa na kuwa Daily News ambalo Mkapa alikuwa Mhariri wake Mkuu wa kwanza Aprili 1972.

Baadae mwaka huo wa 1972 Mwalimu alimteua kuwa Mwandishi wake binafsi na anasema ilibidi amfuate Butiama kuanza kazi kwa kuwa alikuwa likizo huko wakati anafanya uteuzi kazi ambayo alifanya kwa muda wa miaka miwili. Katika kipindi hicho alifanya kazi kwa karibu na katibu myeka wa Rais Joan Wickens na alikuwa akiambatana na Mwalimu katika Mikutano hasa ile ya Nchi zilizokuwa Mstari wa Mbele wa Ukombozi wa Kusini mwa Afrika.
Mwaka 1974 Mwalimu alimwambia aanzishe Shirika la Habari la Taifa( SHIHATA) na alikuwa Mtendaji wake Mkuu kwa miaka miwili.

Aliteuliwa kuwa balozi Nigeria mwezi Oktoba 1976  na baadae kuitwa kuwa Waziri wa mambo ya nje Februali 1977. Anasema huo ndio ilikuwa mwanzo wa safari yake ya Kisiasa. Mwaka 1977 aliteuliwa kuwa Mbunge kupitia Ushirika na Mwaka 1985 alisimama kugombea Ubunge wa jimbo la Nanyumbu na pia Mwaka 1990 alitetea kiti chake. Mwaka 1995 hakugombea.

Anasema Mwalimu alikuwa akimtegemea sana na kwamba kati ya 1976 hadi 1985 wakati Mwalimu anastaafu alifanya kazi sehemu mbalimbali ikiwemo  Nigeria1976, Canada 1982, USA 1883-84, alikuwa Waziri wa nje mara mbili 1977-1980 na pia 1984 -1990 pia kama waziri wa Habari na Utamaduni 1980-1982.

Baada ya Mwinyi  aliendelea kuwa waziri wa Mambo ya Nje  kabla ya kuwa Waziri wa Habari na Utangazaji 1990-1992 na Waziri wa Sayansi Teknolojia na Elimu ya juu 1992-1995  . Anasema hamahama hiyo ilikuwa ngumu kwa familia yake hasa kuhamisha watoto shule mara kwa mara. Hata hivyo anamshukuru Mke wake Anna ambaye alikuwa muelewa. Kuna kipindi anasema ilibidi watoto wao wabaki Marekani ili kuweza kukamilisha masomo yao.

Mkapa anaelezea kuwa baada ya kipindi cha Mwìnyi kufikia ukingoni aliona baadhi ya watu waliokuwa wametangaza Nia kuwa hawakutosha na kwamba angeweza mwenyewe kupokea kijiti. Baada ya kushauriana na mkewe na kuungwa mkono ilibidi amtumie ujumbe Mwalimu akimueleza kuwa anataka kugombea urais, na baadae alikutana naye na kumueleza   sababu zake za kufanya hivyo:-

Mosi, kuwa Mahusiano ya chama na Serikali hayakuwa mazuri na pia Vyama vya Ushirika ambavyo Mwalimu alikuwa amavipigania na vilikuwa imara wakati kudai uhuru na wakati wa utawala wake vilikuwa vikilegalega, kwamba viongozi wa Ushirika walikuwa wamejifanya wamiliki na wezi

Pili, kuwa Vyama vya Wafanyakazi ambavyo vilikuwa imara na watu kama Rashid Kawawa wakiwa Wawakilisha wa Trade Unions waliendesha harakati za kudai Uhuru, lakini Kulikuwa na migogoro na Chama cha Wafanyakazi walikuwa wametishia kuitisha mgomo.

Tatu, alimwambia kuwa Mwalimu alikuwa ameacha uhusiano mzuri na nchi za Nordic ambao walikuwa wafadhili lakini kwa wakati huo walikuwa wameacha kutoa misaada.

Nne, alisema kuwa ingawa Mwalimu alikuwa hapendi IMF na Benki ya Dunia lakini walikuwa wameanza kuonesha namna ya kusaidia katika kuinua Uchumi, hata hivyo walikuwa pia hawana tena imani na Serikali.

Mwisho, Mkapa alisema alikuwa ameona watangaza nia wengine na kuona walikuwa hawatoshi na kwamba nafsi ingemshitaki asingejaribu kurusha karata yake.

Mwalimu baada ya kumsikiliza Mkapa alimwambia kuwa japo hakumpigia chapuo na kuwa kulikuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa akimfikiria lakini mtu huyo alitaka kama vile kubembelezwa. Basi akasema atamuumga mkono. Hivyo ndivyo Mkapa alivyotangaza Nia baada ya hapo, na kufanikiwa kuupata Urais.

Mkapa pia anaongelea Ubinafsishaji na jinsi Mwalimu  hakupenda hasa uuzaji wa NBC. Anatetea kuwa Mwalimu baada ya kueleweshwa alielewa na hakuwa na neno na Ubinafsishaji wa NBC. Hasa baada ya kuunda NMB, Anaendelea kusema kuwa Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma ulikuwa wa lazima na kuwa hakuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuyapiga mnada wa jumla

Mwalimu pia alifurahia misamaha ya madeni kutoka Paris Club ambayo ilanzishwa wakati wa Mkapa na anasema wakati akiwa kitandani Katika Hospitali huko London Mkapa alimpigia simu na kumwambia nchi ilivyosamehewa baadhi ya madeni ,anasema ndio ilikuwa simu ya mwisho kwa Mwalimu kabla ya kuaga dunia na kwamba alifurahi sana.

Mkapa anasema katika kutekeleza malengo aliyokuwa amesema angeyarekebisha wakati akiomba ridhaa ya Mwalimu aweze kugombea ni kuwa:- Aliunda time ya Warioba kuhusu mianya ya rushwa na baadae akaunda PCB,
Pia aliunda Tume ya Makinda na Kahama kuhusu Ushirika, na baadae alimteua Sir. George Kahama kuwa Waziri wa Ushirika na Masoko japo anasikitika kuwa baadae Kikwete aliivunja hiyo Wizara na Ushirika ikawa Idara kwenye Wizara ya Kilimo

Kuhusu Mahusiano ya Kimataifa pamoja na IMF na Benki ya Dunia anasema alifanya vizuri sana na kuwa alikuwa na Mahusiano ya Karibu ya kikazi na Viongozi wa Taasisi hizo kiasi kwamba mwaka 2001 Horst Kohler na James Wolfensohn walifanya mkutano na wakuu wa nchi za ukanda huu hapa Tanzania,
Pia waliendelea kufadhili miradi mkubwa kama barabara.

Mkapa alifanikisha kuunda Mamlaka za Serikali kama TRA, Wakala za Serikali kama TANROADS, Taasisi za udhibiti, Taasisi na mifuko ya kuinua Wananchi kama MKUKUTA, MKURABITA nk.

Pamoja na mafanikio Mkapa anasema kuna baadhi ya mambo hayakwenda vizuri katika utawala wake ikiwemo mauaji ya Zanzibar, pamoja na wizi wa EPA.

Mzee Mkapa ameandika, Wazee wengine nao waige.

Sylvanus Kamugisha
Dar es salaam.
6, Desemba, 2019.

Alhamisi, 14 Novemba 2019

UCHAMBUZI WA KITABU CHA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA "MY LIFE, MY PURPOSE"

UCHAMBUZI WA KITABU CHA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA "MY LIFE, MY PURPOSE"

Na PROF. RWEKAZA MUKANDALA
____________
Mtoto Benjamin William Mkapa, alifundishwa kupika chakula na mama mzazi Stephania akiwa mdogo. Alipokwenda shule hapo kijijini Lupaso, Ndanda na hatimaye St. Francis Pugu na Makerere, alifundishwa kupika, kufinyanga, kubuni na kuchambua mawazo na kuyaweka sawa kama msomi mbunifu na mwandishi. Kitabu hiki ni zao la mpishi wa mawazo mahiri aliyebobea.  Ni kitabu cha kurasa mia tatu na kumi na tisa, katika sura ya kumi na sita.   Kuna utangulizi ulioandikwa na Mheshimiwa Joaquim Chissano, Rais mstaafu wa Msumbiji, Pia kuna picha nyinge nzuri, na viambatisho viwili.  Mchapaji Mkuki na Nyota wamefanya kazi nzuri sana, sikubaini kosa hata moja.

Wasilisho hili linamega simulizi hii katika sehemu kuu tatu. Kwanza tunapewa vionjo vitamu tukielezwa kuzaliwa kwake, kukua na kwenda shule. Hii ilikuwa matayarisho ya kufikia nia au azma yake ya maisha. Kisha tunaletewa mlo wenyewe (main course) uliosheheni kumbukumbu  na ngano za huyo kijana sasa mtu mzima akiwa kazini, mpaka akaukwaa urais wa Tanzania. Mwisho tunaelezwa kwa ufupi maisha yake baada ya kumaliza ngwe yake ya miaka kumi ya urais.

2.      KUZALIWA, MALEZI NA ELIMU

Baba yake mzazi Mheshimiwa Mzee William Matwani alikuwa mpishi msaidizi huko Mission Ndanda. Wamisionari wakambatiza, wakamfundisha kusoma, kuandika na kuhesabu, na kumfanya Katekista. Alipelekwa Lupaso, ambapo alieneza dini na kufundisha Bush school ya Wamisionari. Alimwoa Bibi Stephania Nambanga ambaye hakujua kusoma wala kuandika. Walijaliwa watoto wanne Benjamin akiwa wa mwisho. Kama ilivyo kwa kabila la Makua, Benjamin alipewa jina la ujombani, Mkapa. Mama hakuwa na muda wa kujifunza kusoma na kuandika kwani yeye ndiye alikuwa msingi wa familia, akihakikisha analima, kulisha familia, na kuwalea watoto.  Alikuwa mkali lakini msikivu na mpenda haki. Wazazi hawa ndio vinara wa sehemu hii ya kwanza ya simulizi hii. Waliishi pamoja kwa uadilifu na heshima kubwa, na mapenzi ya pamoja kwa watoto wao.

Ingawa wazazi hawakwenda shule, walipenda sana watoto wao wote waende shule. Hii pamoja na kwamba Baba Matwani alikuwa na kipato kidogo lakini cha uhakika kila mwezi, kiliifanya familia ionekane iko tofauti. Hii ilipelekea wivu na hatimaye chuki kutoka kwa jamii. Wivu huu na chuki ulisababisha tukio moja baya sana ambalo Mheshimiwa Mkapa analikumbuka kwa uchungu. Mwaka 1947, kulitokea ukame mkali, basi watu wakamleta mganga wa kienyeji akaamua kuwa mama mzazi, mama yake na bibi yake ndio walikuwa wameloga na kuzuia mvua. Walipigwa na kuteswa sana hadi Padri Mzungu alipofanikiwa kuwanasua. Bibi wa mama aliaga dunia muda mfupi baada ya tukio hilo.

Kijana Benjamini na mwenzie mmoja ndiyo waliopata bahati ya kuendelea na masomo ya Sekondari, kutoka darasa la watoto 25 hadi 30.   Kuchaguliwa ilikuwa bahati nasibu.

Shule ya sekondari ya Ndanda ilikuwa kilometa 60 kutoka Lupaso. Yeye na wenzie walitembea kwa miguu, bila viatu, kwa siku mbili, wakiwa wamebeba kichwani vitu vyao ambavyo vilikuwa vimefungwa katika mkeka. Baadae alipata sanduku la chuma.

Walimu wa Ndanda walikuwa wamisionari na walikazia sana sala na kazi “Ora et labora’’.   Wanafunzi walipika chakula chao wenyewe. Kwa kuwa kijana Benjamini alikuwa mdogo sana alipewa kazi ya kuosha vyombo. Kawaida alivibeba vyombo kichwani mpaka mahali pa kuvioshea, na kuvirudisha. Anasema kubeba vyombo hivyo ndiyo sababu ana upara hadi leo

Mwaka 1952, akiwa na umri wa miaka 15, aliamua kwenda Seminari darasa la nane. Baada ya muda mfupi aliamua kuwa upadre haukuwa wito wake, akarudi Ndanda kuendelea na shule. Mwaka 1957, alichaguliwa kwenda St. Francis College Pugu ikiwa ni shule kuu ya Wakatoliki Tanganyika.  Akiwa Pugu, kijana Benjamini alianza kupata mwamko wa kisiasa. Aliunga mkono harakati za kupata uhuru kwa kuandika barua kwa Mhariri wa Gazeti la “Tanganyika Standard” ambalo sasa ni Daily News akiunga mkono hoja ya Uhuru. Barua ilichapishwa. Ila kijana Benjamini alitumia jina bandia!

Mhe. Mkapa alishinda mitihani yake ya kujiunga Chuo Kikuu Makerere, kwa kupata daraja la kwanza, akiwa kati ya wanafunzi watatu bora katika darasa la wanafunzi 51.

Makerere alikumbana na mambo mengi mapya: Alikuwa darasani na wanafunzi wa rangi tofauti, kwa mara ya kwanza alikwenda kucheza dansi ya kisasa, alipangiwa chumba cha kulala nk.

Mwamko wake wa kisiasa uliendelea.   Alijiunga na Bodi ya Wahariri ya gazeti la “Transition”; alikuwa mwanachama hai wa kikundi cha wanafunzi cha TANU, akiwa katibu na hatimaye mwenyekiti wake. Alishiriki  kwenye siasa za wanafunzi hapo chuoni. Aligombea Urais na ingawa hakushinda, wanafunzi wa kike walimpigia kura nyingi si kwa sababu alikuwa  na rafiki wa kike, ila kwa jinsi alivyoweza kujieleza kuliko mpinzani wake. Alikuwa ‘More articulate!’ Aliteuliwa Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi, na hatimaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la wawakilishi la wanafunzi hapo Makerere. Alihitimu masomo yake Aprili 1962, miezi minne baada ya Tanganyika kupata Uhuru. Alipata shahada ya lugha na fasihi ya kiingereza na fonetiki.  Alikuwa tayari kuifukuzia nia na ndoto yake.

3.      MAISHA NA KAZI

Simulizi ya maisha ya utu uzima iko katika sehemu mbili.  Kwanza ni alipoanza kazi mpaka alipogombea Urais.  Pili ni maisha ya Urais.  Sehemu hii ya simulizi imejaa sifa heshima na upendo mwingi kwa Mwalimu. Anastaajabu kwa jinsi Mwalimu alivyoiunganisha nchi katika kupigania vita vya ukombozi wa bara la Africa.  Kama wazazi wake mzee Matwani na Bibi Nambanga walikuwa mashujaa wa sehemu ya kwanza ya maisha yake, hakika Mwalimu ndiye shujaa katika sehemu hii ya pili.   Anamueleza Mwalimu kama labda alitumwa na Mungu kwa makusudi (Almost divine intervention).

Akiwa mtu mzima na mhitimu wa Chuo Kikuu Makerere Mheshimiwa Mkapa alipenda kuajiliwa kwenye Wizara ya mambo ya nchi za nje: Kwanza ilishindikana lakini, baadae akaambiwa, itawezekana kama ataajiriwa kwanza kama bwana shauri mkufunzi wa Wilaya, wakati akisubiri.  Kwa hiyo aliajiriwa hivyo huko Dodoma April 1962.

Baada ya miezi minne August 1962 aliitwa Dar es salaam aende kujifunza udiplomasia Columbia Marekani.

Baada ya mwaka mmoja alirudi nchini akaajiriwa wizarani.  Kazi yake kubwa ilikuwa kuchukua muhtasari wa mazungumzo Waziri wake au Mhe. Rais alipopata wageni.  Anamsifia kwa ujasiri pale alipovunja uhusiano na Uingereza.   Wakati huu Mhe. Mkapa alitumia muda wake binafsi ama kusoma habari Radio Tanzania Dar es salam, ama kumchumbia Bi Anna.

Siku moja aliambiwa anaitwa Msasani kwa Mwalimu. Walipaita Msasani nyumbani kwa Mwalimu “The Clinic”.  Mwalimu akamwambia anamteua kuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la The Nationalist.  Ilibidi aende Uingereza kujifunza mambo ya magazeti kwenye magazeti ya The Mirror.

Alirudi na kuanza kazi chini ya Mwalimu kama Mhariri Mkuu, Mhe. Mkapa alikuwepo Arusha wakati wa Azimio mwenzie Nsa Kaisi ndiye aliyebuni neno la Arusha Declaration, walilitumia kwenye The Nationalist, Mwalimu akalipenda, basi hayo maamuzi yakaitwa hivyo.

Mhe. Mkapa aliruhusiwa kuhudhuria mikutano ya kamati kuu ya TANU, ambayo wakati ule ilitawaliwa na malumbano ya hoja na uchambuzi yakinifu ambao umepotea.  Alihusika katika kutayarisha sera mbalimbali za chama kutokana na umahiri wake wa kumudu lugha.

Mwalimu na msaidizi wake Joan Wicken ndio walio mfundisha ujamaa na alivutiwa na msimamo wa usawa na umuhimu wa kujitegemea.  Aliunga mkono wazo la Jeshi la Kujenga Taifa na akamuomba Mwalimu akamkubalia ajiunge kwa hiari.   Alijiunga na kuhitimu.  Siku ya kuhitimu Mwalimu alikuwa ndie mgeni rasmi.  Mheshimiwa Mkapa alichaguliwa na wenzie kusoma risala na Mwalimu alicheka sana alivyomtambua kuwa ni yeye kwani alikuwa amepoteza ratili nyingi za uzito.  Alikuwa slim fit.  Mheshimiwa Mkapa aliitwa huko “The Clinic” Msasani mara kadhaa.

April 1972 Mwalimu alimteua kuwa Mhariri Mtendaji wa Daily NewsMuda mfupi baadaye Mwalimu alimteua kuwa Press Secretary wa Rais.  Anasema huu ndio ulikuwa mwanzo wa maisha yake kama mwanasiasa.Mwaka huohuo, Mwalimu alimuagiza aanzishe Shirika la Habari Tanzania – SHIHATA na kuwa Mtendaji Mkuu wake.Mwaka 1976 akamteua Balozi huko NigeriaMwaka mmoja baadaye akaitwa tena “ The Clinic” na kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje.  Hapa alikuwa kama msaidizi wa Rais kwani Mwalimu ndiye aliyeendesha mambo ya Nchi za Nje. Alifanywa pia Mbunge wa kuteuliwa .Aliteuliwa kuwa Balozi wa Canada 1982Balozi Marekani 1983 – 1984Akateuliwa waziri wa habari na utamaduni 1980 – 1982Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje tena 1984.  Anabaini kuwa kwa kweli Mwalimu aliipa familia mtihani mkubwa na hii hamahama, lakini familia chini ya mama Anna walikubali na kupokea yote kwa mikono miwili

Hakika Mwalimu ndiye shujaa mkuu wa simulizi hii.  Mheshimiwa Mkapa anamueleza Mwalimu kuwa:

Alikuwa jasiri, na kiongozi lazima awe jasiriAlikuwa msikivu, kamwe hakumkatiza mtu hata kama alikuwa anaeleza pumba tu.Alikuwa mtu wa msimamo, hakuyumbayumbaAlikuwa mpatanishi na mjenga madaraja kuwaunganisha mahasimu.Alikuwa communicater wa ajabuAlikuwa fundi wa kutafuta sehemu za makubaliano kati ya wanao tofautianaAlikuwa mtaalamu wa kutumia mawazo ya wengine kurutubisha na kuboresha ya kwakeAliupa umuhimu wa kipekee Umoja wa KitaifaHakupenda ukandamizaji ndio sababu hakupenda kuikalia Uganda baada ya vita 1980

Mheshimiwa Mkapa anasema “Mwalimu alikuwa mwalimu wangu kwa kila kitu”.

Alikuwa mwana demokrasia mtu aliyempenda kama mrithi wake mwaka 1985  alipokataliwa na wenzie katika kamati Kuu, Mwalimu alikubali.Alikuwa kiongozi mwenye maono – visionary, alingalia maslahi na mustakabali wa Taifa ndani na nje ya mipaka yake.

Wazazi wa Mheshimiwa Mkapa walifariki akiwa Waziri, wakiwa na furaha na faraja kwa mafanikio yake, ingawa hakuwa Padre, Daktari au Mwalimu kama baba yake mzazi mzee Matwani alivyotaka.

URAIS

Baada ya kutafakari na kushauriana na rafiki zake, Mheshimiwa Mkapa kwanza alimwambia mama Anna juu ya kugombea Urais.  Mama Anna alisita kidogo ila akakubali.  Pili alimueleza Mwalimu kwa barua kwani alikuwa Butiama, kisha akukutana nae ana kwa ana.  Alimpa mwalimu sababu kuu nne za uamuzi wake wa kutaka kugombea.

Kwanza alitaka kurekebisha na kurejesha uhusiano chanya kati ya chama na serikali yake, na vyama vya ushirika ambao ulikuwa umefifia. Pili, alitaka kuhimarisha uhusiano na vyama vya wafanyakazi ambao walikuwa wanatishia kugoma kwa mara ya kwanza. Tatu, ilikuwa kurekebisha mahusiano mabaya na wahisani kuhusiana na kushamiri kwa rushwa. Nne, alitaka kurudisha uhusiano na mashirika ya fedha ya kimataifa ambao walikuwa wamekataa kuanzisha miradi mipya.Mwisho aliwapima hao waliokuwa wamechukua fomu akaona atajilaumu hapo baadae kama naye hata gombea.

Mwalimu alimshukuru, akamwambia hakuwaza kuwa nae angegombea, alikuwa anamfikiria mtu mwingine ambaye alikuwa anasita sita.  Akamwambia hatamzuia kama amefanya uamuzi huo.  Mwalimu aliwaomba watu kadhaa kumuunga mkono, Mwalimu alipenda hasa uwezo wake wa kufanya maamuzi, Mwalimu alishiriki katika kampeni ambapo Mheshimiwa Mkapa alisisitiza ilani, sio mambo binafsi.  Mdahalo wa wagombea wote ambao ulirushwa mubashara ndio ulimfundisha njia ya  ushindi.   Ulikuwa “Game Changer” anasema.

November 23, 1995 aliapishwa kuwa Rais.  Katika kuunda Baraza la Mawaziri, Mwalimu alikataa kujihusisha hakuwa muingiliaji – interventionist.  Mheshimiwa hakuwa mgombea wa mtu kwa hivyo hakuna aliyetegemea fadhila.

Hali ya nchi ya uchumi ilikuwa mbaya sana lakini anasema sikuogopa, kiongozi lazima awe jasiri.   Alikumbana na uzembe, kutowajibika na rushwa.

Kazi kubwa - kwanza ilikuwa kuwashawishi wahisani kuwa mambo yatabadilika.   Nchi ilikuwa na madeni makubwa sana.  Deni letu lilikuwa dola bilioni saba, tulisamehewa bilioni tatu, hii ilikuwa hatua kubwa sana na ilimfurahisha Mwalimu ambaye alishaanza kuumwa.

Mheshimiwa aliamini tulihitaji kujiangalia upya na kujifikiria kimkakati upya namna tulivyo kuwa tunaendesha nchi.

Mheshimiwa anasema kuwa walio iona staili yake ya “Kusema na kuelekeza” kuwa ilijaa kiburi na majivuno ilikuwa lazima kuonyesha kuwa hata tetereka.

Matokeo yake ni kwamba mapato yaliongezeka karibu mara tatu kutoka dola 612,587 mwaka 1995 kufikia dola 1,796,862 miaka kumi baadae. Fedha za kigeni ziliongezeka kutoka uwezo wa kununua bidhaa za mwezi mmoja na nusu kufikia uwezo wa kununua bidhaa za miezi mitano na theluthi moja.  Riba za benki ilishuka kutoka asilimia 36% kufikia asilimia 15% mwaka 2005.

Ilianzishwa TRA kuimarisha ukusanyaji wa mapato Julai 1996.Ukaanzishwa mfumo wa VAT Julai 1998Public Service and Act pamoja na Public Procurement Regulatory Authority vilianzishwa 2001Commision for Human Rights and Good Governance ilianzishwa Julai 2001Prevention of Corruption Bureau nayo ilianzishwa, Mheshimiwa akaitwa Mr cleanRegulatory Agencies nyingine zilianzishwa nyingi ikiwa ni pamoja na Brela, EWURA, TCCRA,SUMATRA, Viwanja vya ndege,Maji safi na taka, TANROADS,na National Business Council kuhimarisha mahusiano na wafanya biashara.

Kati ya mageuzi tuliyofanya yaliyokuwa na utata sana ni kubinafsisha mashirika ya Umma, mageuzi/maboresho ya utumishi, na uuzaji wa nyumba za Serikali.

Kwa kweli mashirika ya Umma yalikuwa yanaendeshwa kwa hasara. Kuna wanaodai kuwa Mwalimu hakkupenda ubinafsishwaji na alisema hivyo hasa wakati wa mtangulizi wake.  Mheshimiwa Mkapa anabaini kuwa, lakini Mwalimu hakunisema ana sijui kwa nini, ukweli ni kwamba Mwalimu alikuwa pragmatist na aliona hali halisi.  Kwa bahati mbaya sikufuatilia utendaji wa mashirika Mheshimiwa Mkapa anaendelea  mashirika tuliyo yaabinafsisha kama ambaavyo nilivyofanya kwa Regulatory Agencies.  Pia kweli kuwa tulibinafsisha kwa watu wan je kuliko wazawa.

Pamoja na ugumu na utata wa baadhi ya mageuzi kura zake katika uchaguzi wa mwaka 2000 ziliongezeka kwa asilimia 100%.  Hii kwake ilikuwa kuambiwa “Songa mbele, endelea”  Na niliendelea, anasema.

Mheshimiwa Mkapa anasimulia kuwa maono yake:  ni maisha ya hali ya juu, amani, utulivu na umoja, utawala bora,jamii iliyoelimika na uchumi shindani wenye uwezo wa kukua kiendelevu na mgawanyo shirikishi wa kipato.  Ili kuyapata hayo ikaanzishwa

Vision 2025MKUKUTAMKURABITAMini Tiger Plan 2020TASAF.  Wengi katika Baraza la Mawaziri, kwenye Chama na Serikali hawakuviunga mkono.  Lakini sasa naiona TASAF kama “High Point” ya Urais wangu, anasema Mheshimiwa Mkapa.Bima ya TaifaMageuzi katika Elimu, DEDP na SEDPMradi wa maji ziwa Victoria,

Kuhusu mahusiano ya ndani na nje, Mheshimiwa Mkapa anabaini kuwa uhusiano katika ya Bara na Zanzibar ulikuwa mgumu na tete lakini alifanikwa kutatua matatizo.

Anasema alikuwa na wasiwasi pale Rais wa Zanzibar Salmin Amour alipotaka kubadilisha sheria na kutawala kipindi cha tatu.  Lakini baadae yeye na wafuasi wake wakaamua yaishe.

Zanzibar ilianza kupeperusha bendera yake.

Vifo vya watu 22 huko Pemba Januari 2001 vilinishtua na kumhuzunisha sana.  Anasema “hili litaendelea kuwa doa katika Urais wangu ingawa sikuwepo lilipotokea”.

Anabaini kuwa wakati wa utawala wake, wanadiplomasia walionyesha upendeleo kwa vyama vya upinzani na kukutana nao mara kwa mara,  Pia wapo walioamini walistahili upendeleo kuliko wengine.

Kwa upande wa vyombo vya habari ilibidi azoee kukosolewa, kwani waliamini alikuwa dictator ingawa alikuwa anashikilia msimamo. Anabaini kuwa alihitaji kuuza sera zake, kwa hiyo akaanzisha utaratibu wa kulihutubia Taifa kila mwezi lakini mhimili mkuu wa kupokea na kutoa mawazo na habari ilikuwa Chama chake CCM na vikao vyake mbalimbali.

Mheshimiwa Mkapa anakiri kuwa, Kabla hajawa Rais, hakujua kuwa kazi moja wapo ya Rais ni kutoa pole. Moja wapo ya mapungufu yangu ni kwamba si mwepesi wa kuonyesha hisia zangu. Mrithi wangu Rais kikwete ni mzuri sana katika hili.  “Anasema Mheshimiwa Mkapa.

Mwaka 1996 mafuriko yalisababisha maafa makubwa katika Nchi.Kuzama kwa Mv bukoba kulistua na kuhuwisha sana majanga mengine mengi.Niliwahurumia wafungwa wote waliostahili kunyongwa mpaka kufa.

Anasema ingawa hakatai kukosolewa kisiasa au kisera, kukosolewa binafsi kuliumiza sana.  Kwa mfano madai kwamba alimpendelea Baba mkwe wa mwanae katika kubinafsisha mgodi wa makaa ya mawe wa kiwira yalimuumiza sana.

Pia madai kuwa aliwapendelea NET GROUP solutions ltd  wakati wa kubinafisha TANESCO kwa sababu ya shemeji yake kulimuumiza sana pia  jambo moja lilojitokeza baada ya muheshimiwa kumaliza muda wake ni la External payment account (EPA). Mheshimiwa anaeleza kuwa, anavyoelewa urais wake haukuwa wa kwanza kuruhusu ununuzi  wa madeni kama huo. Anasema kwanza alisita ila Gavana wa Benki Kuu Daud Bilali alimuelewesha na akasema watakao nunua hayo madeni walikuwa tayari kuchangia mfuko wa kampeni za uchaguzi wa CCM. Wahuni walitumia uaminifu wake kwa chama kumshawishi akubali. “Ninajisikia kuwa nilitumika na kusalitiwa. Na ukweli ni kwamba mimi binafsi sikufaidika na sikupata chochote”.  Anasema Mheshimiwa Mkapa.

Kuna kukosolewa kuhusu matumizi ya anwani ya Ikulu wakati mimi na mke wangu tulipochukua mkopo NBC kununua nyumba. Ukweli ni kwamba wakati ule tulikuwa tunaishi Ikulu, tulichukua mkopo kwa mashart ya kawaida ya biashara.  Kabla sijaondoka Ikulu, nilimaliza malipo ya mkopo huo na mshahara wangu wa mwisho na mafao yangu, tukapewa hati ya nyumba hiyo.  Anasema Mheshimiwa Mkapa.

Kulikuwa pia na swala la RADAR ambayo ilkuwa lazima kuinunua kuimarisha ulinzi lakini manunuzi yaligubikwa na udanganyifu na hatimaye hela zilizolipwa za ziada zilirudishwa kwa Serikali.

Anafikiri ni muhimu kutazama upya suala la umiliki wa uchumi ili watu wengi zaidi wahusike.  Kuendelea kushamiri kwa umiliki hasa wa viwanda na mashamba makubwa na makampuni ya Kiasia au Kihindi inaweza ikaleta wivu, na kuleta shida kubwa.  Ana wasiwasi na siku za mbeleni kwani umaskini uenda bega kwa bega na uvunjifu wa amani.  Lazima tujiulize kama tunajikita katika utulivu na amani.

Anamalizia kwa kutoa ushauri kwa viongozi wa wakati ujao (future).

Onyesha nia na bidii kwa majukumu upewayo.Uwe tayari kuwashirikisha wengine katika mawazo, mafanikio, matatizo na upimaji utekelezaji, consult more.Usifanye kazi kwa kukurupuka na kutotabirikaFuata  na tii sheria na taratibuUwe tayari kusikilizaMtafute mlezi (mentor) kama mimi nilivyokuwa na Mwalimu.

Katika sehemu anabainisha umuhimu wa mke wake mama Anna Mkapa.  Mapema kabisa katika ukurasa wa 83.  Mheshimiwa anampa saluti mama Anna kwamba yeye ndiye gundi iliyo shikilia familia. Anakiri kuwa yeye Mheshimiwa Siyo mtu rahisi kuishi naye na anamshukuru kwa kuwa mtu wa subira na uwezo mkubwa.  Amevumilia mengi wakati wa safari za mara kwa mara, kutokuwepo nyumbani mara nyingi na  ndiye alibeba mzigo wa kuwalea watoto wao wawili.

4.      KUSTAAFU

Sehemu ya tatu naya mwisho ya simulizi hii, ni maisha ya mheshimiwa baada ya kustaafu Urais.

Kwanza Mheshimiwa ametumika sana Kimataifa katika nyadhifa na Taasisi mbalimbali ingawa hapendi kusafiri, Taasisi hizo ni pamoja na

Club de Madrid The African Wildlife FoundationInvestment Climate Facility for AfricaUN Iniative “Delivering as One”UNCTAD Panel of Environment Persons.UN Commission on the Legal Empowerment of the PoorMwenyekiti wa Seventh Centre tangu 2006Trustee the Aghakhan UniversityThe Mkapa Foundation

Kote huku amejichanganya na watu wenye akili nyingi.

Pili, amehusika sana katika upatanisho wa migogoro huko South Sudan, Congo Mashariki, na Kenya.

Mheshimiwa Mkapa, anamalizia simulizi hii kwa kugusia mambo kadhaa.

Kwanza, anaona Rais mstaafu anathaminiwa zaidi uongozi na uwezo wake Kimataifa zaidi kuliko nyumbani, jambo ambalo hata Mwalimu aliliona.  Mara nyingi huitwa kwenye hafla ambapo anakuwa kama Ua au pambo ukutani, lakini natakiwa kwenye kazi muhimu na nyeti za kitaifa.Pili, anaongelea umuhimu wa kuanzishwa kwa Baraza dogo kama sehemu ya  Bunge kupitia miswada iliyopitishwa na Bunge kabla ya utekelezaji.Tatu, anazungumzia kukosekana kwa itikadi na fikra pevu za kina juu ya mustakabali wa Taifa letu.  Inabainishwa kuwa tunahitaji ukombozi wa pili, Kisiasa, Kiuchumi, Kiutamaduni.  Tunahitaji kama Taifa, na mtu mmoja mmoja kuona aibu kuwa ombaomba.  Tunahitaji kujitegemea na kuthamini uendelevu (sustainability) wa maendeleo.Nne, anagusia mwendo wa goigoi katika kuimarisha Jumuia ya Afrika Mashariki (EA).  Sioni juhudi kubwa, naona siasa tu, watu wamepoteza picha kubwa – Big Picture. Tano, anagusia Uongozi.  Anabainisha kuwa uongozi bora ni kipaji au karama na sayansi pia.  Unazaliwa na karama hizo lakini unajifunza pia.   Nia yaani commitment ni muhimu.  Kiongozi bora ni lazima awe mfano wa kuigwa katika utendaji kazi wake, uaminifu na uadilifu.

Anatilia mkazo swala la ongezeko la vijana na kwamba hakuna sera, ya namna ya kushughulikia ongezeko kubwa la watu.  Anagusia pia suala la siasa halaiki yaani Populism na athali zake.

Kuhusu siasa na demokrasia, anabainisha kuwa CCM bado kinajiona kama bado kipo kwennoye siasa za chama kimoja, Kunahitajika more political interaction na engagement.

Mheshimiwa anaendelea kuwa, uwepo wa vyama vingi vya siasa unadhoofisha demokrasia.  Watu wanaingia katika siasa kusaka manufaa ya kiuchumi sio kwa nia tukufu ya kuwatumikia watu na taifa.  Wafanya biashara wanasaka na kulinda maslahi, wasomi hutafuta kusafiri na posho, Wabunge wachache wanajali maslahi ya jimbo, wengi wanapenda safari za nje.  Hakuna interaction ya Wabunge kuhusu sera na utekelezaji wake.

Mwisho Mheshimiwa anajiuliza kama tutaweza kudumisha amani na umoja wetu kama Taifa.  Anagusia kuibuka hapa na pale viashiria vya ukabila, udini, na ukanda.

Mwisho kabisa Mheshimiwa Mkapa, anamalizia kwa kusema; Nitamuachia Mungu wangu na nyinyi kuamua ni tofauti gani nimeifanya humu duniani.

Jumanne, 5 Novemba 2019

MAKOSA YALIYOWAENGUA WAGOMBEA WA UPINZANI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

MAKOSA YALIYOWAENGUA WAGOMBEA WA UPINZANI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

1. Kama majina yake yatatofautiana kati ya majina aliyojaza kwenye fomu na majina aliyojiandikisha kwenye daftari. Angalia kanuni ya 13 (e) Uk. 152

2.  Endapo mdhamini hataandika majina matatu na cheo ktk vyama. Angalia muongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.2 (d) Uk. 10-11

3. Jina alilojaza wakati anachukua fomu lifanane na lililopo kwenye fomu ( dispatch book vs forms). Angalia kanuni ya 17 (1) Uk. 153

4. Mgombea arejeshe fomu mwenyewe na kusaini. Angalia kanuni ya 17 (2) Uk. 153

5. Majina ya mdhamini yafanane na ya mgombea yaliyojazwa kwenye fomu. Angalia muongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.2 (a-d) Uk. 10-11

6. Fomu ya kiapo iwe halisi iliyotolewa na msimamizi msaidizi na ishuhudiwe na msimamizi msaidizi ngazi husika. Angalia kanuni ya 16 (e) Uk. 152

7. Fomu zijazwe na mhusika lazima ziwe zimesainiwa. Angalia muongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.2 (e&f) Uk. 10-11

8. Fomu zishuhudiwe na ngazi ya chini ya chama itakayobainishwa na chama. Angalia muongozo wa uchaguzi kipengele cha 14.1 & 14.2 (a) Uk. 10-11

9. Ambaye hajajiandikisha hana sifa ya kuwa mgombea. Angalia kanuni ya 13 (e) Uk. 152, ilinganishe na Kanuni ya 16 (d) Uk. 152 na Kanuni ya 14 (a) Uk. 152

10. Aliyejiandikisha mara mbili atakuwa amepoteza sifa ya kugombea au kupiga kura. Angalia kanuni ya 14 (b)Uk. 152

11. Lazima aeleze shughuli halali inayomwingizia kipato na endapo atabainika kudanganya atakuwa amepoteza sifa. Angalia kanuni ya 15 (d)Uk. 152

12. Atakayeomba nafasi zaidi ya moja kwenye fomu moja atakuwa amepoteza sifa. Angalia kanuni ya 17 (1) & (5) Uk. 152-153

13. Nafasi anayoomba ionekane mpaka kwenye fomu ya kiapo. Angalia kanuni ya 17 (1)Uk. 153 isome sambamba na Kanuni ya 16 (e) Uk. 153

14. Fomu zijazwe kwa ukamilifu. Angalia kanuni ya 17 (2) Uk. 153

15. Eneo la uraia ajaze uraia siyo nchi mfano: Mtanzania na siyo Tanzania. Angalia kanuni ya 17 (1-5) Uk. 153-154

16. Usahihi wa maeneo kwa mujibu wa GN mfano Chankobe akiandika chakobe atakuwa amepoteza sifa maana eneo hilo litakuwa halipo ktk GN. Angalia kanuni ya 15 (e) Uk. 152 & Kanuni ya 17 (1-5) Uk. 153-154.

17. Muombaji aeleze anaomba nafasi ipi na wapi mfano nafasi anayoomba mwenyekiti wa Kijiji cha Kagera vinginevyo atakuwa amepoteza sifa. Angalia kanuni ya 15 (e) Uk. 152

18. Fomu ijazwe taarifa inayohitajika tu, kuwepo kwa maandishi au michoro isiyohitajika hilo ni kosa. Angalia kanuni ya 17 (5) Uk. 154

19. Mgombea arejeshe fomu zote mbili kinyume na hapo hana sifa. Angalia kanuni ya 17 (2), (3) na (4) Uk. 153-154

20. Kama mgombea ameomba nafasi mbili unaweza kumteua nafasi moja. Angalia kanuni ya 17 (1)& (5) Uk. 153-154

21. Mgombea akiwa na ajira, wadhifa au uteuzi wowote katika mihimili ya Serikali atakuwa amepoteza sifa za kuchaguliwa. Angalia kanuni ya 16 (f)Uk. 153

22. Ikiwa Mgombea alichukua fomu na hakurejesha atakuwa amepoteza sifa za kuchaguliwa. Angalia Kanuni ya 17 (2), (3) na  (4)

23. Mgombea ambaye hatadhaminiwa na ngazi ya chini ya Chama chake atakuwa amepoteza sifa za kuchaguliwa. Angalia muongozo wa uchaguzi sehemu  14.1 na 14.2 (a)

Kabla ya kulalamika kuenguliwa kwenye uchaguzi jiridhisheni kwa kila hatua kama mmekidhi wagombea walijaza fomu kwa usahihi na kuzingatia muongozo ili kukidhi vigezo na masharti sio kulalama tu....

Ijumaa, 25 Oktoba 2019

VISAWE VYA MANENO

VISAWE VYA MANENO

Garimoshi-treni
Pipi -peremende
Fedha-pesa
Kwea-panda
Gari-motokaa
Mende -kombamwiko
Beseni-karai
,jogoo-jimbi
,nyati-mbogo
,ndovu-tembo,
banati-msichana
,barobaro-mvulana
Kaa-keti
Dagaa-kauzu
Chooni-msalani
Bafuni -maliwatoni
Karo-ada
Konde-shamba
Tamati-mwisho
Luninga-televisheni

Ijumaa, 11 Oktoba 2019

MFAHAMU ELI COHEN....JASUSI NGULI KATIKA ULIMWENGU WA MAJASUSI

*MFAHAMU ELI COHEN....JASUSI NGULI KATIKA ULIMWENGU WA MAJASUSI*

Makala hii imeandaliwa na ***** kwa msaada wa Mitandao....

*Eli Cohen ni nani?*

Eliyahu Ben-Shaul Cohen (Eli Cohen) alizaliwa mjini Alexandria nchini Misri mwaka 1924 katika familia ya kiyahudi iliyokuwa ikiishi nchini humo. Katika ujana wake alishiriki katika mtandao wa siri ulikokuwa ukiwasafirisha wayahudi kutoka Misri kwenda Palestina iliyokuwa chini ya utawala wa kiingereza. Uhamiaji wa wayahudi ulikuwa ni maandalizi ya kuanzisha Taifa la Israel. Kazi hiyo aliendelea nayo hata baada ya kuzaliwa kwa Israel mwaka 1947. Ilipofika mwaka 1954 mamlaka za Misri zilifanikiwa kuharibu mtandao huo, huku Cohen na wenzake wakikamatwa na kuwekwa kizuizini. Hata hivyo hakukuwa na ushahidi wa kutosha kumfunga Cohen, na kwa hiyo aliachiwa huru.

Eli Cohen aliendelea kuishi nchini Misri hadi mwaka 1956, mara tu baada ya vita ya Suez kumalizika, akatimkia Israel. Huko alijiunga moja kwa moja na Intelijensia ya jeshi la Israel, Aman.
Kwa sababu ya ufasaha wake wa kuzungumza lugha za Kiarabu, Kiebrania na Kifaransa, alifanya kazi ya kutafsiri taarifa za siri hasa zilizohusu mataifa ya kiarabu.
Cohen hakuwa akibanwa sana na kazi za kiintelijensia kwa sababu alikuwa kama mtu wa kujitolea tu. Kutokana na historia yake ya kukamatwa nchini Misri alihisi kwamba hayupo makini na kazi hiyo. Ingawa ndani ya jumuiya ya kiintelijensia aliheshimiwa. Aliendelea kuishi maisha ya kawaida kama raia wengine, huku akipata na muda wa kutosha kwa familia, mke na watoto.

Haikuwa hivyo ilipofikia mei 1960 wakati mgogoro wa mpaka baina ya Israel na Syria ulipoanza. Israel ilihitaji Shushushu wa kuingia Damascus- Syria na kuvuna taarifa nyeti kutoka katika kitovu cha serikali ya Syria. Na jambo hilo lilikuwa la dharura.
Eli Cohen ndiye aliyekua mtu sahihi kwa kazi hiyo. Kikosi cha ushushushu namba 188 chini ya intelijensia ya jeshi kilipewa kazi hiyo. Kikosi hiki kilikuwa ni boresho la kikosi namba 131 cha awali.

Hatua ya kwanza ilikuwa kumtengeneza mtu tofauti ndani ya mwili wa Cohen, mtu ambaye ataishi mjini Damascus kama raia mzawa wa huko.
Kwahiyo, pamoja na udharura wa misheni hiyo, bado ilihitaji muda ili kuhakikisha kazi inafanyika kwa ufanisi wa kutosha.
Kumtengeneza mtu huyo, ilihitaji miezi sita na kwa kuanzia ilimpasa Cohen kuhudhuria mafunzo ya Quran nchini Israel ili awe mchangiaji mzuri katika mazungumzo yake na jamii ya waislamu atakaokutana nawo huko Syria.
Februari 1961, Cohen alisafiri hadi mjini Buenos Aires, Argentina kama mahala pa kuanzia (Base Country). Alitumia hati ya kusafiria ya nchi moja ya ulaya yenye jina tofauti alilotumia kwa muda nchini Argentina.
Enzi hizo Argentina ilikuwa chaguo la kuanzia kujenga historia ya uongo ya maisha ya mtu (cover story) anayetakiwa kufanya misheni katika nchi nyingine.
Miezi mitatu na nusu baadae, wakala kutoka kikosi cha 188 alitua nchini Argentina na kumkabidhi Cohen nyaraka zenye utambulisho mpya wa jina la Kamel Amin Taabeth, mfanyabiashara, raia wa Syria aliyezaliwa Lebanon.

Tangu hapo mtu anayeitwa Eliyahu Cohen, myahudi na mzaliwa wa Alexandria akapotea na kuibuka kama Kamel Amin Taabeth, mfanyabiashara mkubwa, raia wa Syria, mzaliwa wa Lebanon.

Tabeeth alikuwa na jukumu moja la kujichanganya na jamii ya watu wa Syria waliokuwa wakiishi nchini Argentina na kwengineko barani Amerika ya kusini. Misheni yake ilipaswa kuwa ya bajeti kubwa ili kumfanya kuwa mfanyabiashara tajiri, huku akikutana na Wasyria wenye ushawishi katika siasa za Syria na matajiri wakubwa wa Syria waliokuwa na biashara zao huko Amerika ya kusini.

Hadi kufikia mwanzo wa mwaka 1962, alikuwa amejiweka tayari kuingia katika nchi inayolengwa (Target Country) ya Syria.
Taabeth alisafiri kwa ndege kutoka Argentina mpaka Lebanon, kisha alitumia Taxi kuingia nchini Syria akiwa na mizigo mingi lakini mizigo muhimu ilikuwa miwili tu. Mmoja ni barua halisi ya kumtambulisha kwa mamlaka za Syria, iliyoandikwa na wafanyabiashara wa Syria wa huko Amerika ya kusini. Mzigo mwingine ni radio maalum ya mawasiliano kwa ajili ya kutuma taarifa nchini Israel.
Huko Damascus, Taabeth alikuwa mtu mpya lakini mpendwa na watu.
Kwa sababu ya utajiri wake aliweza kufanya tafrija nyingi huku akiwaalika maofisa wakubwa wa serikali ya Syria katika tafrija na shughuli zake mbalimbali. Wanasiasa na watu maarufu walifika nyumbani kwake na wakati mwingine aliwaandalia wasichana warembo kwa ajili ya kuwaburudisha wageni wake.
Kwa bahati tu, baada ya kitambo kidogo, mmoja kati ya marafiki zake wa mjini Buenos Aires, Major Amin Al-Hafez, alikuja kuwa Rais wa Syria.

Tabeeth alijijengea umaarufu mkubwa na ukaribu na maafisa wa vyombo vya dola. Alialikwa mara kwa mara katika maofisi ya dola na kambi za kijeshi. Hatimaye akawa mtu wa karibu na Rais Amin Al Hafez.
Kila alipotembelea vituo vya kijeshi, Tabeeth alichota taarifa na kuzituma nchini Israel kwa mawasiliano ya siri ya kutumia radio maalum. Alipata ramani ya vituo vya jeshi la Syria vilivyo katika miinuko ya Golan, mpakani mwa Israel (wakati huo), alituma taarifa kuhusu aina na idadi ya silaha kubwa, majina ya marubani wa ndege za kivita na maofisa wakubwa wa jeshi, historia zao, maisha yao na tabia zao, mipango na mbinu za kivita za Syria, pamoja na maeneo ya udhaifu wa Israel ambayo Syria ilikuwa ikiyajua.

Maurice Cohen, mdogo wake Eli Cohen/Taabeth ndiye aliyekuwa akipokea na kutafsiri taarifa hizo kutoka kwa mdogo wake aliyekuwa akifanya kazi ya kujiandaa kufa huko Damascus.
Kabla ya hapo, ndugu hawa hawakufahamu kuwa wote ni watumishi wa intelijensia ya Israel. Eliyahu alimwambia mdogo wake anasafiri kwenda nje ya nchi kununua kompyuta kwa ajili ya wizara ya ulinzi. Hata wakati wa mawasiliano ya kutoa taarifa kutoka Syria kwenda Israel hawakuwa wakifahamu kuwa ni ndugu kwakuwa walitumia majina maalum ya siri (Code names)

Kifo cha Cohen.
Novemba 1964 Cohen alirudi kwa siri nchini Israel kusabahi familia yake. Kisha aliamua kukutana na viongozi wa intelijensia wa Israel na kuwaeleza kuwa anahisi hatari. Kiongozi wa intelijensia ya kijeshi wa Syria, Kanali Ahmed Suedani alikuwa anamuhisi Cohen.
Cohen alitanabaisha kuwa anataka kurudi nyumbani baada ya kazi ya karibu miaka minne ya kwenye "baridi kali". Alihisi kifo kinamkaribia. Akiwa Israel ndipo yeye na mdogo wake Maurice walipogundua kuwa walikuwa wakibadilishana taarifa kutoka Syria kwenda Israel. Lakini hakukuwa na tija ya kujadili zaidi jambo hilo.
Kwa bahati mbaya, aliyekuwa na jukumu la kuratibu shughuli za Cohen (Case handler) huko Israel hakutilia maanani kauli za Cohen. Wakati huo, mgogoro wa mpaka ulikuwa umeibuka upya, na vita ilikuwa inakaribia. Jeshi la Israel lilihitaji mtu wa kuchota taarifa kutoka Damascus wakati huo kuliko wakati wowote. Hakukuwa na mtu mwingine zaidi ya Cohen, na kwa hiyo Cohen alitakiwa kurudi katika kituo chake cha kazi mara moja.

Pengine ni kwa sababu ya kuchoshwa na kazi hiyo ya siri, au kwa sababu zingine Cohen alisahau kanuni ya busara. (Rule of prudence) na hivyo akawa anatuma taarifa bila ratiba maalum. Kwa muda wa wiki 5 alifanya mawasiliano mara 31. Na kwa sababu ya unyeti wa taarifa hizo, Wapokezi wa taarifa huko Israel, akiwemo Maurice aliyekuwa anatafsiri taarifa hizo, walijisahaulisha na kushindwa kumuonya.
Majasusi wa Sovieti (Urusi ya leo) walinasa mawasiliano hayo na wakati huo Syria ilikuwa rafiki wa Soviet. Baadae majasusi hao wa Soviet walimpa taarifa kiongozi wa intelijensia ya jeshi la Syria, Kanali Ahmed Suedani na kumsaidia kunyaka mawasiliano ya Cohen/Taabeth aliyokuwa akifanya na Israel. Januari 18, 1965 vijana wa Kanali Suedani walivamia ndani ya nyumba ya Cohen/Taabeth na kumkuta akifanya mawasiliano na Israel. Akadakwa.
Kulikuwa na hali ya mshtuko mjini Tel Aviv, Isael. 'Mtu' wa nchi ingine aliyekuwa Syria alitoa taarifa ya kukamatwa kwa Eli Cohen siku moja baadae.
Serikali ya Israel ilianza mara moja mipango ya kumkomboa Cohen kutoka Syria, au hata ikibidi kumuepusha na kifo.
Mwanasheria mahiri wa Kifaransa alikodishwa na kuomba msaada wa kidiplomasia kutoka jumuia ya ulaya na kutoka kwa Papa Paulo IV huko Vatican. Pia serikali za Canada, Ubelgiji na Ufaransa, kwa kuombwa na Israel ziliishawishi Syria kuachana na adhabu ya kifo kwa Cohen.
Hata hivyo, mnamo tarehe 18 Mei 1965, Cohen alinyongwa hadharani katika eneo la mraba wa Marjeh, mjini Damascus.
Kabla ya kunyongwa Cohen alimuandikia mkewe Nadia ujumbe mfupi akisema "Nakuomba usiomboleze ee Nadia kwa mambo yaliyopita. Jitazame mwenyewe na kuitafuta kesho mpya". Pia kabla ya kunyongwa, Cohen aliomba kukutana na kiongozi wa kidini wa huko Syria, "Rabbi" Nissim Andabo ambaye aliruhusiwa kuongozana naye alipokuwa akipelekwa kunyongwa.

Tangu wakati huo, Nadia amekuwa akiomba mwili wa mumewe urudishwe nchini Syria kwa ajili ya maziko, kaka yake Eli Cohen, Maurice kabla ya kufariki kwake mwaka 2006, aliwahi kufanya kampeni kadhaa za kutaka kurudishwa mwili wa kaka yake, akisaidiwa na serikali ya Israel bila mafanikio.

Septemba 20, 2016 video ya kunyongwa kwa Cohen ilirushwa katika mtandao wa facebook, haikuwa ikijulikana kama video hiyo ipo. Mamlaka za Israel zilithibisha kuwa Video hiyo si ya kutengenezwa bali ni halisi.
Julai 5, 2018, Shirika la ujasusi la Israel, Mossad wametangaza kuipata saa ya mkononi ya Eli Cohen iliyotangazwa kuuzwa huko Syria. Nadia, mke wa Cohen mwenye miaka 82 bado anaomboleza hadi leo, anaamini siku moja mifupa ya mume wake itarudishwa kuzikwa Israel.
Katika sherehe za kuonesha Saa hiyo, alikuwapo kiongozi wa Mossad wa sasa, Yosi Cohen.
Saa hiyo itahifadhiwa katika makao makuu ya Shirika la Mossad, Tel Aviv, Israel.

Picha zipo ukurasa wa twitter wa @jashyie

Jumatano, 2 Oktoba 2019

DARASA* *HURU

**

Itifaki - ni mpangilio au utaratibu wa mambo uliowekwa na Watu au taasisi fulani.
Itifaki ya Chama cha Mapinduzi - ni mpangilio au utaratibu wa kuendesha , kupanga au kupangilia mambo ya Ccm au shughuli mbalimbali za Chama.
Pia Itifaki ndani ya Ccm ni sehemu ya kanuni zilizokubalika na kutumika katika Chama mara baada kupitishwa na Halmashauri kuu ya Taifa.
Chama cha Mapinduzi kinaongozwa na Katiba , kanuni, Miongozo , Taratibu na Maelekezo toka ( Waraka nk ) kutoka Makao Makuu.
Itifaki nyingi hazipo katika Katiba , hazipo katika Kanuni wala hazipo katika Miongozo,  isipokuwa zipo katika taratibu na Waraka mbalimbali za Chama.
Mfano: Itifaki ya Ukaaji katika Mikutano ya Chama, huwezi kuona katika Katiba, huwezi kuona katika Kanuni lakini Chama kina Itifaki ya ukaaji , yaani nani akae wapi na kwa nafasi gani , au Itifaki ya Utambulisho katika Chama nani aanze na nani wa mwisho kutambulishwa katika watu waliohudhuria eneo hilo.
Itifaki nyingi za Chama hazifahamiki na Wanachama na Viongozi kwa kuwa Wanachama au Viongozi wengi hutegemea kupata mambo mengi Katika Katiba na Kanuni tu, wanasahau kuwa kuna Taratibu, miongozo na Waraka mbalimbali zinazoendesha Chama cha Mapinduzi.
Leo nitazungumzia *Itifaki* *ya* *Mikutano* *tu*
Itifaki ya ukaaji katika Mikutano ya Chama cha Mapinduzi imegawanyika katika sehemu kuu zifuatazo :-
*1* *.* *JUKWAA*
*2* *.* *HADHIRA*

Tuanze na *JUKWAA*
Eneo hili ni sehemu ya mbele ambayo Viongozi wa Mkutano pamoja na wageni (Rasmi) hukaa. Sehemu katika Chama imezoeleka kuitwa meza kuu. Sehemu hii Viongozi hukaa kutokana na nafasi (vyeo ) walivyonavyo katika kupata mpangilio wa ukaaji meza kuu.
Utaratibu wa ukaaji meza kuu ni kwamba Mwenyekiti wa Kikao hukaa kiti cha Katikati mwa Meza Kuu, Katibu wa Kikao atakaa mkono wa Kushoto wa Mwenyekiti , Katibu Mwenezi ( kama kikao ni cha Chama au Mhamasishaji kama kikao cha Vijana au Katibu Malezi kama kikao ni cha Wazazi ) atakaa pembeni ya Katibu ( kushoto ) , Wajumbe wengine wa Kamati ya siasa au Kamati ya Utekelezaji watakaa pembeni kulia na kushoto kwa ku-balance meza isizidi sana upande mmoja.
Ukaaji huu ni kwa vikao visivyo Kamati za Siasa na Kamati za Utekelezaji.
*Endapo* *kikao* *hiki* *kitakuwa* *na* *Mgeni* *rasmi* *na* *Msafara* *wake* Mgeni rasmi atakaa kiti cha  katikati mwa meza kuu , mkono wa kushoto wa Mgeni rasmi atakaa Mwenyekiti wa Kikao husika , mkono wa kushoto wa Mwenyekiti wa Kikao watakaa wenyeji yaani Katibu nk. Mkono wa kulia wa Mgeni rasmi watakaa aliofutana nao kwa kuzingatia vyeo vyao.
Ikumbukwe idadi ya viti vya meza kuu mstari wa kwanza visizidi kumi na moja, kama wageni na Viongozi wenyeji watakuwa wamezidi watakaa mstari unaofuata, kama hakuna nafasi ya kupanga mstari mwingine vitapangwa viti eneo la mbele mbele karibu na meza kuu kwa kufuata utaratibu wa kushoto Wenyeji na kulia wageni.
*2* *.* *HADHIRA*
Eneo hili ni sehemu wanayokaa wajumbe mbalimbali wa kikao / mkutano ambao watakaa kwa kuangalia meza kuu.
Eneo hili itifaki inatutaka kukaa kwa kuzingatia uwakilishi wa maeneo tunayotoka, mfano wajumbe watakaa Kimkoa , kiwilaya, kikata, kimatawi au kimashina.
*UINGIAJI*
Itifaki ya uingiaji katika Vikao/ Mikutano wanatangulia Wajumbe kabla ya Mwenyekiti / Mgeni Rasmi
*NYIMBO* *ZA* *KUINGILIA*
Sio kila nyimbo ya Chama inatumika kuingiza Viongozi katika Vikao, kwa vikao vya Chama nyimbo inayotumika kuwaingiza Viongozi ni *"* *Chama* *chetu* *cha* *Mapinduzi* *chajenga* *Nchi* *”*
Umoja wa Vijana nyimbo ya kuingiza Viongozi katika  Vikao ni " *Eee* *Vijanaa* , *Vijana* , *Vijana* *tayarii* , *kulitumikia* *Taifa* , *Taifa* *Tanzania* ”
Asanteni sana , naomba niishie hapo tutaendelea kujuzana mengine.

Jumatano, 11 Septemba 2019

MAJUKUMU YA AFISA MTENDAJI

YALIYOMO-----------------------
1. Majukumu ya afisa mtendaji wa kijiji
2. Majukumu ya afisa mtendaji wa kata
3. Majukumu ya afisa tarafa
4. Majukumu ya diwani
5. Majukumu ya meya/mwenyekiti wa halmashauri
6. Majukumu ya mwenyekiti wa kijiji
7. Majukumu ya mwenyekiti wa mtaa
8. Majukumu ya mwenyekiti wa kitongoji
9. Majukumu ya katibu tawala wa wilaya
10. Majukumu ya mkuu wa wilaya
11. Majukumu ya katibu tawala wa mkoa
12. Majukumu ya mkuu wa mkoa
------------------------------
I. MAJUKUMU YA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI
(i) Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na Kamati zake katika Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.
(ii) Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia mapato na matumizi ya Serikali ya kijiji
(iii)Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
(iv) Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya kijiji
(v) Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Kijiji.
(vi) Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Kijiji.
(vii) Ataratibu na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuziwasilisha kwenye Halimashauri ya Kijiji na baadae kwenye kata.
(viii) Ataongoza vikao vya maendeleo ya Kijiji vitavyowahusisha wananchi na wataalamu waliopo kwenye eneo lake.
(ix) Atahamasisha wananchi katika kampeni za kuondoa njaa, umasikini, na kuongeza uzalishaji mali.
(x) Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.
(xi) Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika Kijiji.
(xii) Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, wataalamu mbalimbali na NGO waliopo katika kijiji.
II. MAJUKUMU YA AFISA MTENDAJI WA KATA
(i) Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika kata na atashughulikia masuala yote ya kata
(ii) Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbali ya uzalishaji, mali, kuondoa njaa na Umasikini.
(iii)Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
(iv) Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na vitongoji.
(v) Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibuna kusimamia shughuli za Uchaguzi katika Kata.
(vi) Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo lake.
(vii) Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katika ngazi ya Kata.
(viii) Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na nakala kwa Katibu Tarafa.
(ix) Atakuwa mwenyekiti katika vikao vya vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa vjiji, na NGO’S katika kata yake.
(x) Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji, vitongoji, na kata yake.
III. MAJUKUMU YA AFISA TARAFA
(a) Majukumu ya Afisa Tarafa Kwenye Mamlaka ya Serikali Kuu
(i) Kumwakilisha na kumsaidia Mkuu wa Wilaya katika utekelezaji wa shughuli za Serikali Kuu katika Tarafa.
(ii) Kuandaa na kuratibu taarifa na ripoti zinazohusu masuala ya ulinzi na usalama ya kata kwenye tarafa yake na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
(iii) Kuhamasisha na kuhimiza wananchi iliwashiriki kwenye shughuli za maendeleo kwenye Tarafa.
(iv) Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Wananchi Katika Tarafa.
(v) Kuwa mlinzi wa amani katika eneo lake.
(vi) Kufuatilia na kuhimiza utekelezaji wa sera za Serikali katika eneo lake na kuhakikisha kuwa zinatekelezwa ipasavyo.
(vii) Kuratibu shughuli zote za maafa na dharura mbalimbali katika eneo lake
(viii) Kuandaa taarifa zote zinazohusu masuala ya Serikali Kuu kuhusu utendaji wa kazi za maafisa Watendaji wa kata wa eneo lake na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
(ix) Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa. katika eneo lake.
(x) Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Katibu Tawala wa Wilaya.
(b) Majukumu ya Afisa Tarafa Kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa;
(i) Kuwasaidia Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa katika shughuli za Maendeleo katika eneo lake
(ii) Kusimamia utendaji wa shughuli za Maafisa Watendaji wa Vijiji, Kata na Mitaa.
(iii)Kushiriki na kutoa ushauri katika upangaji wa mipango ya Maendeleo katika eneo lake
(iv) Kuhudhuria vikao vya kamati za Halmashauri na Baraza la madiwani na kutoa ushauri.
(v) Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake kama zitakavyopokelewa kutoka kwa Watendaji wa Kata.
(vi) Kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa au Jiji.
IV. MAJUKUMU NA KAZI ZA DIWANI
(i) Kuwakilisha wananchi katika Halmashauri. Diwani huwakilisha wakazi wote wa Kata yake hivyo anatakiwa kuwa karibu na wapiga kura wake na kufikisha mbele ya Halmashauri na Kamati zake vipaumbele vya wananchi ili vijadiliwe na kutolewa maamuzi.
(ii) Kuhamasisha wananchi katika kulipa kodi na ushuru wa Halmashauri.
(iii) Kusimamia matumizi ya Fedha za Halmashauri. Diwani anatakiwa kuhakikisha Fedha za Halmashauri zinatumiwa kwa madhumuni yaliyokusudiwa na sio vinginevyo.
(iv) Kuwa kiungo kati ya Halmashauri na ngazi za msingi za Serikali za Mitaa. Diwani ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata. Atumie mamlaka hayo kuwasilisha kwenye Halmashauri maamuzi ya Kata yake na vile vile kuwasilisha kwenye Kata maamuzi ya Halmashauri.
(v) Kuhamasisha wananchi kuhusu vita dhidi ya umaskini. Katika kulitekeleza hili ni lazima ajue kwa ufasaha hali ya kiuchumi na kijamii inayowakabili wananchi wake na kushirikiana nao ili kupanga mipango endelevu ya kujikwamua.
(vi) Kufuatilia utekelezaji wa mipango yote ya wananchi na ya Halmashauri. Ili kutimiza jukumu hili ipasavyo, Diwani anatakiwa kufuatilia utekelezaji wa miradi yote ndani ya Kata yake ambalo ni jimbo lake la uchaguzi bila kudai malipo yoyote toka kwenye Halmashauri au wadau wengine. Kimsingi hii ndiyo kazi ambayo Diwani aliahidi kuitekeleza wakati wa kampeni.
(vii) Kutetea Maamuzi ya Halmashauri. Wakati wa majadiliano ndani ya Halmashauri, Diwani ataelekeza na kutetea maoni yake au ya wakazi wa eneo lake. Hata hivyo, iwapo uamuzi utakaofikiwa na wengi utakuwa kinyume na matarajio yake atalazimika kuunga mkono maamuzi ya wengi yaliyofikiwa kidemokrasia.
(viii) Kuzingatia misingi yote ya Utawala Bora wakati wa kutekeleza majukumu yote ya Udiwani.
V. MAJUKUMU NA KAZI ZA MEYA/MWENYEKITI WA HALMASHAURI
(i) Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri ni Kiongozi Mkuu wa Halmashauri mwenye dhamana ya kisiasa. Dhamana hii humfanya kuwa kioo ndani na nje ya Halmashaui yake.
(ii) Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri ni Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani na Kamati ya Kudumu ya Fedha na Mipango/Utawala.
(iii) Kwa mujibu wa Kifungu Na. 193 (2) cha Sheria Na. 7 ya 1982 na Kifungu Na. 108 (2) cha Sheria Na. 8 ya 1982, Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri ni mtia lakiri/mhuri katika nyaraka zote rasmi za Halmashauri.
(iv) Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri analo jukumu maalum la kudhibiti na kuongoza mikutano ya Baraza la Madiwani ili liweze kufanya maamuzi yenye maslahi kwa wananchi wote wa Halmashauri. Katika kutimiza jukumu hili Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri anatakiwa kutenda haki kwa Madiwani wote bila kujali itikadi za Kisiasa, Jinsia, Dini, Rangi au Kabila na wakati wote awe mtulivu, imara na asiyeonyesha udhaifu wakati wa kuendesha vikao.
(v) Ili kutimiza wajibu wake wa Uongozi ipasavyo, Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri anatakiwa kupewa Ofisi na Halmashauri ambayo ataitumia kukutana na wananchi wote wenye shida, kero na maoni ya kuboresha utendaji wa Halmashauri mara mbili kwa wiki. Ratiba ya siku hizi mbili lazima iwe wazi na ifahamike kwa wananchi wote. Aidha, Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri kama atataka kutembelea Halmashauri yake katika harakati za kuhimiza maendeleo, atalazimika kufanya kazi hiyo katika siku hizo mbili tu zilizoruhusiwa na sio vinginevyo.
VI. MAJUKUMU NA KAZI ZA MWENYEKITI WA KIJIJI
(i) Atakuwa ndiye Mkuu wa Serikali ya Kijiji;
(ii) Atakuwa na wajibu wa kuitisha na kuongoza mikutano yote ya Halmashauri ya kijiji, pamoja na Mikutano Mikuu ya Kijiji. Lakini endapo Mwenyekiti hayupo katika mkutano wowote, wajumbe wa mkutano unaohusika wanaweza kuchagua Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo;
(iii)Atakuwa mwakilishi wa kijiji kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata;
(iv) Atawahudumia kwa usawa wanakijiji wote, bila kujali tofauti za Kisiasa, Kijinsia au za Kidini;
(v) Atakuwa mfano wa uongozi bora na utendaji bora wa kazi, kwa kuwa na shughuli zake mwenyewe za kujitegemea, ambazo zaweza kuigwa na wanakijiji wenzake.
VII. MAJUKUMU NA KAZI ZA MWENYEKITI WA MTAA
(i) Kuwa Mwenyekiti wa Mikutano yote ya Kamati ya Mtaa na Mkutano wa Mtaa;
(ii) Kusuluhisha migogoro midogomidogo ambayo haistahili kuitisha mkutano wa Kamati ya Mtaa au kupelekwa kwenye Baraza la Kata au Mahakama;
(iii)Kuwa msemaji wa Mtaa;
(iv) Kuwaongoza na kuwahimiza Wakazi wa Mtaa washiriki shughuli za maendeleo, sherehe za Taifa, Mikutano ya hadhara itakayoandaliwa na Mtaa, Halmashauri ya Mji Manispaa au Jiji na Serikali;
(v) Kuwakilisha Mtaa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata;
(vi) Kutekeleza kazi atakazopewa na Kamati ya Mtaa na Mkutano wa Mtaa na Kamati ya Maendeleo ya Kata;
(vii) Kusimamia utekelezaji wa kazi na Majukumu ya Kamati ya Mtaa;
(viii) Kusimamia utunzaji wa rejesta ya wakazi wote wa Mtaa.
VIII. MAJUKUMU NA KAZI ZA MWENYEKITI WA KITONGOJI
(i) Kutunza rejista ya wakazi wa kitongoji na nyaraka nyingine muhimu zinazohusu maendeleo ya kitongoji kwa jumla ikiwa ni pamoja na kumbukumbu za vizazi na vifo;
(ii) Kusimamia shughuli za ulinzi na usalama wa watu na mali zao waishio katika eneo lote la kitongoji;
(iii)Kuhamasisha ulipaji wa kodi na ushuru mbalimbali, kama utakavyoamuliwa na kuwekwa mara kwa mara na Halmashauri ya Kijiji, Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji;
(iv) Kusimamia katika eneo lake suala zima la Hifadhi ya mazingira hususan vyanzo vya maji n.k.;
(v) Kusimamia suala la afya katika eneo lake ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa kampeni za afya za Kitaifa, Kimkoa au Kiwilaya dhidi ya magonjwa ya kuambukiza, na hasa, Vita dhidi ya UKIMWI;
(vi) Kusimamia utekelezaji wa kanuni za kilimo na ufugaji bora ili kuinua hali ya lishe na uchumi wa wakazi wa kitongoji;
(vii) Kufuatilia na kuhakikisha kuwa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anapatiwa nafasi na kushirikiana na viongozi wa shule katika udhbiti utoro shuleni;
(viii) Kuhamasisha elimu ya watu wazima;
(ix) Kusimamia na kuwahamasisha wakazi wa kitongoji katika kutekeleza shughuli za kujitegemea;
(x) Kusuluhisha migogoro midogo midogo isiyostahili kushughulikiwa na Mabaraza ya Kata au Mahakama;
(xi) Kuwakilisha kitongoji katika Serikali ya Kijiji;
(xii) Kuwaongoza na kuwahamasisha wakazi wa kitongoji washiriki katika sherehe za Taifa na mikutano ya hadhara itakayoandaliwa na kuitwa na Serikali au Halmashauri;
(xiii) Kutekeleza kazi nyingine atakazopangiwa na Halmashauri ya Kijiji, Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji.
IX. MAJUKUMU YA KATIBU TAWALA WA WILAYA
(i) Kumshauri Mkuu wa Wilaya katika masuala yanayohusu ulinzi na usalama
(ii) Kumshauri Mkuu wa Wilaya katika masuala yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya sherehe na dhifa za kitaifa
(iii) Kumshauri Mkuu wa Wilaya katika masuala yanayohusu malalamiko ya wananchi
(iv) Kumshauri Mkuu wa Wilaya katika masuala yanayohusu uwekaji wa mazingira bora ya kuziwezesha Halmashauri za Wilaya kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sera za serikali.
(v) Kuwa Kiongozi Mkuu wa Utawala katika ngazi ya Wilaya.
(vi) Kuwa Msajili wa Vizazi na Vifo.
(vii) Kuwa msajili wa ndoa.
(viii) Kuandaa makadirio ya matumizi ya Wilaya.
(ix) Ushughulikia masuala ya itifaki Wilayani
(x) Kuratibu harakati za kupambanana dharura za maafa Wilayani.
(xi) Kutekeleza majukumumengine kama atakavyoagizwa na Mkuu wa Wilaya na Katibu Tawala wa Mkoa.
X. MAJUKUMU YA MKUU WA WILAYA
(i) Kumweka mtu kizuizini kwa muda wa saa 48 mfululizo iwapo atashukiwa kuwa ni mhalifu au anayehatarisha hali ya utulivu na Amani (Sheria ya tawala za mikoa Na 19/1997)
(ii) Kufungisha ndoa za serikali (Law of Marriage Act No 5/1971)
(iii) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwa mwenyekiti wa Kamati yaMkoa inayochambua maombi ya watu wanaotaka kuuza madawa ya sumu (Pharmaceuticals and Poisons Act No 9/1978)
(iv) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuongoza Kamati ya kusikiliza rufani za leseni za biashara mkoani (Business Licensing Authority Act No 25/1972, ib. 1)
(v) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya leseni za vileo (Intoxicating Liquours Act No 28/1968)
(vi) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuteua wakaguzi wa magereza (Prisons Act No 34/1967, ib. 100)
(vii) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwashughulikia watu wanaodhaniwa kuwa ni wachawi (Witchcraft Ordinance Cap 18)
(viii) Kuwa mhimili msaidizi wa Halmashauri za Wilaya (Sheria Na 7/1982).
(ix) Kuwa mwenyekiti wa Kamati mbalimbali zitakazoundwa Wilayani.
(x) Kuhudhuria vikao vya Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kamamjumbe
(xi) Kushughulikia malalamiko ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi
(xii) Kumsaidia Mkuu wa Mkoa katika kuzisimamia Halmashauri za Wilaya na kuhakikisha kuwa zinatoa huduma nzuri kwa wananchi na kwa ufanisi
(xiii) Kuziwekea Halmashauri za Wilaya mazingira mazuri na kuhakikisha kuwa zinatekeleza majukumu yake kulingana na sera za serikali.
(xiv) Kutekeleza majukumu yote atakayopewa kisheria au kukasimiwa na Mkuu waMkoa.
XI. MAJUKUMU YA KATIBU TAWALA WA MKOA
(i) Kuratibu shughuli zote za utawala kwenye sekretariati ya mkoa
(ii) Kuwa mshauri mkuu wa mkuu wa mkoa katika masuala ya sharia,kanuni na taratibu za uendeshaji wa shughuli za serikali za mitaa.
(iii) Kuwa katibu wa Kamati ya ushauri ya mkoa (RCC)
(iv) Kuwa mkuu wa watumishi waserikali kuu katika mkoa
(v) Kushauri na kuratibu upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya serikali za mitaa
(vi) Kuwajibika kwa fedha zote zitakazopelekwa mkoani kwa ajili ya matumizi ya kawaida na mipango ya sekretariati ya mkoa na ofisi za wakuu wa wilaya
(vii) Kuwa afisa mhasibu wa fedha za serikali kuu mkoani
(viii) Kuwa mwenyekiti wa bodi za zabuni ya mkoa
(ix) Kuwa mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Utumishi serikalini (KAMUS)
(x) Kuwa mwenyekiti wa kamati ndogo ya wataalamu katika sekretariati ya mkoa na kamati nyingine zitakazotokea kwa dharura
(xi) Kupokea na kuchambua takwimu na taarifa za utekelezaji zinazotoka kwenye halmashauri na mashirika mbalimbali
(xii) Kufuatilia upatikanaji na usambazaji wa pembejeo na zana muhimu za kazi ikiwa ni pamoja na mahitaji mengine kama vile wataalamu na fedha
XII. MAJUKUMU YA MKUU WA MKOA
(i) Kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoa aliokabidhiwa (Katiba 1977, ib. 61(4))
(ii) Kuwa mwenyekiti wa RCC inayotoa ushauri kuhusu masuala mbalimbali mkoani mwake (RAA No 19/1997).
(iii) Mhimili wa Halmashauri za wilaya (LG Finance Act No 9/1982)
(iv) Mhimili msaidizi wa Halmashauri za Miji iliyoko katika mkoa wake (LG (Urban Authorities) Act No 8/1982)
(v) Kumwekakizuizini kwa saa 48 mfululizo mtu anayehisiwa kuwa ni mhalifu au anayehatarisha hali ya utulivu naamani (Regional Admin Act No 19/1977)
(vi) Kuongoza Kamati ya Mkoa ya maombi ya leseni za magari (Motor Vehicles, Registrations, Acquisitions and Dispositions Act No 5/1972, ib 24(2))
(vii) Kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa inayoshughulikia uteuzi wa vijana wanaojiunga na jeshi la kujenga taifa (National Service Act No 16/1964)
(viii) Kuwa mwenyekiti wa Kamati yaMkoa inayochambua maombi ya watu wanaotaka kuuza madawa ya sumu (Pharmaceuticals and Poisons Act No 9/1978)
(ix) Kuongoza Kamati ya kusikiliza rufani za leseni za biashara mkoani (Business Licensing Authority Act No 25/1972, ib. 1)
(x) Kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya leseni za vileo (Intoxicating Liquours Act No 28/1968)
(xi) Kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa ya utoaji wa leseni za magari na uchukuzi (Transport Licensing Act No 1/1973)
(xii) Kuteua wakaguzi wa magereza (Prisons Act No 34/1967, ib. 100)
(xiii) Kuwa mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoani kwake ili kuhakikisha kuwa kuna ulinzi na usalama mkoani wakati wote na kuishauri serikali ipasavyo (National Defence Act No 24 1966)
(xiv) Kuwashughulikia watu wanaodhaniwa kuwa ni wachawi (Witchcraft Ordinance Cap 18)

Alhamisi, 22 Agosti 2019

MASWALI YA SAYANSI

Mwili wa binadamu una mifupa mingapi na misuli mingapi?

Mwili wa binadamu una mifupa mingapi na misuli mingapi?

Mifupa 206
Misuli 600

Msaada
    Kuna jumla ya sayari ngapi ktk mfumo wa jua?

Nane(8)

Jumapili, 18 Agosti 2019

NYIMBO ZA UZALENDO TANZANIA

TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuota wewe, niamkapo ni heri mama wee
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote.

Tanzania Tanzania , ninapokwenda safarini
Kutazama maajabu, biashara nayo makazi
Sitaweza kusahau mimi mambo mema ya kwetu kabisa
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote

Tanzania Tanzania karibu wasio kwao
Kwenye shida na taabu kukimbizwa na walowezi
Tanzania yawakaribisha tuungane kiume chema wee
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote

Tanzania Tanzania watu wako ni mema sana
Nchi nyingi zakuota nuru yako hakuna tena
Na wageni wakukimbilia ngome yako imara kweli wee
Tanzania Tanzania mola awe nawe daima

TAZAMA RAMANI
Tazama ramani utaona nchi nzuri
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzaniaaaaaaaaaa….
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere
ameukomesha X2

Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,
Kila mara niwe kwako nikiburudika,
Nakupenda sana hata nikakusitiri,
Nitalalamika kukuacha Tanzania.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere
ameukomesha X2

Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde name nikulinde hata kufa.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere
ameukomesha X2

Alhamisi, 15 Agosti 2019

UJUE UMBALI WA KWENDA KWENU

UJUE UMBALI WA KWENDA KWENU

1. DAR - ARUSHA *646* KM
2. DAR - KAHAMA *1012* KM
3. DAR - BABATI via moro *876* KM
4. DAR - BARIADI *1127* KM
5. DAR - BUKOBA via kahama *1433* KM
6. DAR - DODOMA *450* KM
7. DAR - GEITA *1226* KM
8. DAR - IRINGA *501* KM
9. DAR - KIBAHA *35* KM
10. DAR - KIGOMA via itigi *1258* KM
11. DAR - KIGOMA via kahama *1476* KM
12. DAR - LINDI *452* KM
13. DAR - MBEYA *822* KM
14. DAR - MOROGORO *194* KM
15. DAR - USANGI *575*KM
15. DAR - MOSHI *530* KM
16. DAR - MPANDA via itigi *1383* KM
17. DAR - MTWARA *556* KM
18. DAR - MUSOMA *1370* KM
19. DAR - MWANZA *1200* KM
20. DAR - NJOMBE *710* KM
21. DAR - SHINYANGA *989* KM
22. DAR - SINGINDA *725* KM
23. DAR - SONGEA via moro *949* KM
24. DAR - SONGEA via lindi *1054* KM
25. DAR - SUMBAWANGA *1166* KM
26. DAR - TABORA *829* KM
27. DAR - TANGA *350* KM
28. DAR - TUNDUMA *937* KM
29. ARUSHA - DODOMA via kondoa *425* KM
30. ARUSHA -KIGOMA *1054*KM
31. DAR - KIBITI *128* KM
32. ARUSHA - MWANZA *787* KM
32. MORO - TANGA *329* KM
33. NGARA - DAR via kahama *1310* KM

Share kwa marafiki na tujulishe umbali wa mikoa tofauti unayoifahamu hapa nchini ili tupate kutambua.

Jumatano, 14 Agosti 2019

Compilation of words which lawyers use (which makes them a class apart):

Compilation of words which lawyers use (which makes them a class apart):

1. Lawyers don't "correct" pleadings; They amend them.

2. Lawyers don't merely "think". They opine.

3. Lawyers don't "outline" remedies or issues; They adumbrate them.

4. Lawyers don't "suggest" to court; They submit.

5. Lawyers don't "lie"; They misguide the audience

6. Lawyers don't "support" with evidence; they corroborate it.

7. Lawyers don't "show" in court; They demonstrate.

8. Lawyers don't "say" anything; They aver.

9. Lawyers don't "disagree with a fact"; They contend it.

10. Lawyers don't "finish submitting"; They rest their case.

11. Lawyers don't use the word "understand"; They use "construe".

12. Lawyers don't "agree with other people's opinions" ; They concur with them.

13. Lawyers don't "investigate"; They probe.

14. Lawyers don't "disagree with other people's opinions"; They dissent from them.

15. Lawyers don't "ask for permission"; They seek leave.

16. Lawyers don't "fall sick"; They get indisposed.

17. Lawyers don't "ask court"; They pray.

18. Lawyers don't "increase" anything they "augment" it

19. Lawyers don't ask court to  "postpone cases"; They ask it to adjourn them.

20. Lawyers don't "find solutions"; They seek remedies.

21. Lawyers "know" everything; what you think they don't know is "what they have not addressed their minds to".

22. Lawyers don't "go on" ; They proceed.

23. Lawyers don't "refuse"; They object.

24. Lawyers don't "ask court to take a step"; They move it.

25. Lawyers don't "leave an issue"; They abandon it.

26. Lawyers are not "wordy"; They articulate their point.

27. Lawyers don't "find solutions"; They resolve issues.

28. Lawyers call themselves lawyers among "lay men"(all other professions and non professionals); They call themselves "Learned Friends" when they are addressing themselves.

29. Lawyers don't "disagree" with each other; They just differ.

30. Lawyers don't "seek help" from court; They seek redress.

31. Lawyers don't "speak" in court; They address court.

32. Lawyers don't "agree" to what someone has said; They associate themselves with it.

33. Lawyers don't say something is "irrelevant or useless"; They say it is immaterial.

34. Lawyers don't "arrive" in court; They enter appearance.

35. Lawyers don't "go" to a judge; They appear before him or her.

36. Lawyers don't "die" ; They relocate to God's domicile !

37. Lawyers don't get "late"; They delay.

38. Lawyers don't "disagree" with somebody's opinion; They dissociate themselves from it.

39. Lawyers don't "stand in for" anyone; They hold brief for them.

40. Lawyers don't ask court to "force";They ask it to compel.

41. Lawyers don't say something is "the same"; They say it is parimateria.

42. Lawyers don't say someone is "responsible"; They say he/she is liable.

43. Lawyers don't "explain" what they have said; They substantiate it.

44. Lawyers don't "tell lies"; They amend the facts! 

Appreciate a lawyer today!

Jumanne, 6 Agosti 2019

Some SWAHILI translations:πŸ™†πŸΎ‍♂️πŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎ

Some SWAHILI translations:🙆🏾‍♂️🙌🏾🙌🏾
1. Charger - kimemeshi
2. Remote - kitenzambali
3. Password - nywila
4. Akala (bladder shoes) - kirikiri
5. Passion fruit - karakara
6. Kangaroo - bukunyika
7. Fridge - jokofu
8. Juice - sharubati
9. Chips - vibanzi
10. PHD - uzamifu

11. Masters degree - uzamili
12. Degree - shahada
13. Diploma - stashahada
14. Certificate - astashahada
15. Keyboard - kicharazio
16. Scanner - mdaki
17. Flash disk - diski mweko
18. Mouse (for a computer) - kiteuzi
19. Floppy disk - diski tepetevu
20. Computer virus - mtaliga

21. Distillation - ukenekaji
22. Evaporation - mvukizo
23. Synthesis - uoanishaji
24. Oesophagus - umio
25. Greenhouse - kivungulio
26. Femur - fupaja
27. Germ cell - selizazi
28. Humus - mboji
29. Nector - mbochi/ntwe
30. Nutrients - virutubisho
31. Crystal - fuwele

32. Appetizers - vihamuzi
33. ATM - kiotomotela
34. Business card - kadikazi
35. Scratch card - kadi hela
36. Simcard - kadiwia/mkamimo
37. Memory card - kadi sakima
38. Microwave - tanuri ya miale
39. Mobile phone - rununu/rukono
40. Stapler - kibanizi

41. Laptop -kipakatalishi
42. Power saw - msumeno oto
43. Duplicating machine - kirudufu
44. Photocopier - kinukuzi
45. Cocktail party -tafrija mchapulo
46. Air conditioner - kiyoyozi
47. Calculator - kikokotozi
48. Lift - kambarau
49. Reaction - radiamali
50. Toothpick -kimbaka

Ijumaa, 5 Julai 2019

Jumatano, 26 Juni 2019

MAMBO YANAYO HAMASISHA MAHABA KWA MUME.

MAMBO YANAYO HAMASISHA MAHABA KWA MUME.

1 *KITANDA*
_*Mwanamke jitahidi kitanda chako kiwe vizuri NA cha kuvutui kipambe vizuri, kwa mashuka mazuri yenye nakshi, na shuka inyooke vizuri, sio kitanda kinakuwa kama  vile stoo ya nguo chafu.*_

2. *MANUKATO*
_*Katika chumba chako jitahidi sana, kiwe kinanuka kila Mara mumeo anapo rudi akiingia chumbani akutane na harufu nzuri, sio chumba chanuka jasho.*_

3. *USAFI*
_*Hili ni jambo la muhimu sana maana  utakuta chumbani kuna vyupi vya wiki nzima, hazijafuliwa mataulo chini, masidiria, mumeo akikuta chumba kiko hivo ujue unaondoa mvuto.*_

4. *USAFI WA MWILI.*
_*Pia usafi wa mwili, mwanaume anavutiwa na utakavokuwa umejipamba na atavutiwa kimapenzi na wewe sio vichaka, au mwiko unatoka na kutu, mwili anakutana na chumvichumvi kwenye ulimi wake sio sahihi jamani.*_

5. *KUJIPAMBA.*
_*Mke jipambe vile mume anapenda sio ulazimishe mapambo yako mfano piko huwa inawamaliza ipake au hina kachore viua, wanja, shanga, bangili, kipini, kikuku, marashi, UDI, na kusuka vile anapenda sio kutwa kushinda na janaba.*_

6. *MAPOKEZI MAZURI.*
_*Wanaume wanapenda sana kupokelewa vizuri, kwa mahaba tele mapokezi utakayo mpa mtu jitahidi yawe ya mahaba, legeza macho, mwili, yaani ili mradi tu umchanganye mwanaume, Siyo umeshupaa kma mwanajeshi kwenye paredi.*_

7. *CHAKULA*
_*Jitahidi mwanamke kujua kupika sio tu kupika michakula kama ya jela michukuchuku mibaya, mamchuzi chururu kama watoto wanapika.*_

8. *MITEGO*
_*Hii ni njia ambayo  watakiwa uwe mjanja ukimuona mumeo kakaa sebleni basi vaa hata shumizi jipitishe huku ukijitingisha Mara kwa Mara,ujue lazima atakutizama tu tena kwa mwendo nzuri wa maringo.*_

9. *MAPENZI*
_*Mapenzi si lazima kitandani tu popote  ni muhimu maana wengine mpaka  mume amwambie cheza basi.*_

10. *UKARIMU NA  KUJIPENDEKEZA KAULI TAMU.*
_*Hata kama kwenu ulizoea kuwa na domo kama bakuli la togwa jitahidi kuchunga mdomo ukiona huwezi mumeo ngoja aondoke ufunge mlango ubwatuke peke yako kaa chizi, akirudi funga upuuzi wako zungumza maneno mazuri mnyenyekee.*_

11. *MAKELELE*
_*Wanaume wengi huwa hawapendi makelele wanapenda wakirudi nyumbani kuwe kumetulia isiwe kma  choo cha umma, Wanaume wanapenda ukimya mahala panapokuwa kimya huzidisha mapenzi, sauti toa  kitandani mukifanya  tendonii na sio mida mingine.*_

12. *ZAWADI*
_*Jitahidi kumnunulia vizawadi  pindi unapokwenda sokoni au dukani mwanaume hujisikia faraja pale ukimpatia zawadi sio akupe wewe tu hata pipi.*_

13. *MAVAZI*
_*Pendelea kumchagulia mavazi tazama rangi ya mwili wake kisha mchagulie nguo inayoendana na rangi yake ya mwili  siyo mume mweusi waende kumvisha nguo nyekundu  kma anaenda kupunga mapepo  mamaa.!!!*

Mlale unono.... Mimi Bibi Sabry

Jumanne, 25 Juni 2019

KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI YA MTAA

*KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI YA MTAA.*

Katika kuchagua viongozi wa ngazi ya Serikali ya Mtaa, tafuteni Watanzania wenye sifa zifuatazo:

(i) *Awe mchapakazi* mwenye kujitoa sadaka kuwatumikia watu, hasa wananchi wa kawaida;

(ii) *Awe mwepesi* kuona, kusikiliza na kuguswa na shida za wananchi wake. Tena awe jasiri katika kupigania haki za wanyonge na awe na uwezo na ubunifu katika kutatua kero za wananchi hao;

(iii) *Awe mwadilifu*, anayechukia na kupiga vita rushwa na ufisadi kwa matendo;

(iv) *Anayetambua fursa* zilizopo katika eneo lake, kubuni mikakati ya kuwaendeleza wananchi anaowaongoza na kuwatia watu wake hamasa ya kuthubutu kutumia fursa hizo;

(v) *Awe mtetezi hodari* wa kulinda mazingira na mpambanaji dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi; 

(vi) *Mwenye kutoabudu nyadhifa*; anayetambua kuwa nafasi na vyeo tulivyopewa ni vya muda tu. Ni vya kupita! Thamani halisi ya kiongozi ni kufanya kazi kwa bidii na kuacha kumbukumbu nzuri kwa ustawi wa eneo analoliongoza na Taifa kwa ujumla; 

(vii) *Awe kama mchezaji mzuri* wa kiungo katika timu ya ushindi, anayetambua kwamba mkono mmoja hauwezi kupiga makofi ya shangwe;

(viii) *Awe mwenye kutambua kwamba kazi za kiongozi* zina maana sana kwa kuwa zinamwezesha kubadilisha maisha ya maelfu ya Watanzania, hasa wanyonge, kuwa bora zaidi;

(ix) *Awe na uwezo wa kuwaeleza wananchi kinaganaga* kuhusu Serikali yao inawapeleka wapi na wajibu wa kila mmoja ili waendelee kuiunga mkono; na

(x) *Awe anatoka ndani ya chama cha siasa(CCM)* kinachotetea maslahi na haki za wanyonge na chama hicho ni CCM!

Jumatatu, 24 Juni 2019

Mfahamu mnyama simba kiundani zaidi*

*Mfahamu mnyama simba kiundani zaidi*

Simba ni miongoni mwa wanyama ambao ni jamii ya paka, ukiondolea mbali kwamba ndiye mnyama mkubwa anayewinda katika jamii yao hiyo, lakini pia ni wanyama ambao hupenda kuishi katika makundi makundi, kwa lugha nyingine naweza sema wanaishi kifamilia kama ilivyo kwa binadamu, na familia zao huweza kuwa na simba takribani kumi na watano.

Njia rahisi ya kuwatambua kwa jinsia zao ni muonekano pamoja na majukumu, wakati simba dume shingoni likiwa limejaa manyoya Mengi, simba jike huwa na manyoya sawa mwili mzima, hapo ni kwa mtizamo wa namna wanavyoonekana.

Katika majukumu Simba hugawana, kazi ya kuhakikisha chakula cha kutosha kinapatikana katika familia hilo ni jukumu la simba jike, na simba jike aendapo mawindoni Jukumu lA simba dume ni kulinda mipaka tuu, uzito wa mnyama huyu huwa kati ya kilo 120 mpaka 240 inategemea na umri pamoja na afya.

Uhai wa simba kuishi ni kati ya miaka 10 mpaka 14 lakini kwa simba wa Africa hufika hadi miaka 17, Simba huanza kufundisha mbinu za uwindaji watoto wake tangu wakiwa wadogo kabisaa, ambapo huwatanguliza mbele na kuanza kuwabughuzi kwa kuwapiga piga ngwala, jambo ambalo hufanya watoto wake kuwa wenye hasira na wakali sana, na mbinu hizo ndio hutumia akiwa anawinda ukubwani.

Simba Mara zote hupendelea kukaa sehemu ambazo kuna miamba mizuri, pamoja na nyasi kavu kavu ambazo hufanana kwa mbali na rangi yake, kwakuwa huishi kifamilia dume ndio huanzisha makazi mapyaa, ambapo likiunguruma kwa sauti yake, sauti hiyo husafiri umbali mrefu sana na sehemu inayoishia ndio huwa mpaka wa makazi yao, na kama katikati ya sauti hiyo itakumbana na makazi ya simba wengine, basi dume jingine litaitikia, hapo kinachofuata ni simba hao kuhama lakini kama hawatakubaliana kutoka basi madume ya panda hizo mbili yatakutana kuoneshana ubabe na litakalokubali kushindwa litaondoka na familia yake.

Simba dume huchukia sana jike akizaa dume, hasira yake huja pindi anapoyafikiria madaraka, kwani hutambua jamaa hao ndio watakao kuja kumpindua ili wao ndio wawe watawala, hivyo chuki yake hukuwa kila watoto hao wanapozidi kuongezeka kimo, jukumu kubwa la kuyalinda madume hayo huwa chini ya mama yao, siku akizembea tuu Simba dume huvinyonga kikatili sana, mtifuano huo huwa hauishii kwa watoto tuu, hata Simba dume linapozeeka na kushindwa kutimiza majukumu yake kwa ustadi hufukuzwa kabisa na wanafamilia wenza na nafasi yake itachukuliwa na Simba dume ambaye anachipukia kwa wakati huo.

*Zifuatazo ndizo mbinu anazotumia simba kuwinda;*

1. Naweza sema ni mnyama pekee anayewinda kwa kutumia akili sana.

2. Ni ngumu kumuona awapo katika mawindo hasa hasa kiumbe anayewindwa.

3. Hana papara anapowinda na hutumia mahesabu makali, kwanza hutambua udhaifu wa anayemuwinda na baada ya hapo shughuri yake huanza, kama mnyama anayemuhitaji anauwezo mkubwa wa kunusa basi atacheza na upepo , kama anayemuwinda ana uwezo wa kuona mbali basi atajificha kwa ustadi sana.

4. Anayepanga kumkamata huangaika naye huyo huyo, hata kama kuna chansi ya kumkamata mwingine, simba hana tamaa na hii ni kwa sababu huofia kuharibu mahesabu ya washirika alionao katika mawindo.

5. Ni mkatili sana kwani kabla ya kumkamata windo lake cha kwanza anachokifanya ni kukiharibu kisaikolojia, ukishapaniki tuu ndio anakushughulikia.

6. Akiruka juu anapotua huongezeka uzito mara dufu, hufikia karibu kilo 300 sawa na mifuko 6 ya cement utupiwe kwa pamoja.

7. Tofauti na anapowawinda wanyama wengine akikuona mwanadamu huja kwa spidi huku mgongo wake akiupindisha kushuka chini, siku ikikutokea hali hiyo kumbuka hata kumtaja Mungu.

*Sifa zingine za mnyama huyu.*
1. Anapowinda unyayo wake huwa haugusi kabisa chini.

2. Simba ni mnyama mvivu pasina mfano, hutumia muda wake mwingi kupumzika hata kama hajachoka, takribani masaa 15 hadi 20 katika Masaa 24 hutumia kubadilisha mapozi tuu.

3. Pamoja na ukali wake wote lakini cha ajabu mnyama fisi ana uwezo wa kumnyang'anya chakula alichowinda.

4. Anapokula hapendi kabisa kelele na zikitokea kelele au harufu ambayo itamkera yupo tayali kuacha nyama aende zake.

5. Hali nyama ambayo hajawinda mwenyewe.

6. Ni mnyama ambaye anajiamini sana na anajiua kwamba anaogopwa sana.

7. Ni mnyama ambaye ana uwezo mkubwa wa kuona mbali, ikiwa ni pamoja na kusikia, uwezo wake humsaidia kuwinda wakati wowote ule anaojisikia iwe usiku au mchana.

Chakula apendacho samba.
Simba ni mnyama anayekula nyama tu, ule msemo wa kusema akikosa nyama anakula majani, hata fisi hafai kusingiziwa, simba ukiona anakula majani basi ni kwa sababu ana maumivu ya tumbo, chakula chake kikuu ni nyama na wanyama anaowapendelea sana ni pamoja na:
1. Nyati
2. Pundamilia
3. Nyumbu.
4. Mbuni
Nk.

*Pamoja kwamba Simba hujipatia kitoweo chake kwa urahisi sana, lakini baadhi ya wanyama humpa tabu sana nao ni kama wafuatao*.

1. Nyati kuna wakati wakichachamaa huweza hata kumuua simba asipowaingia kwa akili mkubwa.

2. Pundamilia hutumia vyema miguu yake ya nyuma kwa kukimbia pia kama silaha, simba wengi hupata majeraha sababu ya wanyama hawa.

3. Tembo pamoja kwamba wao ni hatari, lakini kushindwa kuwaangusha hata tembo wadogo tena wao wakiwa zaidi ya watano.

Ijumaa, 17 Mei 2019

MFAHAMU BRIAN DEACON MUIGIZAJI WA FILAMU YA YESU "

MFAHAMU BRIAN DEACON MUIGIZAJI WA FILAMU YA YESU " MIMI SIO YESU NI MUIGIZAJI TU"
Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi, ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon, ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.
Aliigiza filamu ya Yesu baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.
Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.
Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.
Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho
Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo.
Deacon anaeleza kuwa wakati wa kucheza filamu hii kuna mambo mengi sana yaliyofanyika ambayo yalileta kizaa zaa kwani baadhi wa washiriki walitaka kuleta vurugu baada ya kuchelewa kupata pesa yao.

Wakati wa kuchukua filamu hii Deacon alibandikwa nta puani ili kuboresha umbo la pua yake ili iendane na ile ya Wayahudi ambako ndio asili ya Yesu Kristo.
Deacon alipoangukwa msalabani alikuwa anajisikia maumivu kwa sababu kuna makosa yalikuwa yanafanyika na ikamlazimu kukaa pale msalabani kwa muda mrefu.
Hakupigiliwa misumari bali alishikizwa na kamba ambazo zilikuwa hazionekani.
Brian Deacon amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu.
Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.
Maisha yake ya kiroho
Baada ya kucheza filamu hii Deacon anasema ilimbadili sana kiroho. Aliamua kumfata Kristo.
BRIAN ANAWAAMBIA WATU WOTE DUNIANI KUWA YEYE SI YESU BALI YEYE NI MUIGIZAJI TU, WALA HAFANANI NA YESU KWANI ENZI ZA YESU HAPAKUWEPO NA TEKNOLOGIA YA CAMERA HIVYO HATA SURA HALISI YA YESU HAIJULIKANI ZAIDI YA WATU KUOTEA NA KUBUNI JINSI YESU ALIVYOFANANA KAMA DIRECTOR WAKE ALIVYOBUNI KWA DEACON
BRIAN PIA AMESHANGAZWA NA BAADHI YA WAUMINI KUWEKA PICHA ZAKE KWENYE MAJUMBA YAO NA KUVAA ROSARI ZENYE PICHA YAKE WAKIAMINI YEYE NI YESU KITU AMBACHO NI MAKOSA
AMESEMA ILI KUTHIBITISHA KUWA YEYE NI MUIGIZAJI TU AMEZITAJA filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985, The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.
Huyu ndie Brian Deacon mtu maarufu sana duniani kutokana na kucheza filamu ilitazamwa na mamilioni ya watu.

Share na wenzako wajue

UBARIKIWE NA BWANA