Jumapili, 11 Julai 2021

.. #MpeMwanafunziAjipime #MwalimuBahati

NASABA
Uhusiano wa kifamilia

Majina ya ukoo/nasaba
1. Mama/nina: Mzazi wa kike.
2. Baba: Mzazi wa kiume.
3. Kaka: Ndugu wa kiume.
4. Dada: Ndugu wa kike.
5. Nyanya/Bibi: Mama wa baba au mama.
6. Babu: Baba wa mama au baba.
7. Mjukuu: Mtoto wa mwana.
8. Kitukuu: Mwana wa mjukuu.
9. Kilembwe: Mwana wa kitukuu.
10. Kilembwekeza/kining’ina: Mwana wa kilembwe.

11. Ami/amu: Kaka wa baba.
12. Shangazi/mbiomba amati: Dada wa baba.
13. Mjomba/hau: Kaka wa mama.
14. Halati/hale: Dada wa mama bila kubagua kama ndiye mdogo au mkubwa kwa mama yako mzazi. Pia huitwa hale.
15. Mkazahau: Mke wa mjomba.
16. Mkazamwana: Mke wa mwana au mke wa mtoto wako.
17. Mavyaa: Mzazi wa kike wa mume.
18. Bavyaa: Mzazi wa kiume wa mume wako.
19. Mamamkwe: Mama wa mke.
20. Babamkwe: Baba wa mke.

21. Mcheja: Mzazi wa mke au mume (mkwe).
22. Kivyere : Jina wazazi wa mume na wazazi wa mke hutumia kuitana.
23. Mpwa: Mtoto wa ndugu. Yaani unayemwita ami, shangazi, mjomba na halati naye atakuita mpwa.
24. Mkoi: Mtoto wa shangazi, mjomba, halati.
25. Binamu: Mwana wa kiume wa ami.
26. Bintiamu: Mwana wa kike wa ami.
27. Shemeji: Ndugu wa mke au ndugu wa mume.
28. Mama wa kambo: Mama asiyekuzaa lakini anakulea.
29. Baba wa kambo: Baba asiyekuzaa
30. Umbu: Jina waitanalo kaka na dada. Ni jinsi kaka anavyomwita dada naye dada anavyomwita kaka wakiwa wamezaliwa na mzazi mmoja.

31. Ndugu mlungizi: Ndugu anayekufuata
32.Ndugu mlungizi: Ndugu anayekufuata nyuma.
33. Wifi: (a) Mke wa kaka. Iwapo wewe ni msichana, mke wa kaka yako utamwita wifi. (b) Dada wa mume: Iwapo msichana ameolewa dada wa mumewe atamwita wifi.
34. Mwamu/mlamu: a) Kaka wa mke. Mwanamume akioa, kaka wa mkewe atamwita mlamu. b) Mume wa dada: mvulana au mwanamume atamwita mume wa dadaye – mlamu.
35. Mwanyumba: Ni mwanaume mwenzako aliyeoa kutoka boma moja ulikooa wewe. Ni mume wa dada wa mke wako.
36. Mkemwenza/mitara: Jina wanalotumia wanawake walioolewa na mwanamume mmoja.
37. Kifungamimba/ kitindamimba/ mzuwanda: Mtoto wa mwisho kuzali- wa katika familia.
38. Mwanambee/kifunguamimba/kichinjamimba: Mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia.
39. Nyanyamkuu: Mama wa nyanya.
40. Babamkuu: Baba wa babu.

41. Maharimu: Mtu usiyeweza kumwoa au kuolewa naye kwa sababu ya uhusiano wa nasaba.
42. Mnuna: Ndugu anayenifuata ndugu mdogo.
43. Baba mkubwa - Ndugu wa kiume, mkubwa wa baba yako.
44. Baba mdogo - Ndugu wa kiume, mdogo wa baba yako.

.. #MpeMwanafunziAjipime #MwalimuBahati

logo

Viumbe na vikembe vyao (Young ones of animals in kiswahili )
The September 14 2018, on Elimika Nyumbani
Ng'ombe......................Ndama
Nzige...........................kimatu/maige/tunutu/matumatu/funutu
Ndege..........................Kinda
Kipepeo/nondo............kiwavi
Nzi..............................Buu
Farasi..........................Kitekli
Mamba....................... Kigwena
Nyangumi................... Kinyangunya
Fisi..............,.............. Kikuto/bakay
Ngamia....................... Nirigi/nirihi
Paka............................kinyaunyau/kipusi
Ndovu......................... Kidanga
Mbweha...................... Nyamawa
Nyani.......................... Kigunge
Kondoo....................... Kibebe/katama
Mbuzi..........................Kibui/kibuli/kimeme
Farasi na punda.......... Nyumbu
Punda........................ Kiongwe/kihongwe
Mbu............................kiluwiluwi
Chura......................... kiluwiluwi
Kuku.......................... Kifaranga
Papa.......................... Kinengwe

Alhamisi, 16 Januari 2020

MBUNGE WA ROMBO MR SELASINI AJIUZULU NAFASI YA MNADHIMU WA UPINZANI BUNGENI: Sasa msiseme ni njama za CCM.....

MBUNGE WA ROMBO MR SELASINI AJIUZULU NAFASI YA MNADHIMU WA UPINZANI BUNGENI:

Sasa msiseme ni njama za CCM.....

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesikitishwa na uamuzi wa Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini wa kujiuzulu nafasi ya Mnadhimu wa Upinzani Bungeni na kusema wazi sababu alizotoa hazina mashiko.

Mbowe ameshangazwa na taarifa ya Selasini kwamba hakuwahi kupewa Barua ya Uteuzi. Ameuliza, kama hakupewa barua ya uteuzi imekuwaje aandike barua ya kujiuzulu?.

Mbowe amesema, Selasini amekuwa Mnadhimu kwa miaka miwili, anaheshimiwa na Wabunge wote wa Upinzani huku akipewa ushirikiano wote na Ofisi ya Bunge, amekuwa akihudhuria Vikao vyote vya Kamati za Uongozi na kulipwa posho.

Kiongozi huyo Mkuu wa Upinzani Nchini ameonyesha wazi kutofurahishwa na uamuzi huo wa Mbunge Selasini na kusema labda kama ana mambo yake ya Siri ndiyo maana ameamua kufanya hivyo.

Mnasemaje wadau?😋😋🇹🇿

KOMBORA LA MTAMBO WA DR. BASHIRU ALLY KAKULWA Katibu mkuu CCM Taifa leo wilayani Tanga limesambaratisha ngome ya CUF wilayani Tanga baada ya Waheshimiwa Madiwani 8 kujisalimisha mikononi mwa kamanda wa vita Mhe. Katibu Mkuu Dr. Bashiru. *Madiwani hao ni* :-

KOMBORA LA MTAMBO WA DR. BASHIRU ALLY KAKULWA Katibu mkuu CCM Taifa leo wilayani Tanga limesambaratisha ngome ya CUF wilayani Tanga baada ya Waheshimiwa Madiwani 8 kujisalimisha mikononi mwa kamanda wa vita Mhe. Katibu Mkuu Dr. Bashiru.
*Madiwani hao ni* :-
1.Mhe. Mswahili Njama ( Chongoliani)
2.Mhe. Said Alei (Masiwani)
3.Habibu Mpa ( Ngamiani kati)
4.Mhe.Nassoro Salim (Tongoni)
5.Mhe.Akida Akida ( Ngamiani  kaskazini)
6.Mhe.Mwanasha Abdallah ( Viti maalum)
7. Mhe. Thurekha Mahadh (Viti maalum)
8. Mhe. Haniu Ally ( NAIBU MEYA JIJI LA TANGA - Tangasisi).

*VIONGOZI* *WENGINE* :
9.Mhe. Mambea Pashua (Mwenyekiti wa CUF wilaya na mkoa wa Tanga)
10. Mhe.Hidaya Ahamed (Kampeni meneja CUF).

Mhe. Bashiru amewambia wanaccm kuwa amefunga mitambo mikali Wilayani Tanga, kiasi kwamba imelazimika kuwa na VITUO VIWILI VYA KUPOZESHEA MITAMBO HIYO.  Kituo kimoja kimesetiwa Pangani na kingine hapa Tanga. Kwa hiyo ushindi wa jimbo la Tanga ni lazima katika jambo hili CCM haina utani.
Awali Mhe. Bashiru Ally jana  aliongea na kupata chakula cha pamoja na wazee nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa, na leo alitembelea ofisi ya CCM  wilaya ,  Mabalozi kata ya Majengo na kuzindua mpango wa vitambulisho kwa mabalozi wote wilayani. Na akatoa vitambulisho.
Aidha  katika uwanja wa mkwakwani alisikiliza wimbo maalum wa KIKUNDI CHA SANAA CCM ikiwa ni agizo lake na kukabidhiwa CD kama zawadi toka IDARA YA SIASA NA UENEZI wilaya ya Tanga.

Jumapili, 12 Januari 2020

#BARIADI :- DC BARIADI AMTEMBELEA MWANAFUNZILAMECK LUGEDENGA ALIEPATA A MASOMO YAKE YOT E TISA

#BARIADI :- DC BARIADI AMTEMBELEA MWANAFUNZILAMECK  LUGEDENGA ALIEPATA A MASOMO YAKE YOT E TISA

Festo Kiswaga- DC Bariadi,Leo nimemtembelea  kijana yohana lameck lugedenga aliyefaulu mtihani wa kidato  cha nne kwa kupata  A masomo yote tisa, kutoka  shule ya igaganulwa  kata ya dutwa wilaya ya Bariadi, mkoa wa Simiyu,  . Hapa ndio nyumbani kwao. Baba yake mzazi kijana huyo alimtelekeza  akiwa darasa la tano. Inasemekana alitokomea kusikojulikana kutokana na hali ngumu ya maisha lakini zaidi kukimbia majukumu ya kulisha familia yake. Hapa Chini ni nyumbani kwa mama yake Masalu  Lulyalya . Picha ya Kwanza ni mimi na kijana huyu mwenye akili sana maana hata mtihani wa form two  alipata A nane na B moja. Picha ya pili ni mimi na mama yake mzazi. Na picha ya tatu ni mimi, mama  yake pamoja na bibi yake Mbuke Limbu. Niliposikia historia ya familia hii initia hamasa sana na kumshukuru sana Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli kwa kuleta elimu bure maana taarifa ni kwamba kijana huyu hata uniform za shule kwa miaka yote alikuwa ananunuliwa na walimu wake kwa vile alijulikana kwa kuwa na akili nyingi sana. Je isingekuwa elimu bure ingekuwaje kwa watoto Hawa kutoka familia masikini . AHSANTE DR JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI kwa maono  ya hali ya juu kwa waTanzania wako Hawa. Yohana amexlelewa na mama yake pekee.

Ijumaa, 10 Januari 2020

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AWAPONGEZA UVCCM KWA KUENDELEA KUYAENZI MAPINDUZI YA ZANZIBAR KWA VITENDO

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AWAPONGEZA UVCCM KWA KUENDELEA KUYAENZI MAPINDUZI YA ZANZIBAR KWA VITENDO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika kilele Cha Matembezi ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ameipongeza UVCCM kwa Kuendelea kuwa Na Umoja na Mshikamano katika Shughuli mbalimbali za kukijenga Chama na Serikali.

Akizungumza katika Mkutano huo Mhe,Samia Suluhu amempongeza Mwenyekiti wa Umoja Wa Vijana Wa CCM Ndugu Kheri James na wasaidizi wake wote kwa namna Umoja huo ulivyo yaendesha matembezi hayo kwa kutoa michango ya nguvu kazi Katika maeneo mbalimbali ya kujenga Chama na Serikali kwa kujenga madarasa na Ofisi za Chama Cha Mapinduzi katika maeneo ambayo matembezi hayo yalikuwa yanapita.

Aidha, Katika Mkutano huo Mama Samia Suluhu amesema  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepiga hatua kubwa katika sekta mbalimbali  kutokana na misingi bora iliyowekwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar na Muasisi wa Mapinduzi Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,.

Mhe, Samia ameyasema hayo katika kilele cha kufunga matembezi ya Miaka 56 ya Maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar , ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yatakayo Tarehe 12 Januari 2020.

Amesema juhudi zilizochukuliwa na Muasisi huyo, zimeweka misingi bora ya upatikanaji wa masuala mbalimbali mfano katika Elimu nchini na kubainisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa elimu bure kwa wananchi wake pamoja na kuimarisha sekta hiyo kwa kuweka miundombinu bora ikiwemo kujenga Skuli za kisasa Zanzibar.

Ameongeza kuwa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Dk. Ali Mohammed Shein inajitahidi kuhakikisha watoto wote nchini wanapata elimu bora na katika mazingira bora kuanzia ngazi ya Maandalizi, Msingi na Sekondari ikiwa ni msingi wa kuendeleza malengo ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya kufuta ujinga kwa kuwapatia wananchi wake elimu bora.

Katika hatua nyengine, Mhe. Samia amewataka vijana nchini kutokubali kutumiwa  na watu wachache  wanaobeza Mapinduzi matukufu ya Zanzibar pamoja na juhudi hizo za Serikali badala yake waongeze bidii katika kusoma kwa manufaa yao na Taifa kwa jumla.

#Zanzibar
#Miaka56YaMapinduzi
#TogetherTunaweza
#MatembeziYaVijanaWaCCM