WATANZANIA VS WANA WA ISRAEL.
Na Thadei Ole Mushi.
Kilichowachelewesha wana wa Israel kufika nchi ya ahadi toka utumwani ni masikilizano tu. Kutoka Misri hadi Israel hazifiki KM 700. Lakini walitumia muda wa miaka 40 kufika Israeli. Musa alienda kuwaokoa akiwa kijana kabisa lakini alizeekea njiani na kufa kabla hajafika Israel. Kama walikuwa wanasikilizana wangetumia hata nusu ya mwaka wangefika. Lakini walikuwa wanafika mahali wanaanza kulaumiana,kugombana na hata kumkufuru Mungu kwa matendo yao.
NATAKA KUSEMA NN?
1. #Hili swala la Korosho wakati linaanzia Bungeni kwa wabunge wa kusini kulalamikia Fedha ya makato ya Korosho kutokurudishwa kwa wakulima Mimi nilichagua upande na nikasimama na kina Nape.
Wengine wakasimama na Mpango, wakati wa kuhitimisha kikao cha Bunge waliosimama na Mpango wakashangilia huku Mpango akijinasibu kuwa hakuna wa kumzuia kwenda Mtwara na Lindi.
Nikitahadharisha kuwa mjadala haukufungwa Bali utahamia mtaani watu hawakunielewa.
2. #Wakati Serikali inapiga Marufuku ununuzi wa Korosho kwa kutumia mtindo wa Kangomba niliibuka tena nikasema kuna watu watafilisika kwa kuwa hawa walikopa kwa ajili ya kuwa Middle Man katika biashara ya Korosho. Hakuna biashara isiyokuwa na Broker. Huu ni utaratibu wa kawaida kabisa kwenye biashara.
Tumefilis watu waliokuwa wanafanya biashara ya Kangomba na Bado Tumeshindwa kuimaliza Korosho na mkulima ameendelea kuteseka.
3. Sasa Tumehamia kwenye Indo Power, Ni Korosho ile ile iliyoanzia Bungeni Mwaka Jana.
Gazeti la Mwananchi Jana limeripoti kuwa Indo hawana Hata account bank. Kwa maana hiyo hawa hawana tofauti na waliokuwa wanafanya biashara ya Kangomba.
Kwa maana Rahisi tumekataa mabroker wakwetu Tanzania tukakubali mabroker toka Kenya.
Tatizo ni kutokusikilizana tu.
Tufike mahali Ndani ya Serikali tuwe na kitengo cha kuchuja michango ya watu mbalimbali. Si vibaya kukubali ushauri toka kwa upinzani.
Kazi kubwa ya Upinzani pamoja na kuwa wanaitaka Dola waiongoze lakini kazi yao nyingine ni kutoa mawazo mbadala. Tujenge utamaduni wa kuyaheshimu mawazo yao.
Ole Mushi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni