Jumatano, 20 Februari 2019

Teaching methods and classroom management.

Teaching methods and classroom management.

Uingiapo darasani kumbuka kuandika tarehe upande wa kulia juu ya ubao, gawa ubao x 3 na andika heading ya somo sehemu ya katikati juu ya ubao.
Andaa lesson plan vizuri ili iwe ni kiongozi wako kujuwa uliachia wapi na unaanzia wapi, haitakiwi kwa mwalimu kuwauliza wanafunzi KIPINDI KILICHOPITA TULIISHIA WAPI!! mwalimu wa namna hiyo inaonekana kabisa haandai lesson plan na inabidi afukuzwe kazi haraka Sana.

Mwalimu tumia sana njia ya kuwashirikisha wanafunzi katika kuelezea baadhi ya mambo LEARNER CENTERED ili kujuwa uwezo wa wanafunzi pia unaweza kwa njia hi kujifunza baadhi ya taaluma kutoka kwa wanafunzi.

Mwalimu uwapo darasani hakikisha kabisa unazima simu yako kwani ni makosa kwa mwalimu kupokea au kupiga simu wakati akiwa katika kipindi darasani kwani hii husababisha pia kutafuna muda wa kipindi ambao tayari umeshakadiriwa kwa kila dakika katika lesson plan.

Mwalimu unapokuwa darasani jitahidi kujuwa majina ya wanafunzi wote kwani haipendezi kumuita mwanafunzi WEWE.

Mwalimu uwapo darasani ni lazima ujuwe wanafunzi wenye akili sana na slow learners na unapofundisha wazingatie zaidi wale ambao uelewa wao ni mdogo.

Mwalimu uwapo darasani kuwa mcheshi na jenga urafiki na utani usiopindukia mipaka kwa wanafunzi wote wajenge wanafunzi wakuheshimu wasikuogope.

Mwalimu uwapo darasani epuka kuwakatisha tamaa wanafunzi waliokosea kujibu maswali au kushindwa kusomo vizuri Bali wapongeze sana kwa kujaribu na tumia njia bora ya kuwasahihisha.

Mwalimu uwapo darasani usichague wanafunzi haohao tu kujibu maswali hi inapelekea wengine kujiona hawana umuhimu.

Mwalimu unapomaliza kipindi darasani ni Bora kuwafahamisha wanafunzi topic ijayo ili wanafunzi wajiandae nayo.

Mwalimu uingiapo darasani hakikisha una teaching instruments kama chaki, rula, ufutio nk, epuka kuwatuma wanafunzi chaki na kadhalika kwani kufanya hivyo kunatafuna kipindi chako ambacho kimewekewa muda maalumu.

Kwa leo tuishie hapa tutaendelea Kesho Inshallah.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni