Jumanne, 4 Septemba 2018

SHAIRI KUHUSU WALIMU NA VIBOKO

Enyi  wenzangu walimu,
pole kwa haya mashaka,
Ule wetu umuhimu,
nchini umefutika,
Daima kutulaumu,
Kila kukipambazuka,
Walimu viboko sumu,
Tusichape ni mashaka,

Viboko sasa ni sumu,
Tusichape ni mashaka,
Ingawa hiyo nidhamu,
ya wanetu itashuka,
Kwa taifa hili bomu,
hatari likilipuka,
Walimu viboko sumu,
Tusichape ni mashaka,

Sisi ni wataalamu,
walimu siyo vibaka,
Walezi wenye elimu,
watu wa kuheshimika,
Kukosea si wazimu,
vipi tunadhalilika?
Walimu viboko sumu,
Tusichape ni mashaka.

Tusiache kujihimu,
Shuleni kuwajibika,
Iwe mwalimu wa zamu,
wa darasa kadhalika,
Wana tusiwahukumu,
Tukwepe kuwatandika,
Walimu viboko sumu,
Tusiwachape mashaka.

Watoto wanaharamu,
wale wasiyoonyeka,
Tusijipe kazi ngumu,
ya kuwafundisha nyoka,
Tumekuwa mahasimu,
Kundi liso thaminika,
Walimu viboko sumu,
Tusichape ni mashaka.

Kila kosa la mwalimu,
pale linapofanyika,
Yeyote huwa hakimu,
Makosa kuyabambika,
Tuelewe tufahamu,
Taifa limetuchoka,
Walimu viboko sumu,
Tusichape ni mashaka.

Malipo hii awamu,
nyongeza hawajaweka,
Maisha bado magumu,
pato halijanyanyuka,
Tukichapa washutumu,
Kwamba tumekasirika,
Walimu viboko sumu,
Tusichape ni mashaka.

Tumpe pole binamu,
Mwalimu alohusika,
Kwa ile adhabu ngumu,
Ajira kumponyoka,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni