*WANAFUNZI WETU WANAPOKARIBIA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA NI VIZURI WALIMU TUJIKUMBUSHE YAFUATAYO*
_*Mfumo mpya wa kutahini darasa la saba umebadilika, maswali sasa ni 45. Kila somo limetolewa ufafanuzi juu ya maeneo ya upimaji tamati na namna ya upimaji tamati huo utakavyokuwa. Leo tuanze na KISWAHILI*_
*Sehemu A: Sarufi*
Sehemu hii itakuwa na maswali ishirini (20) ya kuchagua Maswali yatajikita katika kubainisha aina za maneno, kutumia kwa usahihi aina mbalimbali za maneno, miundo ya sentensi na nyakati mbalimbali.
Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote katika sehemu hii kwa kuchagua jibu sahihi kutoka katika chaguzi A, B, C, D na E.
*Sehemu B: Lugha ya Kifasihi*
Sehemu hii itakuwa na maswali kumi (10) ya kuchagua. Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote.
Maswali katika sehemu hii yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi kutoka katika chaguzi A, B, C, D na E.
Maswali yatajikita katika mada ya methali, nahau na vitendawili.
*Sehemu C: Ushairi*
Sehemu hii itakuwa na maswali sita (6) ya kuchagua jibu lililo sahihi. Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote.
Maswali katika katika sehemu hii yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi kutoka katika chaguzi A, B, C, D na E.
Maswali hayo hayo yatajikita zaidi katika mada ya ushairi na tenzi
*Sehemu D: Utungaji/Uandishi wa Habari na Barua*
Sehemu hii itakuwa na sentensi nne (4) zilizochanganywa ambapo mtahinwa atatakiwa kuzipanga katika mtiririko unaoleta maana.
Maswali haya yatakuwa ya kuchagua sentensi sahihi kutoka katika chaguzi A, B, C na D.
Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote.
*Sehemu E: Ufahamu*
Sehemu hii itakuwa na maswali matano (5) na mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote.
Maswali yote yatakuwa ya kujaza nafasi iliyoachwa wazi.
Maswali yatajikita katika ufahamu wa kusoma habari.
*Mada Zitakazotahiniwa*
1 Sarufi
2 Lugha ya kifasihi
3 Ushairi
4 Utungaji/Uandishi wa Barua/Uandishi wa Habari
5 Ufahamu
Kesho tutapitishana kwenye somo jingine. Lengo hapa ni kuwakumbusha walimu kutunga mitihani hasa hii ya kujiandaa kwa kuzingatia mwongozo.
Ahsanteni sana
Moses Kyando
Mshauri wa Elimu
PPF House 6th Floor
0714414282
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni