Jumanne, 20 Machi 2018

Mabadiliko ya mtihani wa Taifa darasa la saba PSLE

YAH: MUUNDO MPYA WA MTIHANI WA DARASA LA VII(PSLE) KUANZIA MWAKA 2018
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania, leo tarehe 20/03/2018 ametangaza muundo mpya wa utungaji wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) kuanzia mwaka huu.Mabadiliko hayo ameyatangaza wakati anawasilisha mada ya TATHMINI YA UFAULU WA SHULE ZA SERIKALI NA ZISIZO ZA SERIKALI katika mkutano mkuu wa tano wa Maafisa Elimu Mkoa na Wilaya unaofanyika Dodoma.
Muundo mpya utakuwa kama ufuatao:
1.Kila somo litakuwa na maswali 45
2.Kati ya hayo ,maswali 40 yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi na 5 yasiyo ya kuchagua (yatakuwa ya kujieleza/kuonyesha njia na jibu nk)
3.Maswali 40 kila swali litakuwa na alama 1 na maswali 5 kila swali litakuwa na alama 2.
4.Majibu ya maswali 40 yatajibiwa kwenye OMR FORM na maswali 5 yatajibiwa kwenye karatasi maalum itakayoandaliwa.

Hivyo basi kutokana na mabadiliko hayo tarajiwa walimu wakuu anzeni kuwapima wanafunzi kwa kutumia muundo tarajiwa ili kuwajengea uzoefu.Upimaji huu uanze sasa katika mitihani yote kuanzia ngazi ya shule, kata, na kanda

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni