Jumanne, 20 Machi 2018

Jifunze kitu bureee hapa


___________________
Umeenda semina Dodoma, una ndugu yako kule. Unamtaarifu unakuja kumtembelea. Anakuambia karibu sana. Anakuelekeza panda daladala za Chamwino shukia St.Gaspar. Unashuka stendi unamkuta ndugu yako na mkewe na watoto stendi wamekuja kukupokea! Mnatembea kitambo na kufika kwake. Watoto waliobaki home wanakuja ulipokaa, wanakushika kichwani kukusalimia. Wakubwa kidogo wanakuja wanapiga magoti "shikamoo baba mkubwa!".

Wanakuzunguka kuulizia habari za ndugu zao unawasimulia, huyu std 2, huyu std 7, kaka yenu form 2. Ndani kumechangamka kila mtu yuko engaged nawe in one way or another.
Mama anahangaika na msichana kukuandalia chakula. Baada ya muda mke wa mdogo wako anakuja kupiga magoti kukuambia karibu chakula. Unaenda mezani, anakuja kukunawisha mikono huku akisema "tusamehe shemeji mboga zenyewe hivyo hivyo.." Unakula unashiba.

Baadaye unaaga. Nyumba nzima wanafunga, wanakusindikiza hadi kituoni. Watoto wanakuaga, "ba mkubwa msalimie Jerry na Irene. Ukija tena uje nao" Unaondoka kwa heshima zote.

Siku ya siku nduguyo naye kapata kitrip cha Dar. Anakuambia nakuja kukutembelea. Unamwambia tumehamia kwetu Mbezi panda mwendokasi hadi mbezi mwisho. Anafika anakupigia, unasema kuna bodaboda hapo mpe niongee naye. Unaongea na boda "huyo jamaa mlete kwangu geti linatazamana na kituo cha afya cha Mbezi, lina waya za umeme juu".

Anafkishwa. Anagonga kengele, mko ndani familia, unaagiza housegirl, "si mnasikia kengele? Kafungueni geti" Housegirl anaenda kufungua. Ndugu yako anaingia sebleni anawakuta. Anawasalimu unaitikia marahaba, we mkubwa! Mkeo anaangalia tamthilia kakaa chini. Anageuka, karibu shemeji, za siku! "Nzuri". Amemaliza, anaendelea na tamthilia yake.

Wanao wanacheza game kwenye computer hata hawajashituka kuna mtu kaingia. Unawaambia, nyie msalimieni baba yenu mdogo. Wanatupia shikamoo bila hata kumuangalia usoni, game limekolea!

Mnazungumza kigogo, unamuuliza habari ya Dodoma. Kabla hajakujibu unashika simu unaanza kuchat, mke wako naye anachat! Sitting room imejaa watu, lakini kila mtu kama hayupo vile. Mara housegirl anawakaribisha chakula. Mama anapokea "shemeji karibuni chakula"

Unamgeukia mdogo wako unamwambia "aisee we jitegemee, hapa kima mtu anakula kwa wakati wake.!". Mgeni anainuka kwenda kupambana na meza peke yake. Maji ya kunawa hakuna! Bahati nzuri dada wa kazi anakatiza, anaulizwa maji yakunawa, anajibu kanawe pale kwenye "Hw basin" maji yanatoka!

Anaenda kunawa kinyonge. Anakula peke yake, anamliza na kurudi sitting room. Mnaongea issues kidogo za kifamilia na wazazi kijijini. Muda unafika wa ndugu kuaga. Unamwambia subiri kidogo. Unapiga kwa boda boda. Anakuja, unatoa elfu kumi unampa,  unamwambia chukua hii utalipa hiyo bodaboda.

Boda inafika, ndugu yako anaaga, unasimama unamtoa hadi mlangoni. Wanafamilia wengine wanaagia sitting room bila kuinuka. Mama bado yupo busy na simu anachat. Watoto game limekolea, hawataki kutoa macho kwenye computer. Ndugu yako anawaaga hata hawamuangalii usoni. Wanatupia kwa mbaali "kwa heri ba mdogo" wanaendelea na game. Ndugu anakamata mchuma na kuondoka.
____
Wengi tunaoishi mijini tuna maisha ya aina hii, na tunaona ni sawa. Tunajifanya tupo busy kwenye mambo yasiyo na msingi na kupuuza utu wa wengine. Hata watoto wetu tunawalea ktk mazingira ya kuthamini zaidi vitu kuliko utu. Hii si sawa hata kidogo. Tuwatendee wengine kama tunavyotaka kutendewa.

Mabadiliko ya mtihani wa Taifa darasa la saba PSLE

YAH: MUUNDO MPYA WA MTIHANI WA DARASA LA VII(PSLE) KUANZIA MWAKA 2018
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania, leo tarehe 20/03/2018 ametangaza muundo mpya wa utungaji wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) kuanzia mwaka huu.Mabadiliko hayo ameyatangaza wakati anawasilisha mada ya TATHMINI YA UFAULU WA SHULE ZA SERIKALI NA ZISIZO ZA SERIKALI katika mkutano mkuu wa tano wa Maafisa Elimu Mkoa na Wilaya unaofanyika Dodoma.
Muundo mpya utakuwa kama ufuatao:
1.Kila somo litakuwa na maswali 45
2.Kati ya hayo ,maswali 40 yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi na 5 yasiyo ya kuchagua (yatakuwa ya kujieleza/kuonyesha njia na jibu nk)
3.Maswali 40 kila swali litakuwa na alama 1 na maswali 5 kila swali litakuwa na alama 2.
4.Majibu ya maswali 40 yatajibiwa kwenye OMR FORM na maswali 5 yatajibiwa kwenye karatasi maalum itakayoandaliwa.

Hivyo basi kutokana na mabadiliko hayo tarajiwa walimu wakuu anzeni kuwapima wanafunzi kwa kutumia muundo tarajiwa ili kuwajengea uzoefu.Upimaji huu uanze sasa katika mitihani yote kuanzia ngazi ya shule, kata, na kanda

Alhamisi, 8 Machi 2018

MLOGANZILA

Ahamisi, 08 Machi 2018 03:58

MLOGANZILA YAPOKEA MSAADA WA DAWA.

Serikali ya Korea leo imeikabidhi msaada wa dawa zenye thamani ya Shilingi Milioni Mia Moja kwa Serikali ya Tanzania

ikiwa ni ishara ya mahusiano mazuri kati ya nchi hizo mbili.

Msaada huo umekabidhiwa kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako jijini Dar es Salaam ili zitumike katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS) Kampasi ya Mloganzila.

Mara baada ya kupokea msaada huo Waziri Ndalichako ameishukuru Serikali ya Korea kwa msaada huo na kuwataka wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho kutumia vema miundombinu ya Chuo kwa kujifunzia na kufundishia ili kujijenga kitaaluma kwalengo la kumaliza tatizo la uhaba wa Madaktari na Wataalam wa Afya hapa nchini.

Akizungumza mara baada ya makabidhiano ya dawa hizo Kiongozi wa Ujumbe wa Korea wa Kamati ya Afya na Huduma za Jamii ya Bunge la nchi hiyo, Jun Hey Sook amesema msaada huo wa dawa ni ushirikiano katika kuboresha sekta ya Afya.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano serikalini,

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

VYUO VINAVYOTAMBULIWA NA SERIKAL

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WAOMBAJI WA MAFUNZO KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA NGAZI ZA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MUHULA WA MACHI/APRILI, 2018

Date Posted: 8th March 2018 17:16:38 Posted By:NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION

 

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

(NACTE)

 

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WAOMBAJI WA MAFUNZO KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA NGAZI ZA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MUHULA WA MACHI/APRILI, 2018

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoundwa kwa Sheria ya Bunge, Sura ya 129, kwa lengo la kusimamia mafunzo yanayotolewa katika Vyuo vinavyotoa mafunzo kwa ngazi za Astashahada, Stashahada na Shahada ambavyo si Vyuo Vikuu ama Vyuo Vikuu Vishiriki nchini.

Jukumu mojawapo la Baraza, ni kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa katika Vyuo  vya Elimu ya Ufundi yanakidhi vigezo na ubora unaohitajika katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Kwa muktadha huo, Baraza liliendesha zoezi la uhakiki wa Vyuo vinavyotoa elimu na mafunzo ya ufundi  kuanzia tarehe 27 Julai hadi tarehe 6 Septemba, 2017. Lengo kuu lilikuwa ni kuhakiki ubora wa mafunzo yanayotolewa pamoja na kubainisha changamoto zinazovikabili Vyuo hivyo katika utoaji wa mafunzo.

Katika uhakiki huo, Baraza lilibaini kuwa, baadhi ya Vyuo vilikidhi viwango vya ubora kwa mujibu wa taratibu za Baraza.  Hata hivyo, baadhi ya Vyuo vilibainika kuwa na changamoto mbalimbali zinazoweza kuathiri ubora wa elimu na mafunzo yanayotolewa.  Kufuatia zoezi hilo, Vyuo vyote vilivyobainika kuwa na mapungufu vilitaarifiwa na kutakiwa kurekebisha mapungufu yaliyobainishwa kabla ya kuendelea na udahili wa wanafunzi kwa mwaka mpya wa masomo 2018/2019.

Hivyo basi,  Baraza linautaarifu umma na waombaji wa nafasi za mafunzo kwa ngazi za Astashahada na Stashahada kwa muhula wa masomo wa Machi/Aprili, 2018 kuomba kwenye Vyuo vilivyokidhi ubora ambavyo vimeorodheshwa kwenye tangazo hili.

Aidha, Baraza linaelekeza kwamba Vyuo ambavyo havipo kwenye orodha iliyoambatanishwa hapavisidahili wanafunzi katika muhula wa masomo wa Machi/Aprili, 2018 bila kupata kibali cha Baraza kama ilivyoelekezwa.

Pia, Baraza linakumbusha kuwa udahili wa Muhula wa Machi/Aprili, 2018hauhusishi programu zote za Kada ya Afya na Ualimu.

Kuona orodha ya vyuo vinavyokidhi vigezo bonyeza hapa

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE : 8 Machi, 2018

#Inawezekana

ondoa sumu katika mwili wako kwa kupitia picha hizi hapa kutoka kwenye akaunti yangu

#Inawezekana

#Inawezekana

#Inawezekana

Ijumaa, 2 Machi 2018

WALE WAKALI WA HISABATI

KAMA ULIKUWA AU KWA SASA NIMKALI JE UBONGO WAKO UMESHAGUNDUA JIBU LA SWALI HILI

KUMI NA SITA EUROPA

WATIZAME HAPA WANAOCHEZA SIKU YA ALHAMIS KAMA TIMU YAKO NI MOJAWAPO

itizame hapa top 4 ya

je timu yako unayoipenda umeiona top 4???

MATOKEO YA SIMBA

WAFUNGAJI WA MAGOLI NIMEKUWEKEA HAPA PIA

LIGI KUU VPL

ITAZAME HAPA TIMU YAKO ITACHEZA NA TIMU GANI

BIG MATCH BARANI ULAYA

england, germany, italy, spain n.k hizi hapa

MITIHANI SHULE UA MSINGI

MAARIFA YA JAMII, HISABATI, SAYANSI NA KIINGEREZA

123